Hongera CCM mpya na Halisi kwa Ushindi Mzito; ni salaam tosha kwa Chadema na Mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hongera CCM mpya na Halisi kwa Ushindi Mzito; ni salaam tosha kwa Chadema na Mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mr Emmy, Oct 29, 2012.

 1. M

  Mr Emmy JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,201
  Likes Received: 289
  Trophy Points: 180
  Ushindi Mzito wa zaidi ya 95% asilimia katika chaguzi ndogo ni ishara tosha kuwa CCM Halisi imedhamiria kukijenga chama katika ngazi ya matawi na mashina na hivi karibuni mapinduzi makubwa yatafanyika katika ngazi ya Taifa.

  Hongereni wana CCM wote na Wananchi wote wapenda amani na maendeleo kwa kuifanya CCM mpya kuendelea kuwa Chaguo lenu la kwanza katika kuongoza dola na kuleta maendeleo.

  CCM Halisi haijutii kupoteza au kushindwa katika kata za Udiwani za Daraja Mbili Arusha, Rombo,Mtibwa kwani Mafisadi wanaopigwa vita na CCM Halisi walisimamisha watu wao kwa malengo yao binafsi ikiwa ni pamoja na kukihujumu chama kwa mfumo wa kisayansi na kukipa maujiko chama pinzani cha chadema kwani wao lao ni moja. kwa maana hiyo tunapenda kuwapa pole wananchi wote wakata hizo kwa kuingizwa katika mitego ambayo hawakuigundua mapema.

  CCM mpya na halisi itafika katika kata hizo na kufumua uongozi kuanzia ngazi ya shina na tawi na kutoa elimu ya siasa na maendeleo kwa wananchi hao.
   
 2. a

  aduwilly JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 1,182
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Jaribu kuwa mzalendo hata kama unanufaika na CCM, oneo huruma maelfu ya wanawake na watoto wanaoteseka kwenye nchi hii inayobubujika maziwa na asali kutokana na utawala mbovu wa CCM, kama hao huwahurumii, hurumia mamilioni ya wanaume wanaoishi maisha ya kubahatisha kwenye nchi yao wenyewe kutokana na utawala usokuwa na utu wala usawa wa Chama Cha Mapinduzi.

  Mchezo wenu, mauti yetu watanzania wenzenu
   
 3. zenmoster

  zenmoster JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 953
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  huyu mrs Emmy anajitafutia umaarufu tu hapa....acha shobo we mwanaume bwana.. CCM mpya ina mwenyekiti mpya mbona kikwete bado mwenyekiti...bado ccm ni ile ile yenye malengo haya
  1.KUDUMISHA UMASIKINI
  2.ELIMU DUNI ama KUTOKOMEZA ELIMU
  maana ndo mtaji wenu wa kura tu...
   
 4. sifongo

  sifongo JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 4,597
  Likes Received: 2,408
  Trophy Points: 280
  Umemuambia ukweli mkuu na yeye anajua hilo ila atajifanya hajaelewa, ubinafsi ni hatari kuliko tunavyodhani la msingi kwake ni yeye ashibe wengine hata wakifa njaa haimuumi........NDIO CCM YA LEO.
   
 5. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,818
  Likes Received: 36,916
  Trophy Points: 280
  Tangu unyimwe pesa ya rushwa kwenye uchaguzi wa uvccm umepatwa na jazba kama kunguru aliyenyonyolewa manyoya.

  NB: weka mbali na watoto.


  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
 6. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,481
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  CCM mpya ina mwenyekiti mpya na anasema hivi "WAKIWAPA RUSHWA POKEENI LAKINI MSIWACHAGUE'' hapo vipi mkuu au mna mwenyekiti mwingine? tutajie kama yupo tumjue.
   
 7. u

  ungonella wa ukweli JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 4,227
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kimsingi wa kupongezwa ni vyama vya upinzani.mazingira ya uchaguzi kushinda tanzania ni magumu sana hata kama wananchi wana hamu ya kufanya mabadiliko, matumizi ya vitisho,fitina,kujeruhi wafuasi wa upinzani yamekuwa kawaida kwa wapinzani. Ccm inacheza rafu nyingi sana wakati wa uchaguzi mfano juzi shinyanga raia wamejeruhiwa.kwa hali hii watanzania wenzangu tuwe tayari kuona mengi ya kutisha kwa taifa letu yakifanywa na ccm 2015 ili kubaki madarakani.
   
 8. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  LKN JAMANI SAFARI YA KUIKOMBOA II NCHI BADO NI NDEFU SANA, IZI KURA NAONA KM ZINAPIGWA KWA HILA NA KUWAKOMOA BAADHI YA WATU ILI WAENDELEE NA HALI YA UFUKARA, EBU WAFIKILIE WATU WA MSALATO, BUMBULI, GEITA NK, WATU NI UKO MAFUKARA KUPINDUKIA, WENGINE WANAISH KWA KULA UBUYU, SJUI WANAITOA WAPI NGUV YA KUVOTE 4CCM NA CCM HII NDO INAYOWAPA MAISHA AYA BATILI, MISELABLE LIFE, NATMAI ELIMU YA URAIA AIJAFIKA UKU JAPO NAJIPA MOYO NIKIANGALIA TOFAUT YA KURA KT YA CCM NA CDM NI NDOGO ATA UKO VJIJIN LABDA KIPIND KJACHO MABADILIKO YATAKUWEPO, AU YANAZIDI KUSOGEa MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 9. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  WEWE NDUGU NI MSHENZ, USOKUWA NA ADABU, HUNA HURUMA WEWE, IVI UMEWAI KWENDA JAPO MSALATO UKAONA MAISHA YA WATU WA UKO? HUNA ADABU WEWE, UNAWAKEBEI MAFUKARA, UYO ALOKUTUMA UANDIKE UOZO HUU NAE ATAKUA HANA ADABU KM WEWE, HUJUI KUWA KUNA WATU NDG ZETU, WATZ WENZETU WANAKULA MLO MMOJA, WANAISHA KWA KULA UBUYU, ACHA KUWAKEJELI WE MDHAMBI MKUBWA, TUMEFIKISHWA KT HATUA II NA CCM, WKT WATU TUKO KUZIMU WENZETU CCM WAKO PEPONI, NDO UNAPONGEZA ILO. UNA LAANA WEWE C BURE, ALOKUPA IYO GUT YA KUPONGEZA MFUMO WA KIFISADI RIL ATAKURAHANi
   
 10. MKANDYA

  MKANDYA Senior Member

  #10
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 12, 2009
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mleta mada, mbona kimahesabu ccm haijashinda kwa asilimia 95 kama unavyotaka tuamini.
  Viti vilivyopigombewa ni 29. ccm imepata 23 kihesabu ni 23/29 X100= 79.3 (79.3%); hii ndiyo asilimia ya viti vyote.
  Kama ccm ilikuwa inatetea viti 26 na imepata viti 23 kimahesabu imepoteza viti 3 kiasilimia itakuwa imepoteza 3/26 X100=11.53 (11.53%). Hivyo usituletee hesabu za kufikirika, na hili ni pigo kwa ccm kwani, unaponyang'anywa kiti hata kimoja jaribu kujiuliza kulikoni! Kuliko kubaki ukijisifia, wakati umepoteza, au ccm haikuvitaka hivyo viti ilivyokuwa inavikalia;na sasa imenyang'anywa??
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145

  UNAIITA MPYA kwasababu WANA VIFURUSHI vya KUHONGA Wananchi na Wachaguzi?
  Tangu Lini UKAONA VIONGOZI wana PESA kuliko hata kizo WILAYA wanazogawa?
   
 12. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,493
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ni hatari kwa ustawi wao
   
 13. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,141
  Trophy Points: 280
  CCM Mpya, CCM ya zamani, CCM ya mafisadi???? CDM??? mbona unajichanganya? CCM imeoza, ccm imezeeka beyond repair hata mngeipa majina mazuri kiasi gani.............
   
 14. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hivi wanapiga kura ni kina nani? yaani mtu uonee huruma watu ambao ndio wanakipenda hicho chama? wajionee huruma kwanza kabla ya kuonewa huruma!
   
 15. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Kwa mtu makini akifanya tathmini ya kina atabaini ya kwamba CCM imeendelea kupoteza mvuto wake kwa wapiga kura. Kwa mfano CCM imepoteza viti vitatu ilivyokuwa inavishikilia wakati CHADEMA imefanikiwa kuvitetea viti vyake viwili na pia imefanikiwa kuviongeza viti vitatu zaidi. Kwa hiyo CHADEMA imezidi kung'ara kisiasa wakati CCM ikizidi kufa. Ni brain dead idiot pekee atakayefurahia ushindi wa CCM!
   
 16. isambe

  isambe JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 2,053
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  Kama ni mpya badilisheni na bendera,halafu wote muwe hamna vtambi,hapo ndio nitaamini kwamba the time has come!
   
 17. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wakishinda tusiwapongeze?
   
 18. GOOGLE

  GOOGLE JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 1,876
  Likes Received: 713
  Trophy Points: 280

  Hivi CCM bado ipo? kama bado ipo nawashauri waivunje kabisa afu wanachana wadisolve kwenye vyama vigine,,, najua hata hiyo CCM mpya na halisi ni yaleyale,,,, nakumbuka wakati wanavua magamba yao walisema wanaisuka upya lakini magamba na maganda bado yapo.
   
 19. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,812
  Likes Received: 2,584
  Trophy Points: 280
  Zitto;chadema yaelekea kushinda zaidi ya nusu viti vya udiwani. What went wrong? Dumbfounded i, now find true, ukombozi wa Mtanzania ufunguo Zanzibar.
   
 20. G

  Godie Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Wasomaji,

  Hakika takwimu hizo zinahitajika sana kwetu sisi wasomaji. Ningetamani tungepata orodha ya kata mabazo kulikuwa na uchaguzi wa madiwani, katika hayo tujue chama kipi kilikuwa kinashikilia udiwani wa kata hiyo kabla ya uchaguzi. Zaidi ya ya hapo taarifa za kuwa kata hiyo ipo mjini au kijijini ni vema kujulikana ili kutupa mwanga wa elimu ya kiuraia waliyo nayo wananchi wa eneo husika. Haya yakiwekwa wazi tutakuwa katika mazingira mazuri yakujua nini tutarajie kwa uchaguzi wa 2015, hii ni muhimu sana wasomaji wenzangu.
   
Loading...