ComputersDAR
JF-Expert Member
- Jan 21, 2013
- 213
- 242
Jana niliamua kutembelea hii bar maarufu maeneo ya Shekilango. Nikaagiza makange ya kuku na ugali. Baada ya kuonja ile paja la kuku nikasikia ladha ya kitu kilichooza. Na baada ya kunusa nikagundua ni kweli ile kuku ilikuwa imeharibika. Nilimwita wiater nikamweleza. yeye akaenda kwa supervisor wake ambaya kwa kiffupi hakujali kama ile nyama imeharibika yeye tatizo lake ni kwambanilipe elfu 6 bei kamili kwa kile chakula kwa vile nilishakionja! Ma waiter wawili, supervisor na mdada mooja mnene wote wakawa wanang'ng'ania nilipe. Nililipa lkn sitakwenda tena ile bar. Nawasihi wandugu muwe waangalifu sana sehemu hii wanauza nyama iliyooza na inaonekana wanafanya makusudi kabisa