Hongera Bar -Shekilango- Wanauza Kuku Waliooza

Hongera Bar -Shekilango- Wanauza Kuku Waliooza

yalishamkuta jamaa yangu siku moja tulienda hapo mchana. alikataa kulipa. akasema kama mnanilazimisha kulipa ni mpaka mtu wa TFDA aje hapa na wa serikali ya mtaa washuhudie. wahudumu hao hao ulowadescribe wakaondoka na chakula chao kimya kimya. tatizo la waafrika tunakubali sana kufa na tai shingoni. unauziwa kuku kaoza we bado unalipa. kama kulianzisha wamelianzisha wao. sasa kama wanawalipa wana zirro wa hapo karibu peleka kabisa ITV
Ilishanitokea hapo nliletewa mchemsho wa samaki una mende nashukuru ilikuwa saa tano asubuhi nusu nirushe ngumi sikulipa

sent from my BlackBerry keyone using JamiiForums mobile app
 
Jana nimepita Bar moja maarufu nikaagiza Chips na nusu kuku, nikala kuku nikamaliza sasa wakati namalizia chips nikakuta nzi. Nzi anaonesha kaiva vizuri kabisa. Nikamwita mhudumu nikamwambia naona mnaunga chips zenu na nzi sasa silipi. Akaniomba nilipie kuku nisilipe chips, nikamwambia silipi hata shilingi muite meneja wako hata polisi. Na niliondoka bila kulipa.
 
Pole sana mkuu. Ila maeneo au bar nyingi za aina hiyo huwa tunakula matakataka sana. Kuna sehemu maarufu sana maeneo ya kinondoni makaburini huwa wanapika mchemsho mzuri (Samaki na Kuku). Huwa nikipita pale napendelea kupiga mchemsho wa sato. Siku hiyo samaki waliwahi kuisha mapema. Nikaona niagize mchemsho wa kuku wa kienyeji. Hotpot ilipowasili mezani nikapakua kwenye kibakuli na kuanza na paja. Kwanza nyama ilikuwa ngumu halafu ilikuwa na kishombo fulani hivi kwa wafugaji kuku wa mayai wananielewa hapa. Nikamuita jamaa wa jikoni (incharge) ni mshikaji. Nikamuambia moja kwa moja mbona umeniletea mezani kuku wa mayai badala ya kuku wa kienyeji. Akanijibu pole sana mkuu,kuna dogo jikoni ndio katengeneza hiyo. Akachukua hotpot akarudi nalo jikoni,baada ya nusu saa akarudi na kuku wa kienyeji fresh.
Tuwe makini sana na sehemu tunazokula nje ya nyumbani. Mimi binafsi huwa natengeneza urafiki na watu wa jikoni...nawapiga na bapa siku moja moja wanaenda na mimi sawa. Kuku choma wakiwa hovyo anakushtua,leo boss kuku sio piga samaki au mbuzi. Wakati huo huo unaona meza nyingine kuku wanaenda kama kawaida.
Penye uzia tembeza rupia sio?
 
kwa dunia hii ya leo kitoweo/chakula pekee unachoweza kuwa na hakika nacho ni kile ulichochinja na kupika mwenyewe. Tofauti na hapo ni kujipa moyo tu kuwa unakula kilicho safi. Maana unaweza kuona kuku akichinjwa lakini aliyepika kamasi limeangukia bahati mbaya, hawezi kukwambia na wewe huwezi kujua. Usilolijua halina madhara.
 
Jana niliamua kutembelea hii bar maarufu maeneo ya Shekilango. Nikaagiza makange ya kuku na ugali. Baada ya kuonja ile paja la kuku nikasikia ladha ya kitu kilichooza. Na baada ya kunusa nikagundua ni kweli ile kuku ilikuwa imeharibika. Nilimwita wiater nikamweleza. yeye akaenda kwa supervisor wake ambaya kwa kiffupi hakujali kama ile nyama imeharibika yeye tatizo lake ni kwambanilipe elfu 6 bei kamili kwa kile chakula kwa vile nilishakionja! Ma waiter wawili, supervisor na mdada mooja mnene wote wakawa wanang'ng'ania nilipe. Nililipa lkn sitakwenda tena ile bar. Nawasihi wandugu muwe waangalifu sana sehemu hii wanauza nyama iliyooza na inaonekana wanafanya makusudi kabisa


Usikute umelishwa kunguru maana pale kunguru ni wengi mno na wale wachagga wameweka pesa mbele sana kuliko afya za wateja wao.
 
Jana niliamua kutembelea hii bar maarufu maeneo ya Shekilango. Nikaagiza makange ya kuku na ugali. Baada ya kuonja ile paja la kuku nikasikia ladha ya kitu kilichooza. Na baada ya kunusa nikagundua ni kweli ile kuku ilikuwa imeharibika. Nilimwita wiater nikamweleza. yeye akaenda kwa supervisor wake ambaya kwa kiffupi hakujali kama ile nyama imeharibika yeye tatizo lake ni kwambanilipe elfu 6 bei kamili kwa kile chakula kwa vile nilishakionja! Ma waiter wawili, supervisor na mdada mooja mnene wote wakawa wanang'ng'ania nilipe. Nililipa lkn sitakwenda tena ile bar. Nawasihi wandugu muwe waangalifu sana sehemu hii wanauza nyama iliyooza na inaonekana wanafanya makusudi kabisa
Next time omba risiti kisha waambie unaondoka na chakula chako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom