Pole sana mkuu. Ila maeneo au bar nyingi za aina hiyo huwa tunakula matakataka sana. Kuna sehemu maarufu sana maeneo ya kinondoni makaburini huwa wanapika mchemsho mzuri (Samaki na Kuku). Huwa nikipita pale napendelea kupiga mchemsho wa sato. Siku hiyo samaki waliwahi kuisha mapema. Nikaona niagize mchemsho wa kuku wa kienyeji. Hotpot ilipowasili mezani nikapakua kwenye kibakuli na kuanza na paja. Kwanza nyama ilikuwa ngumu halafu ilikuwa na kishombo fulani hivi kwa wafugaji kuku wa mayai wananielewa hapa. Nikamuita jamaa wa jikoni (incharge) ni mshikaji. Nikamuambia moja kwa moja mbona umeniletea mezani kuku wa mayai badala ya kuku wa kienyeji. Akanijibu pole sana mkuu,kuna dogo jikoni ndio katengeneza hiyo. Akachukua hotpot akarudi nalo jikoni,baada ya nusu saa akarudi na kuku wa kienyeji fresh.
Tuwe makini sana na sehemu tunazokula nje ya nyumbani. Mimi binafsi huwa natengeneza urafiki na watu wa jikoni...nawapiga na bapa siku moja moja wanaenda na mimi sawa. Kuku choma wakiwa hovyo anakushtua,leo boss kuku sio piga samaki au mbuzi. Wakati huo huo unaona meza nyingine kuku wanaenda kama kawaida.