Hongera Aveva, Kaburu, Said Tuli

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,761
Katika uchaguzi huo matokeo ya awali
yalikuwa yakionyesha kuwa, Evans Elieza
Aveva, alikuwa akiongoza kwa kujizolea
jumla ya kura 1452 kati ya 1845
zilizopigwa na kutoa matumaini kwa
wapiga kura wake ya kuibuka kidedea
katika uchaguzi huo.
Mpinzani wake Andrew Tupa, hadi
tunakwenda mitamboni alikuwa
amejinyakulia jumla ya kura 387 wakati
kura sita zimeharibika. Hata hivyo,
matokeo rasmi ya uchaguzi huo
yatatangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya
klabu hiyo chini ya Mwenyekiti Dk Damas
Ndumbaro baadaye.
wakati huo Geoffrey Nyange 'Kaburu'
ameshinda Umakamu wa Rais Simba SC
baada ya kupata kura 1043 akimshinda
mpinzani wake wa karibu Jamhuri Mussa
Kihwelo 'Julio' aliyepata kura 413 na
Swedi Nkwabi kura 300. Hata hivyo, hizo
ni taarifa za awali....
 
Japo nilimpenda wambura lakin niwapongeze wapiga kura. Simba moja ndo tunataka, inayochukua vikombe vya kimataifa. Waliopewa fursa wasikeshe kwa sherehe wafanye kazi
 
japo nilimpenda wambura lakin niwapongeze wapiga kura. Simba moja ndo tunataka, inayochukua vikombe vya kimataifa. Waliopewa fursa wasikeshe kwa sherehe wafanye kazi


unawapongeza nani wakati mtoa uzi hajasema matokeo ?
 
sitegemei chochote kile. ukiona watu mnagombana tu kwenye uchaguzi ujue huko mbeleni hakuna jipya. yu wapi Rage aliyeingia madarakani na mbwembwe nyingi
 
Tatizo majungu yametawala soka la bongo, ila atakaeshinda tumpe ushirikiano
 
Hapo simba tayali kuna simba Wambura na Simba Aveva Mpira pesa na tarebani....
Kupata uongozi wa Aveva bila kukaa na kuondoa makundi na chuki kati yenu hakutakuwa na tija kwa simba na mpira kwa ujumla tafakari na chukueni hatua
 
inamaana hayajatangazwa rasmi tu..
 
julioooooooooooooooooooo.............................
 
Nilikua najiluliza Said Tuli kaingiaje hapa... Au swaumu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…