Honey kwanini hukuniambia mapema kama unakifafa?

Mwanangu visa vyako ni hot,namkumbuka kisa cha demu wako was Mwanza (Cutelove) unadai demu ni mfupi,amekomaa miguu,anaumwa miguu,anataka kurithi mikoba ya uganga na mwisho akataka kukupiga kizinga kuwa umkopeshe fedha!

Hatar sana!
 
Huyu ulimpa kiasi gani cha kujia lodge nahisi uber boda ilihusika, na iyo uliyo ita lodge nawasiwasi labda gesti ya buko chache tu,
 
Mwanangu visa vyako ni hot,namkumbuka kisa cha demu wako was Mwanza (Cutelove) unadai demu ni mfupi,amekomaa miguu,anaumwa miguu,anataka kurithi mikoba ya uganga na mwisho akataka kukupiga kizinga kuwa umkopeshe fedha!

Hatar sana!
mkuu yale yalishapita
 
Huyu ulimpa kiasi gani cha kujia lodge nahisi uber boda ilihusika, na iyo uliyo ita lodge nawasiwasi labda gesti ya buko chache tu,
Huyu nilitaka kuoa kabisa mkuu
 
Huyu nilitaka kuoa kabisa mkuu
Mkuu basi kisicho rizki hakiliki, waswahili usema unapoweka mipango yako yote na imani ndio majanga kama hayo hutokea, kwani huo ugonjwa hauna tiba?? Kama unatibika mtibie apate kuku enzi daima.
 
Kabla sijaandika kitu chochote naomba nieleweke kwamba sio kwamba nalalamika kukutana na binti mwenye kifafa ila ninacholalamika kwanini hakuniambia mapema ili nijue na ili nijipange na yajayo. OK ilikuwa hivi.

JUMATATU YA TAREHE 2- 09- 2019.
Siku hii ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwenda kuwatembelea na kuwakagua wanafunzi wa chuo niliopangiwa waliokuwa kwenye mafunzo (field) ndani ya Ilala na Temeke. Baada ya kufika Temeke niliwakusanya wanafunzi wote ili tufahamiane kwanza maana nilikuwa siwajui japo kuwa wao walikuwa wananijua. Katika utambulisho ndipo nilipokutana na mwanafunzi mmoja mrembo sana wa mwaka wa pili na bahati nziri yeye ndiye aliyekuwa team leader wa lile kundi. Basi nikatoa namba kwa wanafunzi wote ili tuwe tunawasiliana.

JIONI YA TAREHE HIYO HIYO 2-09-2019.
Nilimpigia binti yule tukaongea kidogo kisha tukakubaliana tuonane. Ni kweli tulionana kwenye baa moja inayoitwa TETE BEACH palepale Temeke. Tukaongea kidogo. Mtu mzima nikaona bora nioe tu huyu binti kabisa maana alinivutia sana na nilikuwa nimeshachoka na mikasa ya kimapenzi nikaona bora nitulie sasa na mke kabisa kwani alikuwa anakila sifa ninayoihitaji. Nikamwambia dhamira yangu ya kumuita pale kuwa nina nina hitaji awe mchumba wangu kisha ndoa baadaye. Aliafiki haraka sana mpaka nikaguna mmmmh.

SIKU YA TAREHE 4- 9-2019.
Hii ni siku tuliyokubariana tukutane ili tufahamiane zaidi historia zetu na mambo mengine. Basi tukakubaliana tukutane mida ya saa kumi na mbili jioni ndani ya hotel moja pale pale Temeke. Tuliongea mengi sana ila cha ajabu hakunigusia kama ana matatizo ya kifafa na akipiga mihayo mdomo haurudi mara moja mpaka awepo mtu wa kumrudisha mdomo huo.

KIMBEMBE KINAANZA SAA SABA USIKU.
Kwanza alipiga mihayo, miayo au mwayo Mimi sijui jina sahihi. Baada ya kupiga mihayo hiyo mdomo wa binti ukabaki vilevile na akawa ananioneshea ishara ya kumsaidia kuurudishia. Kiukweli ilikata stim kinoma nikaona mmmh mimeo na ikaniogopesha sana. Na sikua na hamu ya kupiga gemu tena nikawa naomba pakuche tu. Aliniomba msamaha kwa kuto kuniambia mapema na akaomba nimvumilie tu.

KIMBEMBE CHA PILI NI SAA KUMI NA MOJA ASUBUHI.
Tukiwa tukelala nikasikia mtu pembeni yangu anafurukuta. Nilipostuka na kumuangalia nikamkuta anatoka povu mdomoni huku ameuma meno kwa nguvu na anatoka povu nyingi sana mdomono na macho yamemtoka huku mkojo ukimtoka. Mwanzo sikujua kama ni kifafa nikajua mtu ndio anakufa hivyo. Nikapanga nisepe ila nikakausha kidogo.

BAADA YA DAKIKA SABA HIVI KUPITA.
Binti akashusha pumzi kubwa sana na kisha akazinduka, na alikuwa ameumia kichwani kwani alikuwa anajigonga mwisho wa kitanda. Aliponiona akaanza Julia akiniomba nisimuache ila nimsaidie kumtibia tatizo lake maana linamnyima raha na amani. Muda wote huo nilikuwa kimya nikishikuru kimoyomoyo kwa kuzinduka kwake tu na sio kitu kingine chochote.

BAADA YA TUKIO ZIMA.
Nilimwambia tuonde tutakutana siku nyingine ndiyo tutaongea vizuri kuhusu matatizo yako. Tuliagana kila mtu akasepa na njia yake. Jana nilikutana nae kwenye kituo cha kazi kawa mnyonge sana na simu hanipigii tena na Mimi nimekaa kimya nikitafakari.

USHAURI KWA WAPENZI.
Please nawaomba muwe mnawaambia mapenzi wenu matatizo yenu ili wawajue mapema kuliko kuficha na baadaye wakaona wenyewe. Ina umiza sana.
pole baharia
 
Du wee ndugu utavunja zetu hizi stori za kuondoa stres kama una msongo wa mawazo njoo huku jf
 
Back
Top Bottom