Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,178
- 7,319
Naamini JF kuna watu ambao ni wachambuzi wazuri wa siasa. Naomba wanisaidie katika hili...
Tokea jana nimesikia kauli zinazokinzana kati ya Mwenyekiti wa CHADEMA (Freeman Mbowe), na aliyekuwa kiongozi wa upinzani bungeni (Hamad Rashid). Mbowe amekuwa anaelezea ni juhudi gani CHADEMA ilizifanya kutaka kushirikisha CUF katika kambi ya upinzani ya pamoja. Hamad amekuwa akielezea ni masharti gani waliyowapa CHADEMA ili wao CUF waweze kushiriki katika kuunda kambi ya upinzani ya pamoja.
Kauli za pande hizi mbili zimenichanganya kisiasa na kwa namna fulani naona kama kuna mchezo fulani unachezwa hapa.
Kwanza naomba kama kuna mtu amefanikiwa kuwasikiliza kwa kina wadau hawa (kwa bahati mbaya binafsi nimesikia tu sehemu ya maelezo yao), atufafanulie wanataka kuwaambia nini watanzania. Sote tuanafahamu umuhimu wa kambi ya upinzani katika siasa za Tanzania...
Naomba uchambuzi wetu pamoja na mambo mengine ugusie hofu kuwa
- CHADEMA wana uchu wa madaraka
- CUF wana njama ya kuwachongea CHADEMA kwa watanzania
- CUF ni kikaragosi cha CCM
Na mengine mengi ambayo yanaongelewa na watu kuhusu kadhia hii...