Homework kwa wachambuzi wa siasa

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,181
2,000
Naamini JF kuna watu ambao ni wachambuzi wazuri wa siasa. Naomba wanisaidie katika hili...

Tokea jana nimesikia kauli zinazokinzana kati ya Mwenyekiti wa CHADEMA (Freeman Mbowe), na aliyekuwa kiongozi wa upinzani bungeni (Hamad Rashid). Mbowe amekuwa anaelezea ni juhudi gani CHADEMA ilizifanya kutaka kushirikisha CUF katika kambi ya upinzani ya pamoja. Hamad amekuwa akielezea ni masharti gani waliyowapa CHADEMA ili wao CUF waweze kushiriki katika kuunda kambi ya upinzani ya pamoja.

Kauli za pande hizi mbili zimenichanganya kisiasa na kwa namna fulani naona kama kuna mchezo fulani unachezwa hapa.

Kwanza naomba kama kuna mtu amefanikiwa kuwasikiliza kwa kina wadau hawa (kwa bahati mbaya binafsi nimesikia tu sehemu ya maelezo yao), atufafanulie wanataka kuwaambia nini watanzania. Sote tuanafahamu umuhimu wa kambi ya upinzani katika siasa za Tanzania...

Naomba uchambuzi wetu pamoja na mambo mengine ugusie hofu kuwa
- CHADEMA wana uchu wa madaraka
- CUF wana njama ya kuwachongea CHADEMA kwa watanzania
- CUF ni kikaragosi cha CCM


Na mengine mengi ambayo yanaongelewa na watu kuhusu kadhia hii...
 

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,152
1,250
ninachojua kwa sasa ipo haja ya kuutazama muungano wetu upya baada ya mabadiliko ya hivi karibuni ya kativa ya zanazibara kutamaka bayana kuwa zanzibara ni nchi. Sasa hatuwezi katika bunge la nchi moja kuwa na kambi ya uopinzani kutoka nchi jirani, na hoja hiyo inatiliwa nguvu na kitendo cha watanganyika kuipa chadema viti 22 na cufu viti 2 tu.

idadi ya watu wanaowakilishwa na wabunge wote wa baraza la wawakilishi la zanzibar haifikii idadi ya watu ambao mbunge mhe john mnyika wa jimbo la ubungo anawawakilisha. Hivyo cuf hawatakiwi kutusumbua na wabunge 20 kutoka nchi ya zanzibar. Kuhangaika na suala hilo ni sawa na kuhangaika na makando kando ya mwalimu nyerere, badala ya kurithi vitu vyema katika utawala wake.
 

sensa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
397
195
Mie nami nimewasikiliza wote lakini kwa vipengele,ni wazi CUF hawakutaka kushirikiana na chadema tangu mwanzo wakijua tayari wana ndoa na CCM.Mfano hata leo wabunge wa CUF walikuwa wanashangiliwa ccm! ccm! ni dhahiri hakuna upinzani CUF.

Kinachotatanisha ni kwamba NCCR, UDP na TLP wamejiunga na CUF kwa kuelewa ama mkumbo ama wivu na chuki kwa CHADEMA, wanaoelewa zaidi watujuze. Pia kuna swala la future ya CUF nahisi kutokana na hii ndoa ndio kitakufa kabisa kwani kitapoteza sura ya upinzani.
 

MWEEN

JF-Expert Member
Feb 6, 2010
482
250
Kwa muda mfupi ambao hili bunge limekaa, nipepata picha ambayo inazidi kunishawishi kukubali kuwa CUF ni sehemu ya CCM. Nafikiri kule bungeni tuna kambi moja ya upinzani ambayo ni CHADEMA. Haiwezekani kusema kuna upinzani wenye wabunge karibu 25% halafu CCM wanapitisha mambo yao wanavyotaka!

Uchaguzi wa Spika, kumpitisha Waziri Mkuu na uchaguzi wa Naibu spika, wapinzani wamepata kura za possibly wabunge wa CHADEMA pekee. Hata kama ni kumchukia mtu au chama, sielewi lengo la hivi vyama vingine kuungana na CCM katika masuala yote haya. Kinachonikera ni kuwa kuna viashiria kuwa kwa makusudi mazima, wabunge wa vyama vya upinzani wanalazimishwa kufuata maelekezo ya vyama vyao. This is not a healthy opposition!

Nafikia hata kufikiria kuwatenganisha wabunge wa Bara wa CUF from wale wa Zenj kwa kuelewa kuwa kwa Zenj, malengo yao yameshatimia - kupata uongozi, hivyo tusiwaruhusu kutuchafulia upinzani huku bara. Je, upinzani bunge la Muungano uwatenge wabunge wa CUF kutoka Zenj? Inaonekana wanatuchafulia kwa sababu tu wao wameshapata walichokitaka. Wingi wao usiwe hoja kwetu. Tuliweza kutoa changamoto walipokuwa wachache sembse sasa??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom