Homa mitihani kuvuja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Homa mitihani kuvuja

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by BAK, Oct 9, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 9, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,203
  Trophy Points: 280
  Homa mitihani kuvuja

  na Mwandishi Wetu
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  SAKATA la kuvuja kwa mitihani ya kidato cha nne linazidi kuchukua sura mpya tangu Baraza la Taifa la Mitihani lilipotangaza kuahirisha mtihani wa somo la Hisabati.

  Siku chache tu baada ya hatua hiyo ambayo imefuatiwa na shinikizo la kutaka baadhi ya watendaji na viongozi wa serikali kujiuzulu, hali inaonyesha kuzidi kuwa mbaya.

  Katika hatua moja jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, jana alikwepa kuzungumza na wanahabari waliokwenda ofisini kwake kupata kauli yake juu ya kuwapo kwa shinikizo hilo la kumtaka ajiuzulu kutokana na kuvuja huko kwa mitihani.

  Taarifa za awali kwamba Maghembe angezungumza na waandishi wa habari zilibadilika baada ya kutolewa habari kwamba alikuwa ametingwa na shughuli nyingi za kiofisi.

  Badala yake, maofisa wa wizara hizo waliwaeleza waandishi wa habari waliokuwa na shauku ya kumsikia Maghembe kwamba kazi hiyo ingefanywa na mtu mwingine wizarani hapo.

  Uamuzi huo ulisababisha waandishi hao waanze kuzungushwa kutoka ofisi moja kwenda nyingine kusaka mtu sahihi wa kuzungumza.

  Hata hivyo hakuna ofisa yeyote aliyekuwa tayari kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu sakata hilo ambalo limekuwa likichukua sura mpya kila kukicha.

  Mmoja wa maofisa wa wizara hiyo, ambaye hata jina lake hakutaka kulitaja, alisema hawezi kuzungumza na waandishi wa habari kwani tangu amekuwa ndani ya wizara hiyo kwa zaidi ya miaka 20, hajawahi kuzungumza na vyombo vya habari.

  “Mimi nashangaa, tangu nimeanza kazi hapa ni miaka 20, sijawahi kuwaona waandishi wa habari ofisini kwangu, wala kuzungumza nao, leo nimeletewa nitawaambia nini jamani?” alisema na kuongeza kuwa, kuna wasemaji wa masuala hayo na yeye, hausiki.

  Ofisa mwingine wizarani hapo ambaye hakupenda kutaja jina lake, alijitetea kuwa suala la kuvuja mitihani linamhusu Katibu wa Baraza, Dk. Ndalichako na Waziri Maghembe, na akawataka waandishi kuwafuata wao.

  “Hili ni suala la kimaadili zaidi na linamhusu Maghembe yeye mwenyewe. Mfuateni yeye azungumze, alitolee ufafanuzi, sisi wengine hatuwezi kuingilia,” alisema ofisa huyo.

  Wakati waandishi wakiendelea kumsubiri Profesa Maghembe, Ofisa Habari wa wizara hiyo, Ntabi Bunyanzu, alitoa taarifa kwamba wizara ingetoa taarifa baada ya kikao cha Bodi ya Baraza la Mitihani (NECTA) kilichokuwa kikifanyika jana hiyo hiyo.

  Wakati maofisa wizarani wakitupiana mpira, mjini Dodoma jana kulikuwa na taarifa za kuvuja kwa kiwango kikubwa kwa mtihani wa somo la Jiografia unaofanyika leo.

  Taarifa hizo za kuvuja kwa mtihani huo, ambao ulidaiwa kuzagaa mitaani zilisambaa kwa kasi kubwa katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima ambayo pia iliziona baadhi ya nakala za mtihani huo, umebaini kuwa mtihani huo ulikuwa ukiuzwa kwa bei ya kati ya sh 300,000 na sh 200,000.

  Kwa mujibu wa uchunguzi huo, baadhi ya wauzaji wa nakala hizo walielezwa kuwa walifikia hatua ya kutaka kulipwa fedha kwa makubaliano kwamba, malipo yangefanyika baada ya watahiniwa kutoka nje ya vyumba vya mitihani leo hii na kujiridhisha kuwa mitihani iliyovuja ilikuwa ni ya kweli.

  Habari za uhakika zinaonyesha kwamba, kwa kipindi kirefu jana, watahiniwa wengi waliokuwa wamepata nakala hizo za mtihani wa Jiografia walikuwa wamejifungia katika vyumba vya baadhi ya nyumba za kulala wageni, wakiwa na walimu waliowalipa fedha kwa ajili ya kuwafanyia mitihani hiyo leo.

  Baadhi ya wanafunzi waliozungumza na Tanzania Daima, walikielezea kitendo cha watu waliowapa mitihani hiyo kukataa kupokea fedha mapema kuwa ni kielelezo kwamba mitihani iliyovuja ni ya kweli.

  “Tumepata kwa mtu tunayemuamini sana na kwa vile ametuambia tulipe baada ya kuufanya mtihani huo leo, tunashawishika kuamini kuwa mtihani huo ni halisi,” alisema mmoja wa wanafunzi aliyekiri kuona nakala ya mtihani wa Jiografia.

  Vyanzo vyetu vya habari vinasema kuwa mtihani huo umevuja kutoka kwenye moja ya vyuo vikubwa vya mjini hapa.

  Kutokana na hali hiyo, baadhi ya wananchi waliotoa maoni yao, walitaka hatua kali zichukuliwe dhidi ya watendaji wa Baraza la Mitihani nchini (NECTA), kwa kuhusika na uvujaji huo wa mitihani.

  Wananchi hao walisema kuwa serikali inapaswa kuifuta mitihani yote, badala ya mmoja wa Hisabati, kwani kuna uwezekano mkubwa wa mitihani yote kuvuja.

  Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma alipotakiwa kuzungumzia hali hiyo, hakuwapo ofisini kwake, lakini msaidizi wake aliyejitambulisha kwa jina moja la Msoma, alisema ofisi yake imepata taarifa hizo na ilikuwa imeshaanza kuzifuatilia kwa karibu na akaahidi kutoa taarifa zaidi leo.
   
 2. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #2
  Oct 9, 2008
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Huu ni uzembe mwingine katika uongozi.

  kwa nini miaka mingine yote mitihadi ilikuwa inavuja lakini sio kama sasa hivi? ina maana watu tunaowapa jukumu la kusimamia hiyo mitihani ndio wameingiwa zaidi na tamaa hadi wanauza mitihani kama njugu? mfano hai jana nilienda kuwasalimia wazee nyumbani, nikamkuta mdogo wangu (yeye yupo form 5) yupo bize anatuma sms hadi anasahau kunisalimia, namuuliza nbini ananiambia amepewa maswali ya geograph ya form four na mwanafunzi mmoja wa chuo ambaye anayafahamu maswali hayo, hivyo anawatumia rafiki zake wa form 4.

  hali imekuwa rahisi zaidi kwani mtihani mmoja ukivuja kwa mtu mmoja tu hesabu umesambaa kwa watu wote, kwani wanafunzi wanatumia vizuri sana hizi extreme kutumiana maswali na kudiscuss majibu pia, extreme sms nayo inafanya kazi vizuri zaidi kwa ku'foward maswali yaliyovuja kwa wanafunzi wote wa form 4, hii ni mbaya sana

  Na tunaomba Wahusika(wasimamizi wote wa itihani katika vituo vilivyovuja mitihani) wawajibishwe. Waziri naye asijifiche bwana atoke ajiwajibishe mwenyewe.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,203
  Trophy Points: 280
  Date::10/9/2008
  Mitihani: Wasomi wataka Prof Maghembe, Dk Ndalichako wajiuzulu
  Na Omary Magembe, Arusha
  Mwananchi

  SERIKALIi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Arusha jana ilitoa tamko lake kuunga mkono kauli ya Umoja wa Serikali za Wananfunzi wa Vyuo Vikuu (TAHLISO) kumtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe ajiuzulu kutokana na kashfa ya kuvuja kwa mitihani ya kuhitimu kidato cha nne.

  Mbali ya kumtaka Prof Maghembe ajiuzulu, pia chuko hicho kimemtaka Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako aachie ngazi kutokana na kushindwa kusimamia vema idara hiyo hadi mitihani ikavuja.

  Akitoa tamko hilo kwa vyombo vya habari, Waziri mkuu wa serikali hiyo, Silas Noah Bwire alisema, Prof Maghembe ameshindwa kusimamia utendaji na uendeshaji wa mitihani ya sekondari hivyo yeye na Ndalichako waachie ngazi.

  Bwire alisema kitendo cha kuvuja kwa mitihani hiyo ni aina ya ufisadi wa hali ya juu hivyo kwa utendaji bora na wenye kutukuka kwa watendaji hao ni kujiuzulu kama walivyowahi kufanya viongozi wengine waandamizi wa serikali.

  Alisema serikali ifanye uchunguzi wa kina na watakaobainika kuwa nyuma ya kashfa hiyo baada ya kuvuliwa nafasi zao wachukuliwe hatua za kiutumishi na kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mbele ya mahakama.

  "Hii ni sekta muhimu kuliko sekta zote, wizi wa mitihani na vyeti ni kitisho kwa Watanzania, kwa mtindo huu tutajenga taifa la aina gani? La wasomi feki wenye sifa lukuki katika vyeti lakini wabovu katika utendaji? Hili halitavumulika," alisisitiza Bwire.

  Aidha ameonya kuwa suala la mitahini ni la kitaalamu mno na kamwe siasa isiruhusiwe kuingia hata kidogo kwani ubora wa wanafunzi kwa viwango vyote hupimwa kupitia ufaulu katika mitihani yao na si vinginevyo.

  Aliogeza kuwa hata mitihani ya kidato cha nne inayoendelea wakati huu inafaa isitishwe kwani ikiwa Baraza limekiri kuwa somo la hisabati limevuja haiwezi kupinga kuwa hata mingine haikuvuja kwani yote ilikuwa katika stoo moja.

  Wizara ya Elimu na Necta yamekumbwa na kashfa lukuki katika kipindi hiki kama vile migomo ya wanafunzi wa shule na vyuo, vyeti kuibiwa, vyeti bandia kutumika kuingia katika chuo cha ualimu Kange na sasa kuvuja kwa mitihani.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Leo tena NECTA wameendeleza sarakasi zao, wamewaita waandishi wakiwaeleza kuwa Maghembe anataka kuzungumza nao. Walipofika wakakalishwa zaidi ya saa moja unusu na baadaye akaja mtu kutoka kitengo cha fedha kuja kugawa opress release. Nimemona kwenye TBC yule bwana alivyozongwa na waandishi, anatia huruma!
   
 5. N

  Nurujamii JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2008
  Joined: Jun 14, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama kuna mtu ana papers zilizovuja na bado kufanyika ni bora azilete tuzibandike zote hapa JF. Hii itasaidia sio tu kufuta mitihani yote ya mwaka huu bali pia kuwalzimisha hawa jamaa wajiuzulu. Kwa sababu mpaka sasa bado wanajitetea kwamba mtihani uliovuja ni mmoja tu wa maths! Shame on them!
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,203
  Trophy Points: 280
  Wazi lako ni zuri sana. Kuanzia sasa kama kuna tetesi za kuvuja mitihani ya darasa la saba, O'level na A'level juhudi zifanywe ili ipatikane na kuwekwa hapa kabla ya kufanyika kwa mitihani hiyo.
   
 7. O

  Ogah JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Jamani hii aibu hii jamani..........
  ili kuonyesha seriousness
  1. Waziri husika na Katibu Mtendaji Baraza la mitihani la Taifa wawajibishwe
  2. Mitihani yote ifutwe
  3.uandaliwe utaratibu wa haraka kuandaa mitihani mingine na hata ikibidi kutumia chombo independent..........wakati safisha safisha ikiendelea pale Baraza la Mitihani la Taifa
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Mitihani inapatikana hata kwa SMS. Zimevuja nyiingi sio Maths tu!
   
 9. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #9
  Oct 10, 2008
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Mwanawane kama walivyosema waungwana,kama unakutana nayo tuletee hapa JF.Kwani nakumbuka mwaka 1998 ilibandikwa katika nguzo za umeme ndipo Kapuya akaamua kuifuta bila ya kujiuzulu.
   
 10. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #10
  Oct 10, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ogah, Heshima mbele Mkuu,

  Wazo lako kweli ni sahihi sana ila sasa wewe unavyofikiri hata akija Malaika ataweza kutatua hili? Kumbuka bongo kila mtu anajali Tumbo na Isitoshe sisi wazazi bado tunatoa msaada mkubwa kwa watoto wetu kwenye kutafuta hizo Paper. Just imagine wewe ndio mmoja kati ya wahusika wa Baraza na unawatoto wa ndugu zako kama 4 na wakwako 2 utaacha kweli kuchacharika na ukizingatia SHULE ZA SERIKALI ADA NDOGO na watakwenda shule yenye VIPAJA kama unafaulu vizuri.

  Mimi sidhani kama ni suluhu ya hawa waungwana kujiuzulu ila sasa ndio zitafutwe taratibu hasa Mishahara kwa wahusika wote.
   
 11. Masaki

  Masaki JF-Expert Member

  #11
  Oct 10, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,465
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  Nchi hii inatia kichefu chefu. Yaani kila ukiamka unakutana na vichwa vya habari vya magazeti ambayo ni vya kusikitisha tu! Yaani credibility ya wahitimu wa Tanzania katika nyanja za kimataifa inavurugika mchana kweupe na hakuana hatua zozote za makusudi zinazofanyika katika hili! Kuvujisha mitihani ni janga la kitaifa na inahitaji adhabu kali kwa wanaohusika!

  Yaani hata mambo ambayo yalikuwa ndani ya uwezo wetu sasa yanaonekana kama vile hatuwezi kuyadhibiti. Mmomonyoko wa maadili na uzalendo unazidi kuongezeka siku hadi siku. Hii ni kwa sababu wananchi wanakatishwa tamaa na viongozi wasiojali, wanaojilimbikizia mali na kutowajibishana pale wanapokosea!
   
 12. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #12
  Oct 10, 2008
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sisi wa vijijini kila kitu kiovu hasa kikihusisha kununuliwa kwa mtu tunakiita 'richmond'.

  Na hii ni 'richmond' ya kwenye mitihani.

  Poleni sana. Tatizo la letu waTZ ni kuogopa kuchukua hatua. Sasa kama gazeti lilipata mtihani huo kabla haujafanyika, si ingekuwa vyema kama wangeupeleka kwa afisa elimu ili baada ya mtihani halisi kufunguliwa na kuonekana ndiyo huohuo basi NECTA ichukuliwe hatua. Sasa tunasubiri mtihani unafanyika ndipo tunachukua hatua? Its a little late, maana mtu anaweza kusema paper hiyo imetolewa nje baada ya kufanyika, hata kama na hiyo ni makosa lakini siyo sawa na kuvuja.

  WaTZ tunaona maovu mengi lakini hatuchukui hatua - tunapenda mno kunyamaza
   
 13. O

  Ogah JF-Expert Member

  #13
  Oct 10, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  .....kama ni utovu wa maadili......kwa suala hili.....bora nife na njaa.....siwezi kukubali kuchacharika kwa aina hiyo Mkuu wangu..........

  aisee, huwa ninacheka saaana ninapoiona avatar yako.......naona Mizengo kauchapa usingizi ile mbaya
   
 14. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yep, Mizengo yupo na mzee wa Vijisenti. Ten aumenikumbusha ina maana issue ya vijisenti ndio ilishaisha au mbona sisikii tena masuala ya Rada? Au ndio Vumbi lililokutwa ndani ya ukumbi wa Bunge
   
 15. hamix manko

  hamix manko Member

  #15
  Sep 27, 2016
  Joined: Aug 1, 2016
  Messages: 96
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  A
   
Loading...