Homa gani hii wakuu?

Bin Shaib

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
1,315
1,186
Wakuu habari za uzima ,natumai hamjambo, mi mwenzenu si mzima wa afya sababu naumwa.

Kama siku tano zimepita kabla ya hili kutokea, hizo siku tano nyuma nilifanya kazi ngumu ambayo ilipelekea joint zote na viungo kama kiuno, mikono na sehemu nyingine kwenye mwili wangu,

Kazi yenyewe ilikuwa kukata kata mti kwa mashine ya (chainsaw) kwakuwa mi si mzoefu nipo katka mafunzo hivo ilipelekea kuchoka viungo vyote.

Nimekaa na yale maumivu lakini nashangaa kupitia maimivu yale mpaka nimepitiwa na ugonjwa ambao sijajua je, ni sababu ya ile mikikimikiki ya mashine na ule muungurumo Ndo vimenisababishia,

Hapa nilipo nina maaumivu ya mwili yaan mwili hauna nguvu kabisa kichwa kinagonga sana pia koo linauma hadi kumeza mate inakuwa shida.

Usiku wa kuamkia leo March 7 sijapata kabisa usingizi mwili wote ulikuwa wa moto sana, hadi nikipumua hewa kutoka mdomoni niya moto vile vile.

Naandika hili hapa lakini najisikia vibaya sana, nimetumia action lakini bado sijapata ahueni ndo leo nataka nitumie kitunguu swaumu.

Nimepanga kwenda kupima, halafu kumbe ubishi ambao unakuta unabishana kwa sauti nayo inasababisha maumivu ya kichwa maana kabla ya kichwa kuuma tulibishana sana kijiweni, halafu jioni mambo yaka change.

Tafadhali mwenye ujuzi nahili anisaidie, nawasilisha jf.

Bin Shaib Classic 2020

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom