Holy Week. Matukio ya Jumatano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Holy Week. Matukio ya Jumatano

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andrew Nyerere, Mar 31, 2010.

 1. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #1
  Mar 31, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Siku ya Jumatano,kwa kawaida ilikuwa siku ya mapumziko. Kama kulikuwa hakuna kazi muhimu ya kufanya,Yesu aliwaagiza wafuasi wake kupumzika. Kwa hiyo Jumatano hii Yesu akasema kwamba atakwenda peke yake kusali.
  David Zebedee akapendekeza Yesu aende na walinzi watatu kumlinda,kwa ajili hali ya usalama ilikuwa siyo nzuri. Yesu alikataa,akasema,hawezi kupata madhara kama saa yake haijafika. David Zebedee alikuwa messenger na aliongoza kundi la messengers kuiunganisha oganaizesheni yote ya Yesu
  Halafu John Mark,akajitolea kufuatana na Yesu,kubeba kikapu cha chakula. Baada ya John Mark kung'ang'ania,Yesu akakubali.
  John Mark wakaondoka pamoja na Yesu. John Mark akamweleza Yesu kwamba anasikitika kwamba umri wake mdogo haumruhusu kuwa Mtume. Yesu akamwambia kwamba siku zijazo atakuwa mfuasi mzuri wa Dini hii,kwa sababu wazazi wake walimlea vizuri,kwa upendo,alkini bila kumdekeza.
  Yesu akasema,'' Yule rafiki yako Amos naye pia alitaka kuwa mfuasi wangu lakini wazazi wake wakamkataza,naye akaamua atawatii wazazi wake,na amebaki nyumbani. Atapata hasara,lakini ameamua vema,kwa sababu ni vizuri kuwatii wazazi. Lakini wazazi lazima mwenendo wao uwe mzuri ili watoto wao waweze kuwatii bila kukiuka maadili mema.
  Watoo wanalelewa nyumbani ndivyo wanavyokua,na uhusiano wa mtoto na baba yake ndio unaamua mtoto atamfikiria vipi Mwenyezi Mungu. Baba akiwa makali,mtoto atakua anafikiria Mungu ni Mkali. Baba akiwa na Upendo,mtoto ataamini Mungu ni Mungu wa Upendo.
  Mungu yupo,na Mungu ni Upendo,na baba,au kiongozi yoyote anayekuwa mkali,au mkatili hamwakilishi vema Mwenyezi Mungu.
  Caiaphas alishangaa kuona kwamba Yesu hakufika Jerusalem kuhuburi. Siyo kama vile Caiaphas alikuwa anayapenda mafundisho ya Yesu,ila tu alikuwa amependezwa na yale maneno aliyosema Yesu kwamba,'fanyeni wanayosema,lakini msifanye wanayotenda,msifanye mambo yao ya kifisadi,lakini muwe watiifu kuhusu mambo yote yanayohusu kudumisha amani katika Taifa.'' Kwa hiyo Caiaphas aliendelea na matayarisho ya Passover.
  Halafu Judas,ambaye alikuwa ameamua kumsaliti Yesu alikwenda kumtafuta Caiaphas. Alikwenda kwa Caiaphas kwa kupitia binamu yake ambaye alikuwa mmoja wa makuhani katika Sanhedrin. Naye akampeleka kwa Caiaphas. Akasema,''Huyu binamu yangu alikuwa mfuais wa Yesu,lakini sasa ameamua kwamba Yesu ni mlaghai,kwa hiyo amefikia uamuzi kwamba itakuwa vizuri ili kudumisha amani ya Taifa,kwamba Yesu akamatwe;na ili kuthibitisha kwamba amehuzunishwa sana kwamba alishiriki katika yele mafundisho ya upotofu,anataka kujitolea kushirikiana na Mkuu wa Walinzi kwenda kukamata Yesu;amablo anaona ni jambo ambalo litaonyesha hamu yake kubwa ya kupatanishwa tena na Jamii ya Wayahudi na kuonyesha kwamba ametubu kuhusu ulaghai wote uliotokea.''
  Judas akasema,''Yote aliyosema binamu yangu nitafanya. Nataka kujua nitapata zawadi gani.''
  Caiaphas akasema,''Mlete Yesu,leo usiku au kesho usiku,na utapata zawadi.''
  Yesu akarudi saa kumi jioni. David Zebedee alikuwa ameshatuma habari kwa Mama yake Yesu na Familia yote ya Yesu wafike Jerusalem,kwa vile kulikuwa kuna mambo yanatokea,na walileta habari kwamba watafika kesho jioni au mapema kesho kutwa asubuhi.
  Tutaendelea kesho,Alhamisi,kujadili mambo yaliyotokes Holy Thursday.

   
 2. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Amen!
   
 3. JS

  JS JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Thanks Ganesh
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Be blessed
   
Loading...