VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Shirika la Utangazaji la Tanzania almaarufu kama TBC linapaswa kubinafsishwa. TBC inayomiliki Vituo vya runinga cha TBC1 na TBC2 (?) na vituo vya redio vya TBC Taifa, TBC FM na TBC International kwasasa linaonesha kutokuwa na tija.
TBC haliaminiki hata na viongozi wakuu wa Serikali, akiwemo Rais Magufuli ambaye mara kadhaa amekuwa akimwaga sifa kwa Clouds Media.Hata kauli za kiserikali hutolewa na taasisi binafsi. TBC hawana vipindi vyenye mashiko na kuvutia watazamaji na wasikilizaji wake.
TBC imeshindwa kuendana na ushindani katika tasnia ya habari na mawasiliano hapa Tanzania na hata nje ya mipaka yetu. TBC imekuwa nyuma kwa kila idara iliyotazamiwa kuimarika kama Shirika la Utangazaji. Natoa hoja kuwa TBC ibinafsishwe kwakuwa haina tija kwa Taifa.
Nawasilisha.
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam