getrusa
JF-Expert Member
- Aug 16, 2013
- 2,150
- 1,812
Kwa wote wanao husika,
Wakuu amani iwe kwenu, kwa siku za karibuni kumekuwa na mijadala isiyo rasmi inayohusiana na wimbo wetu wa Taifa, ambapo pamoja na mambo mengine wimbo huu unatengeneza hoja mbali mbali ambazo nyingine zinaumiza hisia za Watanzania wanahisi kudhihakiwa kwa Utanzania na tunu yao ya Taifa.
Na Wengine unaumiza maisha yao na familia zao kama Watanzania wenzetu bila kujali itikadi zao za kisiasa. Mfano Nusrat na wenzie tukumbuke hawa ni ndugu zetu pia.
Msingi wa hoja yangu ni Uhalali wa kuufanya wimbo huu wa Taifa kwa maana ya hati miliki ya wimbo huu kwa Taifa letu, kwa sabbu kwa umaarufu wake umeshahaririwa na Mataifa mbalimbali.
Mtunzi wa wimbo huu sio Mtanzania, hivyo huenda hata hati miliki au umiliki wa Utunzi wa Wimbo huu sio wa Tanzania, (sio Wetu)..
wimbo huu unatumika Zambia, Afrika ya Kusini huenda Nchi nyingine pia, hivyo sidhani kama haki ya kubadirisha maneno ya wimbo huo inazuiwaa kisheria..
Angalizo:
Huenda kikaibuka kizazi kitakachodai haki miliki ya wimbo huu, kutoka katika Uzao wa marehemu Mtunzi na kupeleka jambo hili katika vyombo vinavyosimamia hati miliki na sisi kama Taifa tukajikuta tunapaswa kulipa gharama ambazo hazikuwa na ulazima.
Ushauri:
Kuna nyimbo zinazochochea Uzalendo na hari ya kuwa Mtanzania zikiimbwa hata ukiwa mbali ya Nje ya Tanzania unaungwanishwa kihisia na Nchi yako.
Nyimbo hizi zimetungwa na Watanzania wenyewe.
Mfano: " TANZANIA TANZANIA NAKUPENDA KWA MOYO WOTE "
AU "TAZAMA RAMANI UTAONA NCHI NZURI..."
Nyimbo hizi zimebeba ujumbe wa ndani sana wa Uzalendo wa Taifa letu..
Enyi wabunge watarajiwa na Watanzania kwa Ujumla nawasilisha kwa heshima jambo hili mbele yenu ili tusiendelee kuumizana bila sabbu za msingi..
Ahsanteni.