Hoja ya haja tena! Kutoka Michuzi blog | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja ya haja tena! Kutoka Michuzi blog

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumaku, Dec 21, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Dec 21, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ( Mjadala huu nimeunasa kule Michuzi blog)

  Hali ya siasa ‘yatulia’ miaka minne ya JK


  Na Mgaya Kingoba

  "NCHI hii haijawahi kuongozwa na malaika wala haitapata kuongozwa na rais malaika…Rais Kikwete si malaika, lakini ni kiongozi mzuri, msikivu, mvumilivu na mchapa kazi. Sasa linapojitokeza kundi la wachache na kufanya kampeni ya makusudi ya kumpaka matope, lina jambo.”

  Hiyo ni nukuu ya mwanasiasa mkongwe nchini, Pius Ngeze ambaye kwa miaka mingi alishikilia wadhifa wa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Kagera. Kauli hiyo aliitoa wiki iliyopita wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maoni ya baadhi ya waliokuwa viongozi wa chama na serikali wakati wa kongamano la miaka 10 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere lililojadili mustakabali wa nchi.

  Nimeitumia nukuu hiyo kama rejeo langu katika makala haya yatakayojikita kuangalia hali ya kisiasa nchini katika miaka minne ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete aliyeingia madarakani Desemba 21, 2005.

  Kwa maneno hayo ya Mzee Ngeze, hakuna shaka kuwa Tanzania haijapata kuongozwa na malaika na wala hatatokea malaika kuiongoza nchi hii, lakini ni ukweli usiopingika kuwa Rais Kikwete amekuwa msikivu, mvumilivu na mchapakazi aliyetoa uhuru wa watu wengi kutoa mawazo yao.

  Ni kwa msingi huo, ndio maana yanayojitokeza katika siasa za Tanzania, iwe kwenye chama chake cha CCM, vyama vya upinzani au kwa wananchi kwa ujumla, ni kwa sababu ya uongozi wake mzuri.


  Kwa ujumla, kwa miaka minne ya utawala wa Rais Kikwete, hali ya kisiasa nchini ni nzuri, kwa sababu hata ukilinganisha na nchi nyingine za jirani, tumeshuhudia masuala mengi ya kisiasa nchini yakijadiliwa kwa mapana, tena wakati mwingine kwa jazba, lakini Watanzania wameendelea kuwa wamoja.

  Vyama vya siasa vimepewa uhuru mkubwa wa kuendesha siasa zao kuanzia CCM hadi kwa wapinzani ambao wamekuwa wakiikosoa serikali na chama hicho tawala kwa uhuru bila kuwepo kwa vipingamizi.

  Vimekuwa huru kuendesha mambo yao kwa mujibu wa taratibu za vyama vyao na kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Ndio maana leo kumekuwepo na Operesheni Sangara, ikaja Operesheni Zinduka na haitashangaza kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwakani, tutashuhudia operesheni nyingine.


  Lakini zote hizo, zimefanyika bila ya vyama husika, Chadema na CUF kuwekewa mizengwe na haishangazi kuona helikopta inaruka bila kipingamizi! Hayo ni mojawapo ya matunda ya Kikwete katika kuhakikisha siasa nchini inakwenda kama ilivyoelekezwa na Katiba ya Tanzania na wananchi wake wako huru kushiriki katika sehemu hiyo muhimu ya demokrasia.

  Na hata katika uchaguzi mbalimbali wa vyama vya siasa kuanzia CCM hadi vile vya upinzani, hali imekuwa nzuri kwa maana uendeshaji wa uchaguzi huo umekuwa wa amani na utulivu. Tumeshuhudia mvutano katika kuwania nafasi mbalimbali, na hata wakati mwingine baadhi ya wagombea kutishia kwenda mahakamani kusimamisha uchaguzi, lakini mwishowe, uchaguzi unapita kwa amani.

  Hayo yameshuhudiwa kama nilivyoeleza katika vyama vya CCM, CUF, Chadema, TLP na vingine. Vyama hivyo vimetumia demokrasia kuwapata viongozi wao wanaowapenda, na mwishoni wale walikuwa na malalamiko, kila mmoja alikubali matokeo, kuonesha ukomavu wa demokrasia na siasa nchini chini ya uongozi wa Rais Kikwete.


  Aidha, pia kumekuwepo na matukio machache ya vurugu katika baadhi ya uchaguzi hasa ule mdogo wa majimbo. Lakini kuanzia katika ngazi ya vyama hadi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Oktoba mwaka huu, Watanzania na wapenzi wa siasa, wamepewa fursa ya kushiriki katika mchakato huo kwa amani.


  Ndani ya miaka minne ya utawala wa Rais Kikwete, kumekuwepo msuguano wa hapa na pale katika chama chake, CCM, kiasi cha siku za karibuni, kudaiwa kuwepo makundi kadhaa ndani ya chama hicho kikongwe. Kila linaloigusa CCM, linaigusa jamii ya Watanzania kwa sababu chama hicho ndicho kinachoongoza Dola, kwa hiyo uimara wake ni uimara wa Tanzania, na endapo kitayumba, basi nchi nayo itayumba, kama alivyowahi kueleza Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere enzi za uhai wake.


  Hivyo, lolote linalotendeka ndani ya CCM, lazima Watanzania watapenda kulifahamu na ndio maana kumekuwepo na mjadala mzito kuhusu chama hicho kutokana na madai hayo ya msuguano na makundi. Kwa mfano, mwaka huu, imeilazimu CCM kuunda Kamati ya Wazee yenye kuongozwa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, kutafuta kiini cha madai ya kuwepo makundi miongoni mwa wabunge wake, hali ambayo inadaiwa kudhoofisha utendaji wao ndani ya chombo cha kutunga sheria.

  Hiyo imetokana na mijadala mizito inayojitokeza katika Bunge na pia ndani ya vikao vya CCM kama vile Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ambako inaelezwa katika kikao kimojawapo, wajumbe walipewa fursa ya kila mmoja kutoa dukuduku lake mbele ya Mwenyekiti Rais Kikwete.

  Tayari pia wabunge hao wa CCM wamepata nafasi ya kutoa dukuduku zao mbele ya Kamati ya Mzee Mwinyi na sasa kinachosubiriwa na ripoti yao kwa waliowatuma kazi hiyo, NEC.

  Lakini lililo wazi ni kwamba wapo watu, tena wengi, wanaoitazama mijadala na misuguano hiyo ndani ya CCM kama yenye busara na yenye kujenga ustawi wa chama chenyewe na Tanzania kwa ujumla. Wanaona ni suala zuri kwani mwishoni unapatikana mwafaka wa wengi ili kunusuru chama na nchi. Hao ni wale wanaoiona hali hiyo kama yenye siha kwa manufaa ya CCM na Taifa kwa ujumla, lakini wapo pia wanaoitazama hali hiyo tofauti.

  Na hawa ni wale wanaomshutumu Rais Kikwete kwamba alipaswa kushika ‘rungu’ na kukemea au kumaliza matatizo hayo kwa nafasi yake aliyonayo katika chama, ya uenyekiti. Wanamwona Rais Kikwete hana msimamo, walitaka aje na uamuzi wa mwisho kuhusu misuguano hiyo ndani ya chama chake. Lakini hawa wanasahau kitu kimoja. Hiyo siyo staili ya uongozi ya Kikwete. Hawa ni wale wasioheshimu misingi ya demokrasia. Wasioruhusu kuwepo kwa mijadala hata kama wao wenyewe hawaipendi. Ndio maana mwanzoni mwa makala haya nilimnukuu Mzee Ngeze akisema kuwa Rais Kikwete ni kiongozi mzuri, msikivu, mvumilivu na mchapakazi.

  Ni kweli, ndio maana amewaachia watu wajadiliane wanavyotaka, lakini mwishoni mwa siku wanaibuka na msimamo mmoja. Ndio msingi wa demokrasia. Na hili unaweza kuliunganisha moja kwa moja na hali ya kisiasa katika Zanzibar tangu Rais Kikwete aingie madarakani. Alieleza wazi katika hotuba yake ya kwanza bungeni Desemba 2005, kwamba atajitahidi kuhakikisha anamaliza mpasuko wa kisiasa visiwani humo; na amejitahidi kufanya hivyo.

  Amesimamia kupitia chama na serikali yake, majadiliano ya kusaka mwafaka wa Chama cha Wananchi (CUF). Na amehakikishia mazungumzo ya kusaka suluhu kati ya vyama vya CCM na CUF yanakwenda sawa, ingawa yamekuwa wakati mwingine yakipata vikwazo, jambo ambalo katika siasa, haliepukiki.

  Hatua ya hivi karibuni ya Rais Amani Abeid Karume kukutana na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ni ishara mojawapo ya juhudi hizo za kusaka amani ya kudumu katika visiwa hivyo.

  Ingawa hatua hiyo ya Rais Karume kuzungumza na Maalim Seif na kufikia maridhiano kwa nia ya kuijenga Zanzibar, inaweza kuonekana haina mkono wa moja kwa moja wa Rais Kikwete, lakini ukweli mkono wake upo. Kwa sababu Rais Kikwete wakati mwingine hapendi kufanya kile kinachoitwa ‘direct intervention’, lakini atakuwa ameingilia kwa upande mwingine na hasa ukizingatia mfumo wa chama chake cha CCM na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; hivyo huwezi kumtupa nje ya maridhiano ya sasa ya Zanzibar.

  Rais Kikwete ana tabia ya kutotaka “apande mlimani na kupiga baragamu” kila mtu amwone. Hakuna shaka katika hili amefanikiwa angalau sasa kuweka msingi mzuri wa ahadi yake ya kumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar kama alivyoahidi bungeni katika hotuba yake ya kwanza. Hapa pia anastahili pongezi kwa kuweka mazingira mazuri ya siasa katika nchi, kuendeshwa kwa majadiliano na maridhiano.

  Kwa hiyo, kwa miaka minne ya uongozi wake, kwa ujumla unaweza kueleza bila ya kusita kuwa hali ya kisiasa nchini imedhibitiwa, hakuna vurugu na watu wanaendesha shughuli za kisiasa kwa amani. Imani ni kubwa kwamba tunapoanza ngwe ya mwisho ya kipindi chake cha kwanza cha Rais Kikwete na kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwakani, hali ya kisiasa nchini inaonesha matumaini makubwa na uhuru katika kutekeleza moja ya majukumu ya demokrasia nchini.

  Rais Kikwete anastahili pongezi kwa kufanikisha haya.

   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Hehehehe
  Macho yanaona na mdomo unasema ila ukweli unaonekana dhahiri kwamba Muungwana ametupiga changa la macho katika kipindi chake cha uongozi. Kuna waliotabiri hivyo na ikawa kweli
   
 3. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  ndio maana jk kasema asilimia 70 ya wanachi wanafuata upepo tu kutoka na mijitu kama hii.yeye mwenyewe anajijua kwamba sio kiongozi mzuri na anashangaa kuona support kubwa ya wananchi inamuunga mkono na hio asilimia 70 anayozungumzia ni hile iliompigia kura bila kujali historia yake ya uongozi wao wamefuata tu upepo kwa kuwa ana maswahiba wengi.
   
 4. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,554
  Likes Received: 1,902
  Trophy Points: 280
  Tafuteni namna nyingine ya kumpigia debe Muungwana,maana hapa mnachekesha,Muungwana hakuwaahidi wananchi kwamba atawaletea amani,amani tayari ipo na ilikuwepo,kampeni ya mwanzo 2005,ilikuwa ni kuwaletea wananchi maisha bora....Na kwahiyo mnataka achaguliwe kwa mara nyingine kwasababu ni msikivu,je anamsikiliza nani?

  Kuwa msikivu na unayemsikiliza ni mambo mawili tofauti....Kwasababu maamuzi ndiyo what matters at the end of the day...Ni sawa kuhusu hayo mambo ya kina Seif Sheriff,lakini maisha bora vipi?mbona hakuna pahala imegusiwa hilo kuhusu maisha ya wananchi na uchumi kwa ujumla?

  Wananchi wamekuwa wakilalamika kuhusu safari zake za mara kwa mara ambazo zinzligharimu taifa mamilioni ya dollars,sasa mmeshawaeleza manufaa ya safari hizo?Ama sasa mnatumia defensive mechanism na kudai wananchi wana wivu?
   
 5. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #5
  Dec 21, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  WTF, Hii ingeachwa ibaki huko huko michuzi blog - it was meant kwa wasomaji wa hiyo blog na ndiko inakofaa, siyo hapa JF.
   
 6. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pamoja na mapungufu ya ki campeign iliyonayo bado si vibaya kupima ubora au ubaya wa tabia za wanao kwa kutumia tabia za watoto wa jirani kama kielelezo cha tabia unachopenda wanao wawe nayo.
   
 7. Serendipity

  Serendipity JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2009
  Joined: Jan 24, 2009
  Messages: 475
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tatizo la JK hayupo serious na mambo muhimu yanayohusu nchi!
  Yeye anatilia mkazo mambo ambayo sio muhimu na kuzarau serious issues.
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Dec 22, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  ..1995 nasikia Pius Ngeze alimtetea Lowassa kwenye kikao cha NEC-CCM cha mchakato wa Uraisi.

  ..nasikia kitendo hicho cha Pius Ngeze ndicho kilichomtibua Mwalimu kumwambia[Ngeze] kama anampenda sana Lowassa basi waende wakanywe naye chai.

  ..wenye data zaidi naomba mnisaidie kama hicho nilichosimuliwa kuhusu Ngeze ni kweli au la.
   
 9. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Anajitahidi kumpigia debe, hastahili kulaumiwa ndipo ukomo wa ufahamu wake, I think atawachota wana-Michuzi bt not wana-JF:-:The home Of Great Thinkers
   
Loading...