HOJA NZITO: Sheria ni kwa nani?

HOJA NZITO: Sheria ni kwa nani?

franci45

Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
61
Reaction score
93
Tunaona magari ya serikali yanayoonekana wazi kabisa kuwa mapya Prado za 2024/2025 lakini yanatembea na namba za usajili za zamani za miaka ya 2000, mfano T 220 ATZ.

Hii ni akili ya kawaida au ni dharau kwa jamii?

Je, serikali haijui kuwa mfuatano wa namba unaendana na mwaka wa usajili? Au wanajua lakini hawajali?
Kama hii inaitwa “intelijensia”, basi ni intelijensia dhaifu sana.

Katika dunia ya leo, kweli usalama unategemea kubandika namba ya zamani kwenye gari jipya? Hii si ujinga wa wazi?

Na kama kuna utaratibu maalum unaoruhusu hili, kwa nini hauwekwa wazi?

Kwa nini wananchi wa kawaida wakikiuka sheria wanakamatwa papo hapo, lakini magari ya serikali yanakiuka waziwazi bila hata aibu?

Swali la msingi: Je, sheria zipo kulinda haki au zipo kuwakandamiza raia wa kawaida tu?

Kama viongozi na taasisi za serikali ndizo za kwanza kukiuka sheria, basi tunatarajia nini kutoka kwa wananchi?
 
Sheria zinahusu walala hoi, si unaona mtu kaua watu umejiuliza ni sheria gani zinamtaka aunde tume na sio kwenda jela?
 
Gari ya spika wa bunge hailali nyumbani kwa spika wa bunge je dereva wakati anaenda kumchukua spika wa bunge aweke plate no za spika au anapokuwa hayupo na spika ni sahihi kuweka plate no za spika?

Fatilia kwanza taratibu za protocol then ndo uje uongee
 
Gari ya spika wa bunge hailali nyumbani kwa spika wa bunge je dereva wakati anaenda kumchukua spika wa bunge aweke plate no za spika au anapokuwa hayupo na spika ni sahihi kuweka plate no za spika?

Fatilia kwanza taratibu za protocol then ndo uje uongee
Lakini bado haujajibu swali la msingi.
Hoja haikuwa gari la spika linalala wapi, wala dereva anamchukua nani.

Hoja ni matumizi ya namba za usajili zisizoendana na mwaka wa gari.
Protocol haisimamii usajili wa magari.
Usajili unasimamiwa na sheria za nchi, si hisia wala mazingira ya kazi ya dereva.

Kama gari lina plate number ya mtu fulani au ofisi fulani, basi hilo gari liwe limesajiliwa kihalali kwa plate hiyo bila kujali spika yupo au hayupo ndani ya gari.

Huwezi kubadilisha mantiki ya usajili kwa sababu “dereva anaenda kumchukua mtu”.
Na kama kuna utaratibu maalum wa kiserikali unaoruhusu magari mapya kubeba namba za zamani, basi uelezwe wazi.

Kusema tu “fuata protocol” bila kuonyesha kifungu cha sheria au utaratibu rasmi si jibu, ni kukwepa hoja.
Kwa hiyo swali bado lipo pale pale. Je, haya ni matumizi halali yanayoruhusiwa kisheria, au ni upendeleo unaovumiliwa kimya kimya?

Kama una taarifa sahihi za kisheria au waraka unaoeleza hilo, uweke wazi.
Hoja haimalizwi kwa kauli, inamalizwa kwa ushahidi.
 
Back
Top Bottom