Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HOJA na VIOJA vya VC-UDSM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by VUTA-NKUVUTE, Oct 12, 2012.

  1. VUTA-NKUVUTE

    VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

    #1
    Oct 12, 2012
    Joined: Nov 25, 2010
    Messages: 5,571
    Likes Received: 3,357
    Trophy Points: 280
    Jana ulifanyika Mkutano baina ya Makamu Mkuu wa Chuo-UDSM almaarufu kama VC,Prof.Rwekaza Sympho Mukandara na wafanyakazi wote wa chuo hicho. Washiriki,ambao ni wafanyakazi,walitoa hoja mbalimbali ambazo zilikumbana na majibu ya vioja vya Makamu Mkuu huyo wa chuo.

    1.Hoja: Nyumba ya Makamu Mkuu wa Chuo ambayo haikaliwi na mtu yeyote lakini inalindwa na kukarabatiwa kwa gharama kubwa iwekwe mikononi mwa Mhadhiri au Mfanyakazi mwingine ili aweze kuitumia.Hii ni kwasababu Prof. Mukandara anaishi kwenye Hekalu lake kule Makongo Juu.

    Jibu-Kihoja LA VC: Nyumba ile kwasasa inatumika kama ukumbi wa 'Functions' mbalimbali.

    2. Hoja: Nafasi za kiutawala kuanzia na Makamu Mkuu wa Chuo na Manaibu wake sasa zishikwe na watu wenye weledi wa uongozi na uzoefu uliotukuka badala ya Maprofesa ambao wameshindwa kuonesha ufanisi wao.

    Jibu-Kihoja la VC: Acha kazi hapa UDSM ukaipate kwenye Chuo na namna uitakayo.

    3. Hoja: Responsibility allowance(imenishinda kuitafsiri kwa Kiswahili) ziwe zinatolewa kwa wafanyakazi wa kada ya chini badala ya wa juu kwakuwa wachini ndio wanaolundikiwa kazi na Wakuu wao.

    Jibu-Kihoja la VC: Hiyo haiwezekani

    4. Hoja: Kwanini mishahara ilipandishwa kiholela na Chuo ikiwa Hazina hawana taarifa na sasa inashushwa?

    Jibu-Kihoja la VC: Kaiulizeni Serikali....sisi tulifanya hivyo kwa nia njema kabisa.

    Wana-JF pimeni na mjionee wenyewe...
     
  2. Facilitator

    Facilitator JF-Expert Member

    #2
    Oct 12, 2012
    Joined: Oct 30, 2010
    Messages: 2,093
    Likes Received: 173
    Trophy Points: 160
    Hiyo hoja ya kwanza, kwani bodi (senate) ya chuo inalionaje hilo?? Ni kwa vipi uamuzi wa kubadili matumizi ya nyumba ya VC kuwa ukumbi ulifikiwa??
     
  3. Lukolo

    Lukolo JF-Expert Member

    #3
    Oct 12, 2012
    Joined: Dec 2, 2009
    Messages: 5,125
    Likes Received: 34
    Trophy Points: 145
    Hayo ndo majibu mnayoyastahili na unafiki wenu. Huwa nashangaa sana ninapoona maprofessor wazima wanalalamika ooh, sijui mishahara inachelewa, mara oooh PPF mara ooh mishahara hailipwi kwa haki. Yaani na nyie mnakuwa watu wakulalamika? Sisi walimu wa secondary au primary huku tufanyeje kumbe? Maana tulijua nyie wasomi ndiye mnayejua haki zenu za msingi na namna ya kuzitetea.

    Nasikia sehemu nyingine ofisi yenye meza tatu na viti sita inatumiwa na wafanyakazi 20. Really? Wafanyakazi wa university hao? Na wanafundisha na kufanya research? Sitarajii kitu chochote kizuri kutoka kwenye institution ya aina hii. Hata sisi walimu wa secondary huku tuna unafuu angalau kila mwalimu ana meza yake. Nawashangaeni sana nyie wasomi wa siku hizi. Tangu afe Chachage basi hakuna kipya kinachoendelea UDSM. Yaani sasa hivi shida ninazokutana nazo mimi huku uswekeni ni sawa tu na za kwenu. Muache kuja kulalamika hapa, chukueni hatua. Nyie ndo chachu ya mabadiliko ya nchi hii. Kama nyie hamuwezi kusimamia haki zenu za msingi mnategemea sie ambaye hatukwenda shule tutafanyaje?
     
  4. Victoire

    Victoire JF-Expert Member

    #4
    Oct 12, 2012
    Joined: Jul 4, 2008
    Messages: 8,656
    Likes Received: 2,754
    Trophy Points: 280
    mmekubali kudharauliwa,HAYO NDO MAJIBU MNAYOSTAHILI.Kutwa maneno vitendo hakuna,Hongera sana VC.
     
  5. B

    Bulesi JF-Expert Member

    #5
    Oct 12, 2012
    Joined: May 14, 2008
    Messages: 6,420
    Likes Received: 356
    Trophy Points: 180
    Ningependa kujua kama huyu VC wenu aliyeamua kukaa nyumbani kwake badala ya nyumba ya chuo kama analipwa allowance yeyote inayohusiana na kukaa kwake nyumbani kwake? Kwavile chuo kimempatia nyumba ya kuishi na yeye kaamua kuishi kwenye nyumba yake, hastahili kulipwa hata senti moja na kama analipwa huo ni wizi anakiibia chuo!!
     
  6. POMPO

    POMPO JF-Expert Member

    #6
    Oct 12, 2012
    Joined: Mar 12, 2011
    Messages: 6,694
    Likes Received: 8
    Trophy Points: 135
    Alimuuwa Prof Chachage ili atawale, nadhani damu yake ionamtafuna. kuuwa ili utawale si mchezo.
     
  7. M

    Mundu JF-Expert Member

    #7
    Oct 12, 2012
    Joined: Sep 26, 2008
    Messages: 2,718
    Likes Received: 21
    Trophy Points: 135
    Hivi walimvumilia tu na majibu haya mbofu mbofu...hakyanani...yaani hawakumpopoa mawe? Au hawakumwachia hicho kikao...?

    Jeuri ya madaraka ni mbaya sana. Kiongozi anapaswa kuwa mtumishi...
     
  8. F

    Fitinamwiko JF-Expert Member

    #8
    Oct 12, 2012
    Joined: Aug 13, 2012
    Messages: 4,605
    Likes Received: 16
    Trophy Points: 135
    Majibu hayo yanafanana na ya JK
     
  9. mayenga

    mayenga JF-Expert Member

    #9
    Oct 12, 2012
    Joined: Sep 6, 2009
    Messages: 3,434
    Likes Received: 225
    Trophy Points: 160
    Jamani chuo changu,umefikia hatua hii?
     
  10. King Kong III

    King Kong III JF-Expert Member

    #10
    Oct 12, 2012
    Joined: Oct 15, 2010
    Messages: 24,418
    Likes Received: 1,131
    Trophy Points: 280
    Prof Mkandara ni jeuri sana yule mzee bora Prof Luhanga arudishwe VC ana busara sana Prof. Mathew,,,Mkandara jumba lake la makongo ni zaidi ya ikulu sijui hela alitoa wapi kulijenga!!!
     
  11. only83

    only83 JF-Expert Member

    #11
    Oct 12, 2012
    Joined: Oct 15, 2010
    Messages: 5,020
    Likes Received: 59
    Trophy Points: 145
    Kama kweli huyo Mkandara sijui, katoa majibu mepesi na ya kejeli namna hiyo naona hawana tofauti na Prof. Mlacha DVC-PFA wa pale UDOM..na hawa nadhani kiburi chao kinajengwa na ****** mwenyewe, wateule wa ****** wengi ni dhaifu katika uongozi kama yeye mwenyewe. Yani inakera sana.
     
  12. N

    Ndinani JF-Expert Member

    #12
    Oct 12, 2012
    Joined: Aug 29, 2010
    Messages: 5,105
    Likes Received: 518
    Trophy Points: 280
    Huyu ni rafiki yake wa karibu na ndio maana anajibu kwa jeuri kwasababu anajua mkweree hawezi kumfanya kitu; ndio uswahiba wenyewe huo unaoua nchi hii!!
     
  13. L

    Liky Senior Member

    #13
    Oct 12, 2012
    Joined: Apr 2, 2012
    Messages: 176
    Likes Received: 3
    Trophy Points: 35
    Mlacha,mkandara na kikwete wote ni wale wale.wanawekwa kwenye vyuo kukandamiza haki.kuna watu weng wana taaluma ya uongozi lakini wanawaacha na kumpa mlacha mtaalamu wa kiswahili
     
  14. Pangaea

    Pangaea JF-Expert Member

    #14
    Oct 12, 2012
    Joined: Jun 14, 2012
    Messages: 202
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
     
  15. kadoda11

    kadoda11 JF-Expert Member

    #15
    Oct 12, 2012
    Joined: Jan 6, 2011
    Messages: 9,596
    Likes Received: 1,529
    Trophy Points: 280
    mmh!!hizi sasa porojo.mbona wadau wakubwa wa maswala ya elimu ya juu nchini wanadai mzee wa watu Chachage alijifia kwa maradhi haya ya siku hizi.Pamoja na kupenda kwake kuvuta sana Sigara.
     
  16. Ronal Reagan

    Ronal Reagan JF-Expert Member

    #16
    Oct 12, 2012
    Joined: Nov 4, 2010
    Messages: 3,690
    Likes Received: 185
    Trophy Points: 160
    Surprised NO. Sad YES.

    Sishangazwi na majibu yake, he's a confirmed arrogant dumb.

    Ni kielelezo cha hasara ya kuteua watu kwa kujuana au kwa u-kada. Huyu Prof. hafai hata kusimamia kitengo kidogo hapa UDSM.

    Ndio maana pia roho mbaya na majungu vimetia mizizi miongoni mwa wafanyakazi, very sad.
     
  17. Githeri

    Githeri JF-Expert Member

    #17
    Oct 12, 2012
    Joined: Apr 2, 2012
    Messages: 820
    Likes Received: 7
    Trophy Points: 35
    Nakubaliana na hoja zako 100 percent. Aibu sana kwa wasomi kutosimamia na kuhoji haki zao....Umewapa ukweli!
     
  18. Lukolo

    Lukolo JF-Expert Member

    #18
    Oct 12, 2012
    Joined: Dec 2, 2009
    Messages: 5,125
    Likes Received: 34
    Trophy Points: 145
     
  19. Zipuwawa

    Zipuwawa JF-Expert Member

    #19
    Oct 12, 2012
    Joined: Nov 28, 2010
    Messages: 2,956
    Likes Received: 7
    Trophy Points: 135
    Prof Mukandala hakika anajeuri ya ajabu.....inatokana na kubebwa sijui hata maprof wenzie wanamchekea kwanini? Sasa hivi Chuo amafanya kama banda la kuku wake anaamua anachotaka.
     
  20. Zamaulid

    Zamaulid JF-Expert Member

    #20
    Oct 12, 2012
    Joined: May 25, 2009
    Messages: 14,613
    Likes Received: 3,913
    Trophy Points: 280
    kwani hujui huyo VC ni kabila gani!
     
Loading...