Hoja na Haja za Dkt. Tulia kuwa Spika wa Bunge

HOJA NA HAJA ZA MHE DKT TULIA KUWA SPIKA.

Na Elius Ndabila
0768239284

Ndani ya Chama Cha Mapinduzi mbio za kumpata Spika baada ya aliyekuwa Spika Mhe Jobu Ndugai kutangaza kujiuzulu wiki iliyopita.

Wapo Makada wa CCM ambao wamekwisha kuchukua fomu na wapo wanaotajwa kuwa wanataka kuchukua fomu. Leo ninataka nimzungumzie Dkt Tulia.

Uwezo binafsi, Uhodari katika kuchanganua mambo, Umahiri katika uga wa Sheria, Uzoefu katika shughuli za Mhimili huu ni sehemu ya sifa mhimu alizonazo Dkt Tulia.

Hivyo hoja ni kuwa Uzito na Unyeti wa nafasi yenyewe inayobeba Mhilimili, inahitaji mtu hodari, Shupavu, Mahiri na Mzoefu. Dkt Tulia anavyo vigezo hivyo vyote. Nafasi ya Spika tena kwenye Bunge linalotunga tunga Sheria, Bunge linaloishauri Serikali na kupitisha Bajeti ya Serikali halihitaji tu kuwa na kiongozi Munyenyekevu na Mtii, bali mtu ambaye ni Mahiri kwa kujua madhara na faida ya kila jambo linalopita Bungeni.

Uzoefu Mkubwa alionao Dkt Tulia nje ya Bunge na Miaka sita aliyohudumu kama Naibu Spika ni inshara tosha kuwa hii nafasi anauwezo Mkubwa wa kuitendea haki.

Dkt Tulia alizaliwa mwaka 1976, Bulyaga Tukuyu. LL.B na LL.M alisoma UDSM huku akisoma PhD yake Cape Town. Alikuwa Mjumbe wa Bunge la Katiba, amefanya kazi ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kama Deputy Attorney General, amewahi kuwa Mbunge wa Kuteuliwa na akawa Naibu Spika. Mwaka 2020 aligombea Ubunge Jimbo la Mbeya mjini alishinda na baadaye akashinda nafasi ya Naibu Spika kwa awamu ya pili.

Wapo waliochukua fomu, hawajafanya kosa kwa kuwa wametumia haki yao ya kidemokrasia. Lakini kwa kuwa tunaangalia masilahi mapana ya nchi kwa na Uzito wa nafasi yenyewe, kwa wakati huu Dkt Tulia anatosha.

Ninatambua Chama Cha Mapinduzi kinamichakato mingi mpaka kumpata Mgombea wake. Lakini pia ninaamini pamoja na mambo mengine Chama kinazingatia maoni ya wadau na wakati ambao nchi inapitia. Matarajio na Matamanio ni kuona Dkt Tulia ambaye anefanya kazi kama Naibu Spika anapewa fursa ili kwenda kuongeza na kuboresha Mhimili mhimu wa nchi.

HAJA ya Mhe Tulia kuwa Spika ni kwa kuwa Uzoefu wa Miaka ya hivi karibuni baada ya baada ya Mapinduzi makubwa ya kisera na kisiasa Spika amekuwa anatokana na nafsi ya Naibu Spika. Tulimpata Mhe Mama Makinda, tulimpata Mhe Ndugai na haitakuwa dhambi tukimpata Spika Dkt Tulia aliyepikwa kwa Miaka 6 kwenye nafasi ya Unaibu.
Labda ni mimi, huwa namuona huyu mama kama ana dharau na udikteta, hasa alipokuwa ana"deal" na wabunge wa upinzani.
 
Yaani spika ambaye kaiba kura za Sugu! Mbeya wanajua Sugu alipata kura zaidi😂 maigizo kwelikweli ….. kazi iendelee bado sana nchi yetu kwenye demokrasia!
Uwizi ni jinai,mbona hatukumuona sugu akifungua kesi ya kuibiwa kura? Sugu mwenyewe anajua kwamba Dr Tulia ni uzito wa juu kwenye siasa za Mbeya.
 
Chini ya Tulia bunge litakuwa dhaifu kupita mabunge yote yaliyopita. Bunge sio kitengo cha ikulu , bunge ni mhimili unaowakilisha mawazo ya wananchi. Kama serikali imekosea bunge lazima lisimame kukosoa. Huyu atakuwa puppet was ikulu hakuna jipya. Ninachofurahia bunge hili wamejaa CCM , kama upinzani wangekuwepo angetafuta sifa kwa kuwaumiza upinzani hasa CHADEMA. I'll ionekane anafanya kazi.

Tunahitaji maspika Kama msekwa na sitta. Sio mtu anasema wazi sio lazima serikali ikubali ushauri was bunge.
Kwani sita na msekwa wamewahi kuwa tofauti na mkuu wa nchi?
 
Back
Top Bottom