HOJA MBADALA: Tuhamasishe CCM imsimamishe Membe 2015?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,104
Reaction score
43,357
Ukiangalia sana kati ya viongozi wengi wa CCM na walioko serrikalini Membe ndiye anayeonekana kuja kuweza kumudu kuwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama hicho.

Ukimlinganisha na wagombea wengine (hasa Lowassa aliyejiuzulu kwa kashfa) ni Membe tu ambaye anaonekana kulindwa na mlolongo mkubwa wa kashfa mbalimbali na japo - kama nilivyosema wiki kadhaa nyuma - hajajiandaa kuwa Rais ni wazi miaka hii miwili iliyobakia inaweza kumsaidia kujitengenezea na kuwa a true "presidential candidate"

CCM ikimsimamisha Membe kama mgombea wake inaweza kuwa na nafasi ya kushinda tena kiti cha Urais; wakimsimamisha mtu mwingine yeyote itakuwa ni mwisho wa utawala wa CCM.

Ni kweli?
 
Mkuu Mwanakijiji,Subiri kashfa ya pesa za Libya ndio utawajua vizuri wanasiasa wetu wana sura gani ni mapema mno kumjadili huyu nyoka wa mdimu.Ni bora mchawi Lowasa tumkabidhi mwana.
 
Naona itawasaidia sana cdm kushinda! Hizi enzi si tu mtu anabebwa na chama kama ilivyokuwa kwa Mkapa "95, bali pia mtu nae anakibeba chama kama Dr Slaa "10! Membe doesnt fit in any how!
 
si kweli,,,,,maana sisiem hapo ilipo inatumia rafu tu kukaa madarakan ila hata wenyewe wamechoka
 
Kama nimekusoma vizuri Mzee Mwanakijiji umesema "Anaweza kushinda" mimi nadhaini yeye ndiye angalau hajachafuka sana kama hao wengine so anaweza kuleta upinzani!! Ingawaje kwakweli magamba wasahau 2015
 

kwa sisi watu wa intelejensia tunafahamu fika kuwa wewe mwana kijiji ni mpambe wa karibu wa membe, hapa jukwaani umekuja kupima upepo wa huyo rafiki kipenzi chako, kwa taarifa yako ni heri mara mia ya lowasa kuwa rais kuliko an hypocrite in born character benny membe. Naomba umwambie rafiki yako pengine mtaonana US leo au kesho kuwa mmekwama na mipango yenu tunaifahamu tunasubiri muda tu tuwalipue.
 
Membe amekosa uthubutu katika uongozi wake.Tanzania ya sasa inahitaji kiongozi jasiri katika kukabiliana na maamuzi na changamoto mbalimbali ziilizopo.Aina ya watu kama Membe ni wa kupokea maagizo tu na kutumwa siku zote.
 
Kaka mara hii umeishakachuliwa hadi kuwa kuwadi wa mafisadi kama si nepi yao?

Huyo Membe amekupa nini hadi umzimie na kumuabudia hivyo ndugu yangu? Kweli adui yako muombee njaa na penye udhia penyeza rupia. Yaani mihemko yako yote ya miaka yote umeishia hapo? Kwanini siku hizi watu wanashabikia uchanguuu hadi kwenye mawazo yarabi?

Heri ungenyamaza kuliko kuvua nguo mtoni usijue kuna watu. Heri kuamini kwenye unachohubiri hata watu wakakucheka kuliko kuramba matapishi yako. Pole sana bwana mdogo. Je huduma yako unauza bei gani?
 
Mzee Mwanakijiji,

Sintopendekeza mtu isipokuwa kwa manufaa ya taifa na japokuwa Membe ni kichwa, muweza ukiachana na habari za Ufisadi wake maana huko CCM hakuna msafi kihivyo. Wayahudi walilaaniwa tena na Mungu mwenyewe lakini bado wanaitawala dunia.

Hivyo pamoja na utetezi wako bado nakuhakikishia kwamba CCM wataweza tu kushindana ikiwa watamsimamisha Asha Rose Migiro na hii itatokana na WANAWAKE kutumia kauli mbiu ya TUKIWEZESHWA TUNAWEZA. Itakuwa sio swala la chama bali wanawake against the rest...Na amini maneno yangu watu hawatatazama tena nyuma wala kutazama uwezo wa AshaRose isipokuwa ni mageuzi ambayo kwao yatawalemaza akili..

Kwa upande wa ushindani na hasa Chadema wanatakiwa kuanza mapema sana kumtafuta na kumwandaa mgombea japo kwa siri lakini nawatahadharisha mapema - KAZI IPO 2015 wajipange mapema na vizuri sana laa sivyo itakuwa aibu maana elimu ya Uraia haijazama vichwani mwa wananchi hivyo SHIDA na MATATIZO yanatangulia Mapenzi yao..
 
Mtazamo wangu juu ya Mh. Membe kama chaguo la ccm kwa nafasi ya Urais-2015 nilishautoa hapa toka 27th December 2011 13:56:

 
Wala haifanani na issue ya Zitto.
Dah! yaani mtu unakuwa hater hata nikiambiwa wewe ni mlozi sitakataa.
Waachie vijana wapete, we kaa pembeni na vikongwe wenzio ..... time's up!!
 
Hivi huyu Membe hayupo kwenye list!
 
Omutwale asante sana umedadavua fresh kabisa mdau,,,,mimi kila siku huwa napochangia kuhusu membe huwa siach kugusia suala la MTAMA,,,,ukitaka maoni kwamba agombee asigombee waulize wana mtama
 

unamaanisha nini kuwa KICHWA,,,,,
USHAHIDI????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…