Hoja kuhusu uhalali (legibility) wa kuwa mbunge

Hoja kuhusu uhalali (legibility) wa kuwa mbunge

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
457
Reaction score
773
67.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge endapo-
  • ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
Suala hili hata kwenye rasimu ya katiba mpya halijabadilika

Hii ni moja kati ya kitu cha kuangaliwa kwa ukaribu sana, ikumbuke kipindi tunatengeneza katiba hii kulikuwa na idadi ndogo ya wasomi, na hivyo katiba ikataka yeyote mwenye uwezo wa kusoma na kuandika kuwa mbunge ili kuwasemea wengi wasiojua kusoma.

Kama mtakumbuka maswala ya UPE nk ili kufanya watu wajue kusoma na kuandika.

Kwa ulimwengu wetu wa sasa ambao literacy rate imepanda kwa kiasi kikubwa ni upuuzi kukiendeleza kipande hiki cha sheria, na naweza kuto hoja zifuatazo.

  • Mbunge mbali na kuwawakilisha wananchi bungeni pia huhusika kwenye mchakato wa kupitisha miswada mbali mbali kuwa sheria. Hapo inahitaji walau utaalamu wa mambo hayo ambayo hayatokani na kujua kusoma na kuandika tu. Yaani unaweza kujua kusoma na kuandika lakini usiwe mzuri kwenye kujadili masuala ya kodi, uwekezaji, nk. Hapa kunaweza kupelekea sheria mbaya kuendelea kuwepo nchini
  • Kwa sasa wao wahitimu wengi wa shahada mbalimbali ikiwemo sayansi ya siasa, ili kuepuka tatizo la ajira kwa vijana ni vyema kuwapa kipaumbele wenye elimu kwenye masuala ya kisisasa ili kutatua suala hilo lakinipia kuipa tija mijadala inayoweza kuwa inaendelea bungeni
HOJA YA MSINGI.

Suala la kujua kusoma na kuandika lilikuwa kipindi kile ambacho waliokuwa wanajua kusoma na kuandika walikuwa wachache, kwa sasa tunao wengi hivyo ni vyema kubadili kipande hicho kama tulivyofanya marekebisho kwenye sheria nyingine.

Signed
OEDIPUS
 
Lazima uwe mwanachama wa chama cha siasa..!

Natamani kugombea ubunge 2020 ila fitina na matumizi ya pesa ndani ya vyama ni nyingi mno.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usibague watu,elimu au maarifa yamerahisishwa mno kupitia njia mbali mbali hata kupitia Google ni shule tosha kupata maarifa.
Labda tungewashawishi wanasheria kugombea ubunge na udiwani.Ingetusaidia katika kutunga sheria au kurekebisha sheria.
 
Jiulize uwezo wa mtu asiyejua kitu kuhus uhusiano wa kimtaifa/uwekezaji/kodi anakaa kujadili sheria kuhsu mambo hayo kwa kuwa anajua kusoma na kuandika.

Nenda kasome kokote unakosoma lakini uje na certification inayoweza kuonyesha kuwa na ujuzi wa jambo fulani
 
Ibadilishwe wawe na degree ili tupunguze na watoa mipasho kule mjengoni, na hawa wabunge wa viti maalum wafyekelewe mbali maana wengine ni vimada tu wanajaza nafasi na kuwapotezea muda wabunge wa majimbo kuchangia hoja za wananchi
 
ndio maana ya nchi yetu kuwa na katiba isiyo na ubaguzi,hatuwez kubaguana kw misngi ya ukabila,kipato,elimu,wala ukanda,nchi yetu ni kw ajr ya woote,woote wana haki sawa kw mjibu wa katiba ya nchi yetu,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndio maana ya nchi yetu kuwa na katiba isiyo na ubaguzi,hatuwez kubaguana kw misngi ya ukabila,kipato,elimu,wala ukanda,nchi yetu ni kw ajr ya woote,woote wana haki sawa kw mjibu wa katiba ya nchi yetu,

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo ni ombwe! Illusion kabisa, ubaguzi upo kila sehemu

Unajua watu wanaofanyakazi BoT wanatoka wapi?

Unajua bila kuwapa wataalamu kipaumbele mtakuwa mnatengeneza matatizo yapi?
 
Mimi kwanza niende kwenye somo la lugha.

Unachanganya maneno mawili tofauti ya kiingereza.

Legibility na eligibility.

Neno ulilotakiwa kutumia ni eligibility.

Eligibility ni hali ya kuwa na sifa zinazotakiwa au uhalali wa kuwa na nafasi fulani.

Legibility ni hali ya kitu kuweza kusomeka kirahisi.

Kwa muktadha wa maneno yako, kichwa kilitakiwa kutumia neno eligibility, si legibility.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikija kwenye sifa za ubunge, mtihani mkubwa wa mtu kuwa mbunge ni kuwatongoza viongozi wa chama na wananchi mpaka wampigie kura.

Huu ni mtihani mkubwa kuliko degree pengine.

Haifai kuweka vikwazo vya usomi kwa mbunge.

Kwa sababu, vikwazo hivyo vinaweza kupunguza demokrasia.

Wananchi wenyewe wanatakiwa kuamua huyu msomi atatufaa, na huyu msomi lakini hatufai, na hiyu si msomi lakini atatufaa, na hiyu msomi atatufaa.

Ukianza kuweka vikwazo vya usomi, watu wataanza kuweka vikwazo maalum kwa kukata watu maalum.

Ndiyo mambo aliyofanyiwa Samuel Sitta hayo. Watu walitaka kumkata, wakasema "mwaka huu tunataka Spika mwanamke".

Au mambo aliyofanyiwa Lowassa, watu wakasema "safari hii mgombea urais asizidi umri fulani".

Ukitaka kuondoa wabunge wasio na elimu rasmi bungeni, pandisha kiwango cha elimu kwa jamii nzima. Utaona hata bunge linaakisi elimu ya jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipengele cha kujua kusoma na kuandika kimepitwa na wakati ,sasa ni utandawazi , elimu ni muhimu sana . Hata kama una kipaji cha kuongea bila elimu ya kutosha ni bure . Kama mbunge umechaguliwa kusimamia kamati ya uchumi na pesa , utaongea nini kama huna elimu? Utaishia kugonga meza kwa hasïra ukiwaza wanakuonea (ifiriority complex) Hicho kipengele kiondolewe , badala yake (mwenye degree ya chuo kinachotambuliwa kisheria)

Kwanza kabisa, elimu ni nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikija kwenye sifa za ubunge, mtihani mkubwa wa mtu kuwa mbunge ni kuwatongoza viongozi wa chama na wananchi mpaka wampigie kura.

Huu ni mtihani mkubwa kuliko degree pengine.
Haifai kuweka vikwazo vya usomi kwa mbunge.
Kwa sababu, vikwazo hivyo vinaweza kupunguza demokrasia.
Wananchi wenyewe wanatakiwa kuamua huyu msomi atatufaa, na huyu msomi lakini hatufai, na hiyu si msomi lakini atatufaa, na hiyu msomi atatufaa.
Ukianza kuweka vikwazo vya usomi, watu wataanza kuweka vikwazo maalum kwa kukata watu maalum.
Ndiyo mambo aliyofanyiwa Samuel Sitta hayo. Watu walitaka kumkata, wakasema "mwaka huu tunataka Spika mwanamke".
Au mambo aliyofanyiwa Lowassa, watu wakasema "safari hii mgombea urais asizidi umri fulani".
Ukitaka kuondoa wabunge wasio na elimu rasmi bungeni, pandisha kiwango cha elimu kwa jamii nzima. Utaona hata bunge linaakisi elimu ya jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly! For we've seen a professor (in the same parliament) boast himself that he has been brought from the trash! Kama Profesa anadai ametolewa jalalani (Chuo Kikuu cha DSM), tutasema tupo serious?
 
Kiranga - kajaribu kusoma kwa makini kuhusu informal education na formal education , ili upate mwanga kuwa elimu ni nini . Namaanisha elimu ya darasani na nje ya darasa

Kuna watu wana Ph.D lakini si wasomi, wana ubinafsi sana. Tuwape uongozi?

Kuna watu hawana hata bachelor, lakini ukiuliza sababu hawana bachelor zinakuwa so imoressive kuliko hiyo bachelor. Mtu aliamua kuacha nafasi ya kusoma ili afanye kazi aitunze familia yake masikini na kusomesha wengine.

Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza John Major hakuwa na degree. Rais wa zamani wa Brazil Lula da Silva hakuwa na degree.

Hao wote wanaheshimiwa sana.

Lula hakuwa na degree, lakini alikuwa kiongozi wa vyama vya wafanyakazi tangu mdogo sana, uzoefu wake kwenye hayo mambo ulikuwa kama Ph.D. Sasa mtu kama huyo unaweza kumkatalia uongozi kwa sababu hana degree?

Napenda sana usomi, napenda pia elimu rasmi na ma degree, lakini sioendi ulimbukeni wa kuangalia degree kama ni shortcut ya usomi.

Kuna watu wasomi na hawana degree, na kuna wenye Ph.Ds ambao si wasomi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga - kajaribu kusoma kwa makini kuhusu informal education na formal education , ili upate mwanga kuwa elimu ni nini . Namaanisha elimu ya darasani na nje ya darasa

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajuaje sijasoma vizuri informal na formal education? Nineongelea hizi habari kwa mifano ya John Major wa Uingereza na Lula da Silva wa Brazil.

Utasemaje sijasoma haya mambo?

Na kama unatambua umuhimu wa informal education, kwa nini kigezo cha kujua kusoma na kuandika kwenye ubunge kiwe issue?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiulize uwezo wa mtu asiyejua kitu kuhus uhusiano wa kimtaifa/uwekezaji/kodi anakaa kujadili sheria kuhsu mambo hayo kwa kuwa anajua kusoma na kuandika.

Nenda kasome kokote unakosoma lakini uje na certification inayoweza kuonyesha kuwa na ujuzi wa jambo fulani
Katika dunia ya leo inayotaka diversity, mara nyingine mtu asiye mtaalam ndiye anaweza kuchangia vizuri kuliko mtaalamu.

Kwa sababu, mtu asiye mtaalamu mwenye usomi wa asili, wa kujifundisha mwenyewe (autodidact) anaweza kuuliza maswali yanayoibua makosa yaliyo katika masomo ya kitaalamu.

Wataalamu wote wanaweza kuwa wamekariri masomo ya jamii ya Uingereza ambayo hayana uhalisia Tanzania.

Wakawa wamekubali makosa, kupata ma degree yao.

Akaja mtu asiye mtaalamu ambaye yeye hajafundishwa makosa, akauliza swali dogo tu kutokana nanuzoefu wake wa jamii ya Tanzania.

Swali likaibua mjadala unaoonesha wataalamu wamekariri, asiye mataalamu kaonesha udhaifu wao.

Hivyo, ni vizuri kuwa na wataalam, wasomi, na pia, ni muhimu kuwa na watu wanaoangalia mambo kwa hali ya kawaida kwa utashi tu.

Tatizo letu Tanzania kuanzia hao wanaoitwa wasomi mpaka hao wasiosoma wote tunaburuzwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ubunge ni kazi ya kisiasa kama ilivyo urahisi hauitaji usomi wetu wa viuo vikuu. Siasa ktk jamii si taaluma ni jinsi ya kutumikia jamii. Ndo maana hakuna taaluma ya urahisi duniani bali ni ushawishi wa hisia ktk jamii inayokuongoza. Trump wa marekani hajawai kuwa hata karani serikalini leo ni mwamba na mtemi wa dunia kwa ushawishi wa kisiasa. Jiulize wabunge Maprofesa bungeni wametusaidia nin. Ulitakiwa ktk post yako utuwekee comparison kati ya majimbo ya wabunge wasomi dhidi ya majimbo ya wasio wasomi ilii tulinganishe. Tathimini ya haraka majimbo ya elimu ya kawaida wanafanya vzr zaidi.

Mimi swali moja sijajibiwa.

Wananchi hawa wanaolalamikia usomi (wa darasani) wakipewa uchaguzi.

Wachague kiongozi kati ya watu wawili.

Mmoja ana Ph.D tatu, lakini mlafi kweli, anataka kujilimbikizia mali kuliko Mobutu, usomi wake umempa kiburi anaona kila mtu mavi tu.

Mwingine darasa ka saba hakumaliza, anajua kusoma na kuandika, lakini anajua kufuatilia mambo, ana heshimu watu, ana kiu ya kumaliza matatizo na anaweza kufanya kazi na wasomi chini yake.

Hapa uchaguzi wa kiongozi mzuri ni upi?

Ph.D tatu mlafi au huyu ambaye hajamaliza darasa la saba ambaye ana nia ya kweli na utashi kumaliza natatizo?

Wenzetu walioanzisha haya mambo ya mabunge kama Wamarekani na Waingereza hawana vikwazo vingi vya usomi kuwa mbunge.

Kwa sababu wanajua haya.

Wanajua mtihani mkubwa wa mbunge ni kukubalika na wananchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom