Ivi statement ni kutoshirikiana na ofisi nzima ya CAG au ni kutoshirikiana na CAG Prof Mussa Assad? If the second is true then hiyo position si ina kaimu CAG?Kufuatia kuhojiwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad na Kamati ya Maadili ya Bunge kuhusu kauli yake kuhusu udhaifu wa Bunge,hatimaye leo Bunge limepitisha azimio la kutoshirikiana na CAG. Bunge limesikiliza,limejadili na kupigia kura azimio hilo lililopendekezwa na Kamati ya Maadili.
Kutoshirikiana na CAG ni kutofanya naye kazi kwa kipindi cha uhai wa azimio la leo. Kihistoria, Bunge limekuwa likiunda Kamati Teule za Bunge kufanya uchunguzi juu ya tuhuma za ufisadi Serikalini. Ilitokea hata kwenye masuala ya Escrow.
Inapoundwa Kamati Teule ya Bunge kuchunguza ufisadi, utaalamu na uthibitisho wa CAG hauepukiki. CAG Prof. Assad ni nguli katika masuala ya udhibiti na ukaguzi akisaidiana na wataalamu wabobezi waliosheheni kwenye ofisi yake. Anaachwaje pembeni katika utendaji wa Bunge linaloisimamia Serikali na kupitisha bajeti inayopaswa kulindwa dhidi ya ufisadi?
CAG huwasilisha Ripoti zake za ukaguzi kwa Rais. Baadaye,Ripoti hizo huwasilishwa na kujadiliwa Bungeni. Ndimo hasa unapoibuliwa na kuanikwa ufisadi ambao ni adui mkuu wa Rais Magufuli na Serikali yake. Ripoti za CAG huitaji ufafanuzi wake. Asiposhirikiana na Bunge si kukwamisha vita ya ufisadi na kukosa ufafanuzi wa kitaalamu.
CAG haepukiki katika shughuli za Bunge.Nitaelewa vinginevyo kama azimio la Bunge linalenga kutoshirikiana na Prof. Mussa Assad in his personal capacity na si ofisi ya CAG. Kama ni zuio la kutoshirikiana na Prof. Assad binafsi,Bunge litakuwa limewasilisha ombi kwa Rais Magufuli kuteua CAG mpya.
Sent using Jamii Forums mobile app