Hoja fikirishi: Watanzania tufanyeje ili tuwe na vipato vikubwa?

Habari za mchana wakuu,

Baada ya habari na hasa tambo serikali iliyopita kuhusu nchi kuingia uchumi wa kati,ikibidi nijiridhishe kwenye vyanzo mbali mbali.

Ndio nikaja kugundua uchumi wa kati unaozungumziwa na watawala wetu kama njia ya kujisifu/kuonekana wanafanya kazi,ikiwa ni kama lengo la muda mrefu ni ule wa kipato cha usd kuanzia 3956.

Lakini kiuhalisia sisi tupo bado kwenye usd 1080,na hii imetokana na benki ya dunia kuweka vigezo vipya au kugawanya kua kutakua na lower middle income na upper middle income, sasa sisi tumeingia lower middle income lakini viongozi wetu wa kisiasa walikuwa waituaminisha kua tupo level sawa ya hio middle income countries economies.

......

Sasa tuje kwenye mada ikiwa hio higher middle income ya kuanzia usd 3955 hadi 12475, ndio iliokua target ya muda mrefu(kabla hio figure kubadilishwa, hivi karibuni).

Nikajiuliza sana kua usd 3955 ni kama milioni tisa hivi. Je, ni Watanzania wangapi wanaipata hio kwa mwaka?

Nikaja kugundua hata zaidi ya nusu(50%) ukichukulia wafanyakazi wengi Tanzania ni walimu, polisi, askari Magereza na wanajeshi wa vyeo vya kawaida tu. Je, mishahara yao kwa mwaka inafika laki tisa. Tukumbuke kipato kikubwa cha mfanyakazi ni mshahara.

Ni ukweli usiopingika wanaofanya kazi serikali kwa maisha ya Kitanzania ndio wanaonekana wana maisha mazuri kuliko kundi jingine la wakulima, wafugaji na wafanyabiashara ndogo ndogo.

Sasa ukizingatia bidhaa nyingi ukiacha za vyakula Watanzania huzinunua kutoka nje,ina maa ana kwa vipato vyetu vidogo tunatumia asilimia kubwa ya vipato vyetu kuagiza bidhaa nje ya nchi sawa na raia wengine wa nchi zingine wenye uchumi mzuri.

Sisi kama nchi tufanyeje angalau hata kwa hao wafanyakazi walio nusu ya wafanyakazi wote wawe na kipato cha kuanzia milioni tisa kwa mwaka, yaani usd 3955?

Jaribu kuimagine mtu kama daktari mwenye degree msahahara wake kwa mwezi ni chini ya USD 700, huyu mtu anafamilia,ana mke ana ndugu ana mahitaji mengine etc, na huyu ndio angalau mtu mwenye kipato kikubwa miongoni mwa watumishi wa eneo husika

Huyo mtu inabidi anunue gari inayotegenezwa na inayouzwa kwa bei za nchi za uchumi wa juu,anunue nguo,anunue mahitaji mengine yote zaidi ya 60% ambayo hayazalishwi nchini kwake etc.

Kwa kipato hiko?,hapo kumbuka kuna watu vipato vyao ni chini ya USD 200 tena wapo serikalini na sekta binafsi nakufanya biashara, sasa kiukweli watu wa aina hii tutaweza kweli siku moja tuvunje mnyororo wa umasikini na siku moja watoto wetu wawe wakulima wa kisasa, wavumbuzi na watu mbali mbali wenye tija kwa jamii kwa kipato hiko?

Ipo siku mtu atanunua hata usafiri zero km, ama km chini ya elfu 10 tu,kujenga nyumba imara itakayodumu kwa angalau miaka 50 tu?

Matokeo yake mtu unafanya kazi ili watoto wale tu,tena unakuta kwa kipato hicho cha USD 200, kama laki nne na nusu,unahudumia wanafamilia kama nane hivi, ukigawanya kila mtu ni kama elfu 50 kwa mwezi

Kuna haja ya sisi kama raia tuone tunfanyaje tufike wenzetu walipofika.

Tusilizike na hii hali ya maisha tuliyonayo kama mtu mmoja mmoja, jamii na nchi.

Tufanyeje waungwana ili tujikwamue kutoka hapa tulipo, basi angalau hata wafanyakazi wawe na hiko kipato cha uchumi wa kati.

Wakiwekeza wao hata sisi wa mtaani tutafaidika tu na uwekezaji wao na matumizi mbali mbali wanayoyafanya.

Kwa maisha ya Kitanzania hata mtu awe analipwa pesa kama yupo U.S.A basi lazima kuna ndugu yake au jamaa tu au rafiki,anaishi kama digidigi huko kijijini..

Unakuta ni mkurugenzi wa shirika flani anakula mamilioni ya mapesa sema ndugu zake ukiwaona utawaonea huruma.

Na kiukweli hawezi wapa hela wote wakatoboa,hii inaashiria hata kama mtu mmoja atajikwamua basi kwa kua amezungukwa na jamii masikini "impact" ya kujikwamua kwake haionekani.

Wadau wa jamii forum tupeni mbinu za kuondokana na huu unyonge,maana huwezi amini kipato cha raia wa Zimbabwe ni kikubwa kuliko hata raia wa TZ,yaani sisi ni katika ile kumi bora ya nchi masikini na sisi tupo yaani.

Umasikini so kitu cha kujivunia kabisa, imagine unakutana na msomi wa Tanzania taulo la mtumba, chupi, boxer, sidira kwa kisingizio ni nguo imara ila uhalisia hio boxer ikiwa mpya tu ni nusu ya mshahara wake,kama unabisha nenda mwenge,karume etc. Tufanyeje kama nchi kujikwamua hapa tulipo?

Note.
Hapa sizungumzii Watanzania wote bali nazungumzia watanzania wengi kundi linalofikia hata asilimia 90% ya maudhui ya huu uzi.

Mkuu hongera sana kwa kuwaza kwa namna hii kwani tulio wengi mawazo yetu yanawaza mambo tofauti sana na wew, Ni kweli hata mim huwa najiuliza kwanini sisi hatufanikiwi napata shida kidogo kutokana na rasilimali tulizo nazo kama nchi, ni kweli kuna baadhi ya mambo nafikri ndio yanaturudisha nyuma mfano;-

Mfumo wa elimu haumpi mtu maarifa ya kujitegemea kwa namna yoyote zaidi ya kuajiriwa kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu.Wenzetu Kenya wameshaliona hili na wamebadili mitaala yao ili mafunzo yawe kwa vitendo zaidi na kumjengea mwanafunzi uwezo wa kujitegemea.

Sera na sheria mbovu: Sheria zetu nyingi zinatungwa kwa malengo mabaya sana sana yakisiasa wakati mwingine hata hazitekelezeki lakin zinatungwa ili kukandamiza watu na kwa malengo ya kisisasa mfano unalima mazao yako serikali haijakupa chochote kama mbegu au mbolea lakini ukivuna unapangiwa bei na pa kuuza hii si sawa.

Uvivu na kubweteka: Mim sijatembea sana ila kwa kweli huko nilikojaaliwa kufika watu wanafanya kazi acha kabisa watanzania hatufanyi kazi tunacheza bila kujali ameajiriwa au anafanya biashara,mfano mbaya kabisa, unakuta kwa kuwa mjomba au shangazi kaka au dada anfanya kazi ndugu anatoka anaenda anakaa kwake anakula na kulala hata hana wasiwassi, hii kwa wenzetu ni tofauti kidogo.

Uongozi mbaya; Tumeona saivi zao kama parachichi ni Green Gold lakin angalia ile mikoa ambayo inalima parachichi hakuna efforts yoyote ya serikali ya kutafuta masoko na kuwahimiza watu walime zao hilo,hali kadhalika mazao mengine.Wanaotoka Sumbawanga ni mashahidi kule kulima mahindi ni uwezo wako wa kufyeka vichaka tu huhitji kutumia mbolea sjui UREA wala nini sasa hii nayo inhitaji mzungu aje kweli??

Mwisho kuna mahali umezungumzia kuvaa mitumba kinachofanya watu wavae mitumba ni kwa sabab ya purchasing power" nguo mpya wengi hawawezi kuzinunua hivyo basi ili tuweze kununua nguo mpya na vitu vingine ni lazima watu wengi wawe na uwezo wa kifedha ndipo viwanda vitajengwa na nguo zitazalishwa zenye quality nzuri kwa kuwa wanunuzi wapo hapo EPZ ubungo unaambiwa mpaka jezi za machester zinatoka hapo lakin hakuna mtanzania mwenye uwezo wa kuinunua na akiwepo ataenda kuinunulia UK.

Nini kifanyike: Tutunge sheria nzuri zenye kuwajali wananchi bila matabaka, tujenge uzalendo wa kweli wa kupenda bidhaa zetu, tuwainue wananchi kutokana na advantage yao mfano kama kwenu kilimo cha korosho kinakubali watu wahimizwe walime kwa ufanisi na watafutiwe masoko, kama ni dhahabu ( machimbo ) hivyo hivyo na tubdilishe mitaala ya elimu hata tukikopy sio mbaya kama tunacopy kwa faida ya kizazi kizuri cha kesho.
 
Uongozi huu WA vilaza , washenzi wezi wanaonenepesha matumbo na makalio Kwa wizi wa Mali za Uma na kuua biashara za wazawa kuwageuza wanyonge watumike kama mtaji WA kisiasa ?
Imagine kama kule bukoba.

Mtu analima kahawa au vanilla mwenyew yaan anaandaa mwenyew shamba,anapanda mwenyew,analima mwenyew,anavuna mwenyew na kuanika mwenyew wakati wa kuuza serikali inampangia bei na pakuuzia. Tena bei ndogo tena kiduchu wakati ukivuka border Tu ukaingia Uganda bei ya kahawa au vanilla ni mara tatu kama sio nne kuliko ya serikali inayowapangia wananchi.

Kama isingekuwa serikali kudidimiza wananchi Kwa vitu kama hivi tutabaki maskini milele .
Yaan zao kama ndizi na maharage yanaozea bukoba vijijini huko kisa kutoa hayo mazao kuuza mwanza au mikoa mingine Kodi kubwa as if bukoba ni nchi nyingine


Inasikitisha Sana na wakikusanya hizo Kodi sijui zinaendaga wap kama hata kijistendi cha huko bukoba ni matope
 
So inabidi uhakikishe ndani ya huo mwezi mmoja umepata kazi na kupata vibali vya kazi ili uweze kuishi kihalali.

Gharama za kuisho chakula /nyumba usafiri hali iko vipi?
Kuhusu gharama kwa kweli ni kubwa Sana mkuu.
Mfano chumba kimoja tu ni Hadi USD 1000 kwa mwezi ..sema chumba chenyewe ukikiona ni Kama unaweza kuwaga vyumba vitatu humo ndani

Life ni ghali lakini pesa ipo..

Karibu.
 
Pambana aisee.,....maisha yetu wa TZ ni ya kuoena huruma tu,tulio wengi.....kuna jamaa yangu amenunua Rav 4 ya Mwaka 1998,km zaidi ya laki,gari ina miaka zaidi ya 23 toka iundwe anatamba sana mtaani,wafanyakazi wenzake wanampa hongera kwa hatua aliyofikia......sio jambo dogo kusema kweli......lakini gari ina miaka zaidi ya 20?,mtu anapongezwa baada ya kuhurumiwa?.....umasikini mbaya wandugu,unatufanya tupate "fake respect" kwenye jamii baada ya kuonewa huruma
Ilmradi inasaidia kumfikisha anakoenda kwa haraka, hapigwi jua,mvua wala vumbi 😂😂😂 hongera kwake
 
Watu tunao,rasimali kibao,uongozi upo uliotukuka shida ni nini sasa?
Uongozi gani uliotukika?
Huu ujinga ndio unazidi kufubaza waafrika. Uongozi wa waafrika ni duni na ndio chanzo cha umasikini.
Binafsi kuanzia nyerere sijaona kiongozi alioweza kuwatoa umasikini watanzania.
Watanzania wengi nao ni chenga, wanasubiri viongzi walete maendeleo matokeo
yake viongozi wanawahubiria kuw wameisha waletea maendeleo.
Tuna maisha duni sana sana.
Watanzania tunatakiwa tijitafakari sana.
 
Pambana aisee.,....maisha yetu wa TZ ni ya kuoena huruma tu,tulio wengi.....kuna jamaa yangu amenunua Rav 4 ya Mwaka 1998,km zaidi ya laki,gari ina miaka zaidi ya 23 toka iundwe anatamba sana mtaani,wafanyakazi wenzake wanampa hongera kwa hatua aliyofikia......sio jambo dogo kusema kweli......lakini gari ina miaka zaidi ya 20?,mtu anapongezwa baada ya kuhurumiwa?.....umasikini mbaya wandugu,unatufanya tupate "fake respect" kwenye jamii baada ya kuonewa huruma
We jamaa umenifanya nicheke peke yangu aisee 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom