Hoja bungeni: Salvatory machemuli: Jembe la ukweli la chadema ukerewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hoja bungeni: Salvatory machemuli: Jembe la ukweli la chadema ukerewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Donyongijape, Jun 21, 2011.

 1. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  sikuwa nimewahi kabla kumuona au kumsikia huyu mbunge..kwa kweli leo amenidhihirishia kuwa cdm ina hazina kubwa sanaa ya viongozi makini ! ujengaji wake wa hoja,pace yake,umakini wake na kujiamini kwake ni outstanding. Kama kuna mtu anamjua kiundani zaidi atumwagie cv yake zaidi. Viva CDM
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mpaka Rev Masanilo kaipenda!!! Kweli Chadema ipo mambo.
   
 3. l

  lutelemba Member

  #3
  Jun 21, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  endeleeni kutujuza wanajf, maana huu ni muda wa mapambano ili kuondoa magamba ambayo yametumasikisha vya kutosha.
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ungetueleza kasema nini mbona munadhani wote tupo mbele ya TV zetu jamani wana JF musiwe wa choyo wa taarifa hebu twambie kasema nini kilichokufurahisha
   
 5. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwani yeye ni yardstick ya uwezo wa watu?
   
 6. A

  A Lady Senior Member

  #6
  Jun 21, 2011
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aisee huyu mbunge kanifurahisha na kunipa matumaini kuwa kuna watu makini.
   
 7. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,741
  Likes Received: 6,017
  Trophy Points: 280
  Heshima Mkuu. Kuna haja ya kujiuliza inakuwaje hivyo? Kwamba sehemu kubwa ya wabunge wa CHADEMA ni "majembe" ilhali kwa CCM ni kinyume (uozo)? Sitaki kuamini kwamba wabunge wote wa CCM ni vilaza kiasi hicho bali, nionavyo mimi, tatizo la CCM ni mfumo wao - NIDHAMU YA CHAMA hata kuruhusu unafiki kwa suala lisilo na tija kwa umma.

  Yaani, wabunge wenyewe wa CCM wamekubali kuwa watumwa wa fikra na mawazo hata kuruhusu chama chao kufikiri kwa niaba yao - utumwa mbaya kuliko aina zote za utumwa uliowahi kuwepo chini ya jua. Na hata CUF ambao siku za nyuma waliwahi kuwa watetezi wazuri Bungeni nao wanaelekea kwenye unafiki huohuo baada ya ndoa yao na CCM. UNAFIKI, UNAFIKI, UNAFIKI, ... hupofusha.

  Kuna haja kwa CHADEMA, from now, kuanza ku-pin-point, kwa kila jimbo la uchaguzi, watu ambao wanaona watafaa kusimamishwa kwa ajili ya ubunge na udiwani kwa uchaguzi ujao na kuanza kufuatilia mienendo yao tangu sasa na muda ukifika, ikibidi Chama kiwaombe wagombee. Next time hakuna kubakiza jimbo au kata kama ilivyotokea last time ambapo badhi ya maeneo hawakusimamisha wagombea - ikibidi hata Zanzibar na Pemba.
   
 8. c

  chumakipate Member

  #8
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 86
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hata mimi nimemkubali kwa kweli jamaa anajua kujenga hoja na kwa kweli alinifurahisha pale alipomjibu yule mjinga Mh.alipoleta taarifa ya kizushi na kumwaminisha kuwa yeye kweli ni waziri kivuli wa ujenzi kwa data alizompa za barabara ambayo haimo kwenye bajeti na kumhakikishia kuwa hata Magufuli analijua.CDM moto juu
   
 9. Rocket

  Rocket Senior Member

  #9
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu Jmaa alikuwa Mkandarasi pale Moro ,so ana baadhi Data za ukweli
   
 10. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #10
  Jun 22, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  aliponifurahisha mimi ni pale aliposema kuwa CCM ktk ilani yao ya Chama walisema kuwa kuna Barabara wataijenga kwa kiwango cha Lami...
  Then muheshimiwa Machemuli akasema huu ni uongo na hii ishu ni kuwadanganya wananchi...

  Kisha akakurupuka mbunge mmoja wa CCM asiyekuwa na haya na kusema taarifa kuwa eti Barabara hiyo ni miongoni mwa Barabara ambazo zinatarajiwa kuanza kutengenezwa hivi punde coz hata Rais mwenyewe alipokwenda kwenye kampeni kule aliwahakikishia wanachi''...

  Kisha kamanda Machemuli akainuka na kumnyamazisha yule ushuzi kwa kumwambia kuwa yeye Machemuli ni waziri kivuli wa Ujenzi na amemuuliza mh: Magufuli kuwa je hiyo barabara iko ktk mpango wa kuwekewa Lami?
  Na Magufuli akamjibu kuwa hakuna kitu kama hicho.

  So ule uharo wa CCM ulioinuka na kujaribu kuwapotosha wananchi kwa kuleta data za uongo na ili mradi mh: Machemuli aonekane mzushi hakuinuka tena na wala sikumuona hata Bunge lilipoisha.

  Forza Chadema...
   
 11. The dirt paka

  The dirt paka JF-Expert Member

  #11
  Jun 22, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tunda huwa halidondoki mbali na mti, lakini mwisho wa mapambano tusiulizane "NANI ALIFANYA KAZI KUBWA?" Maana kila kiungo wa timu ya CHADEMA product yake inauzito sawa na ya mwenzie na hawabebani.
  WAR FRONT CHADEMA LETS GO.
   
 12. Chizi Fureshi

  Chizi Fureshi JF-Expert Member

  #12
  Jun 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,710
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Hakuwa na mtiririko mzuri wakati anayaeleza matatizo ya watu wa ukerewe, ameshindwa kueleza kwa umahiri mkubwa matatizo hayo na jinsi bajeti hii inavyolenga kuyatatua, imeonyesha dhahiri LCM-Lusato Charles Machemli naluyaga alivyochuja! Nilisoma nae na alikuwa stadi ajabu. Nimefurahi presentation ya regia baada ya LCM, it was superb na hasa alipogusia kuwa walemavu hawahitaji misaada ya spoon to mouth! Ukitaka zaidi ni PM nikutanabahishe kuhusu LCM.
   
Loading...