HOJA BINAFSI: TAKUKURU Ivunjwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HOJA BINAFSI: TAKUKURU Ivunjwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsangulaKG, Oct 27, 2012.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Habari zanu wanajamvi,

  Kwanza niwashukuru wanajamvi wote wanapost habari zinazoonyesha wazi kukerwa kwao na vitendo vya rushwa.

  kwa siku za karibuni malalamiko dhidi ya vitendo vya rushwa yameongezeka maradufu. Mfano mkubwa ni malalamiko yamkambi mbalimbali za uchaguzi ndani ya CCM, malalamiko ambayo hata Rais Kikwete mwenyewe ameyatoa katika majukwaa. Vile vile, wakongwe wa CCM pia wamesikika wakilalama kuhusu rushwa. Wabunge pia wamehusishwa na rushwa ambayo kamati maalumu iliyoundwa ilikamilisha ripoti yake wakati ambao mbunge mmoja ana kashfa ya matairi ya TANESCO.

  Ni muda mrefu sasa TAKUKURU imekuwa kimya dhidi ya vitendo vya rushwa ambavyo hata Rais mwenyewe anaviona na kuvifahamauSwali kubwa ni kama Rais mwenyewe anaoushahidi wa vitendo vya Rushwa...je TAKUKURu wanafanya nini?

  Hivyo basi napendekeza TAKUKURU ivunjwe. Tume hii inatumia fedha nyingi za walipa kodi kuwalipa wafanyakazi ambao hawafanyi lolote. Pia, kuna tetesi kuwa Wafanyakazi wa TAKUKURU ni wapokea rushwa kupindukia. Tunaishi nao mtaani na wanapata maendeleo ya harakaharaka mno ambayo inasadikiwa ni kutokana na malipo ya fadhila za kuzima harakati za kuwafichua watoa rushwa.

  Napenda kuwaomba wanasheria waliomo humu jamvini kuangalia jinsi gani yaweza kutengenezwa motion ya kuivunja TAKUKURU.
   
 2. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  naunga hoja, cha ajabu bosi wao mwenyewe Rais JK amenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akikubali kua ndani ya ccm kuna rushwa lakini TAKUKURU wamekaa kimya kwanini wasimhoji mzee labda ana ushahidi....TAKUKURU are so incompetent and untrustworthy waivunjilie mbali...cdm mkichukua nchi hii ni taasis ya kwanza kuibomoa bomoa
   
 3. a

  artorius JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 758
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  tatizo si takukuru,tatizo liko pale magogoni.Just think in the angle of analytic mind.
   
 4. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  TAKUKURU ni janga la kitaifa,naunga mkono hoja
   
 5. m

  mhondo JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Isipokuwa chini ya Ikulu ndipo inaweza kufanya kazi vizuri.
   
 6. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Nilishasema hapa kuwa kama kuna watu wanakula hela za walipa kodi bure kabisa ni Dr. Hosea na IGP Mwema. Hawa watu ni hawafai kuongoza taasisi wanazoongoza
   
 7. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Hivi Dr. Hosea huwa anafanya Performance Review na Mwajili wake na kama ni ndiyo, ningependa kujua Objectives anazopewa kila mwaka. Nina uhakika huwa anapata Poor Performance kama mwajili wake anajua anachofanya
   
 8. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #8
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Tatizo sio Magogoni man, tatizo ni KATIBA .. KATIBA ya Sasa mfumo wote wa uongozi una Kichwa kimoja Na kiwiliwili kimoja, ukiadabisha mmoja unaathiri system yote hivyo bora uozo uachwe uendelee.. Kwa hiyo KATIBA la NCHI liundwe upya, baadhi ya kada zikasmiwe mamlaka inayojitegemea mbele ya Mahakama, Na Mahakama pia ziwe Na mfumo unaojitegemea. Lazima uvunjwe uongozi wa Kimiungu, Lazima kiongozi awe Na mipaka inayojitosheleza Na hofu kwamba analindwa Na kanuni, taratibu Na Sheria zilizopo.
   
 9. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwani hiko chini ya Ikulu na siyo chini ya Waziri MKUU!!!
   
 10. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 25,013
  Likes Received: 37,741
  Trophy Points: 280
  TAKUKURU,rushwa,ufisadi na cccccm ni watoto wa baba mmoja.Unatarajia nini hapo!
   
 11. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  CCM ndio ivunjwe, maana ndio mzizi wa matatizo yote!
   
 12. o

  obwato JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hiki kitengo hakina maana yoyote,kina kazi ya kuremba rushwa tu na wanachagua watu wa kuwakamata,wanaonea mahakimu wadogo, mapolisi wachache na kupiga mikwala kwenye halmashauri tu ili wapewe rushwa, nakumbuka walikuwa wakwanza kutoa tamko kuwa Richmond haikuwa na tatizo. Kuna mtumishi wao m1 chupuchupu atolewe roho mtukula mkoani Kagera watu walishamchoka alikuwa analazimisha rushwa mpaka kwa wauza mkaa.
   
 13. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu ni taasisi/idara gani ya Serikali inayofanya vizuri kiutendaji hata isivunje?
   
 14. Ngagarupalu

  Ngagarupalu Senior Member

  #14
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  .
  Hiyo hayifanyi kuto perform role zake.
  Dr. Hosea amewahi kusema hadharani kwenye interview
  1. Tatizo siyo PCCB bali ni sheria inayounda, kwani haimpi madaraka ya kupeleka kesi (mtuhumiwa) mahakami , inamtaka kupeleka fail la uchunguzi kwa DPP. DPP yeye ndo anayo maamuzi ya kushitaki au la!!

  2. Wafanyakazi wa TAKUKURU wana maisha bora sababu wamefanyiwa utaratibu wa mikopo toka benki na mishahara yao imeboreshwa, ili kuwaondelea ushawishi! kwa uhakika hayo nayakumbuka!!! kuyasikia toka kwa Mkuu huyo.

  My take: Hoja binafsi izingatie sheria inayounda PCCB, inaweza kuwalinda na kuonekana wametimiza nafasi yao, kosa ni ofisi ya DPP, pengine utaratibu wa sheria una mapungufu. Hoja binafsi ya kuvunja iangalie mamlaka ya PCCB yote na vikwazo vyake. kwanini kabla ya kuivunja hauoni haja ya kuirekebisha? unataka nini kuwa mbadala wa PCCB? "Is it broken that you can't fix it?"
  wajuzi wa sheri wapite hapa, tupate somo.
  wakatabahu.
   
 15. m

  maselef JF-Expert Member

  #15
  Oct 28, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 255
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  TAKUKURU is just "A toothless Bulldog"
   
 16. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #16
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,457
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono hoja 100%. Hata TISS na Polisi navyo vitazamwe kwa minajili ya kuvunjwa au total overhaul
   
 17. m

  mhondo JF-Expert Member

  #17
  Oct 28, 2012
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Itabidi kuvunja pia TBS, TFDA, MSD, EWURA, SUMATRA, POLISI, MAHAKAMA na vyombo vingine vingi maana baadhi ya watumishi wa hizo ofisi pia wanasababisha matatizo kwa kwenda kinyume na majukumu waliyopewa.
   
 18. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #18
  Oct 28, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Mlosi K. Mtulutumbi

  nakuunga mkono mkuu. Polisi wanaweza kufanya kazi hiyo wakilazimishwa kuwa waaminifu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #19
  Oct 28, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 280
  Kama wanavyosema watu siku zote kuwa TAKUKURU yenyewe ni wala rushwa wakubwa tu. In short, Kikwete hajawahi kufanya kitu cha maana katika utawala wake. Jiulize, ushawahi kuona au tu kusikia TAKUKURU imemkamata kigogo yeyote yule? Jibu ni hapana kwa sababu wanakula wote. Wale watu wadogo wadogo wanaokula chini ya milioni peke yao bila kuwagawia TAKUKURU ndo wanakamatwa, wanaoingizia taifa hasara zaidi wanacheka tu baa na machangu wao.
   
 20. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Well said mkuu, mimi binafsi nimewahi kusimuliwa na watu wawili tofauti walio wahi kuonja joto la jiwe la PCCB; those guys are really Professionals - awafanyi mambo ya ubabaishaji pale, nashangaa kusikia eti mafaili lazima yapitie kwa DPP!!
  Mimi mbona niliwahi kumsikia JK akisema wazi wazi kwamba PCCB itafanya kazi independently bila ya kuingiliwa na mtu yeyote hata yeye kama RAIS hatawaingilia katika kazi zao na atawapa vitendea kazi vyote na ofisi zenye hadhi za kufanyia kazi zao bila bugudha, JK is commited katika hilo.

  Inaonekana wazi wazi kwamba walio pitisha kipengele kupeleka kila kitu kwa DPP walikuwa na agenda ya kujaribu ku-contain PCCB isifanye kazi yake kiufanisi - siamini kama JK ana hafiki vipengele vinavyo punguza makali ya PCCB, actually kipengele hicho kinawapa baadhi ya watu ambao wako chini yake kujaribu kuingilia au kuzima baadhi ya tuhuma zilizo wazi, ndio maana nilisema PCCB ingefaa kuwa chini ya Waziri Mkuu, nalisema hili 4 a reason - we unafikili mfanya kazi wa PCCB hata kama anafanya kazi yake kiufanisi akaletewa kimemo/simu kutoka kwa mfanya kazi yeyote ndani ya ofisi ya Rais akiambiwa asiendelee ku-pursue tuhuma fulani - we unafikili anaweza ku-defy agizo hilo?- Hawezi!

  Don't U think aliyependekeza such skewed kipengele alikuwa na madhumuni ya kuwalinda baadhi ya watuhumiwa ambao wanaonekana ni untouchable!! No wonder Dr.Hosea anaonekana hajapewa autonomy ya kutosha deliberately, mimi napendekeza JK ampe full autonomy Dr. Hosea hawe Judge na executioner i.e apeleke case moja kwa moja mahakamani bila ya kumpitishia mafaili ya watumiwa DPP, kama Judge akiona kuna ulazima wa kumu-involve DPP wakati wa ku-appeal well and good.

  Mkuu wajuzi wa sheria ndio walihusika na utayarishaji wa sheria ya kuhunda PCCB in the first place, badala ya kutumia taaluma yao kwa manufaa ya TAIFA letu wanatumika kuongezea vipengere vya kujaribu kuwalinda baadhi ya waharifu incase wakitiwa mbaroni na PCCB, this was/is very frustrating indeed kwa Dr.Hosea na TEAM yake yote pale PCCB. Marekebisho ya sheria ya kuanzisha PCCB wapewe ma-lawyer wenye highiest integrity namely:Mzee Judge Walyoba, Prof.Shivji, Prof.Pragamandi Kabbudi, Dr.Mwakyembe na Judge LUBUVA; bila kufanya hivyo RUSHWA/UFISADI utalifikisha pabaya TAIFA letu.
   
Loading...