Hoja 8 za wanaolalamika Wanyama kupewa mtaa ubungo

Hoja 8 za wanaolalamika Wanyama kupewa mtaa ubungo

Nchi ya maajabu kila siku tunazidi kupuyanga
 
Jina ni Jina tuu tunashangaa Wanyama wakati kuna mtu anaitwa Chibuku na anashangiliwa..
 
Siku zote nitaendelea kuamini kuwa mapinduzi ya kweli katika taifa hili yataletwa na wananchi wenyewe baada ya kuchoshwa na kukinaishwa na utawala huu dhalimu wa CCM na sio wanasiasa ambao wameifanya siasa kuwa ni sehemu ya kujikusanyia mali na umaarufu.......

Ukweli ambao wengi wanaukwepa kuusikia ni kuwa hakuna mwanasiasa hata mmoja mwenye ajenda ya dhati ya na nia madhubuti ya kuwatumikia wananchi zaidi ya mbwe mbwe za majukwaani za kuwalaghai wananchi na kujipatia kura ili kuendesha maisha yao........

Na haya mambo ya kipuuzi tunayobishania hapa yanayofanywa na wanasiasa ni ushahidi kuwa wanasiasa wetu hawana ajenda za msingi za kuwafikisha wananchi kule walipotarajia baada ya kuwapigia kura......

Na ndio maana mpaka leo ukiacha ushabiki wa kisiasa na jazba za kipinzani huwezi kuona tofauti kati ya jimbo la lililo chini ya upinzani na lile la chama tawala.......zaidi ya kelele tu za wanasiasa huku wakiungwa mkono na wananchi waliopoteza uwezo wao wa kufikiria .......
5142e8480f41befb892170b7c95d2d2e.jpg
 
Back
Top Bottom