Hoja 8 za wanaolalamika Wanyama kupewa mtaa ubungo

Hoja 8 za wanaolalamika Wanyama kupewa mtaa ubungo

Kwa kuwa wewe ni poyoyo zuzu ulimwengu upo huku

Hata English uliyo iandika ipo kilumumba Lumumba
asante, mtanzania kukosea English sio habari, Ila Muingereza kukosea kiingereza ndio habari.
ila sina wasiwasi kwa jibu lako ulielewa vizuri mkuu
 
Nimeona uvivu kusoma, ila hilo jina la mtaa lilikuwa linawapa wananchi hata wa mtaa huo au eneo hilo faida gani haswa?

Mnaoyajua mtufunze wengine!!!
Jarida kubwa la uingereza leo limetangaza wanyama kapewa mtaa Tanzania ni moja ya advantage kubwa sana
 
Kwani wewe yule azikiwe amekupa nini ??

We kila siku nakwambiaga unawaza kwa kutumia masaburi yako

Mtaa uliyopo ofisi ya mazwazwa unaitwa Lumumba

Huyo Lumumba kaeasaidia nini


Umeona niliyoandika yanataka wewe uniulize maswali... eeeeh fikiria nje ya bix mnatia aibu watu kama wewe... shaaaa pita hukoooo

Na uwaambie waweke documents za hatua zote... ila kiki imebuma ha ha haaa

Haya ngoja nikasikilize redio safwiii nayo ni Clouds FM
 
Nimeona uvivu kusoma, ila hilo jina la mtaa lilikuwa linawapa wananchi hata wa mtaa huo au eneo hilo faida gani haswa?

Mnaoyajua mtufunze wengine!!!
halikuwapa faida wala halikuwapa hasara, wangeliacha tu

ni siasa za bongo tu kuzinguana wanatia aibu sana

halaf Coco sio kwa kunisusa huko jaman
 
Nimeona uvivu kusoma, ila hilo jina la mtaa lilikuwa linawapa wananchi hata wa mtaa huo au eneo hilo faida gani haswa?

Mnaoyajua mtufunze wengine!!!
Kama kuitwa Wanyama hakungewaletea hasara ngoma ingekuwa droo.
Maana jina la awali lilikuwa lipolipo tu!!
Bora jina la wanyama linaweza kutushushia wakala mmoja kutoka EPL kuja kusaka vipaji.
 
Uzi mreeefu point sifuli.sio kila kitu cha kutete tu et kwakua wamefanya ukawa.we we na vijana wa rumumba wite mnahitaji elimu ya fikra
 
Umeona niliyoandika yanataka wewe uniulize maswali... eeeeh fikiria nje ya bix mnatia aibu watu kama wewe... shaaaa pita hukoooo

Na uwaambie waweke documents za hatua zote... ila kiki imebuma ha ha haaa

Haya ngoja nikasikilize redio safwiii nayo ni Clouds FM

Nje ya bix ndio wapi we zwazwa
 
Ni Tanzania ambapo masuala ambayo hayana impact chanya katika maisha yao yanachukua nafasi kuu kwenye mijadala wakati masuala yenye kuwagusa kimaisha hayachukui nafasi.

Tanzania kuna vituko!

Kweli kabisa,hii imekua mada kubwa sana kwa Uvccm.
Mpaka Makonda kaamua kuingilia kati.
 
Tatizo kubwa ni kuwa utaratibu haukufuatwa!

Utaratibu uliopaswa kufuatwa
1) Jina hupendekezwa na Kamati ya Mtaa husika ( sio Mayor)

2) Mapendekezo kupelekwa Kwny Vikao vya Kata ( WDC)

3) Mapendekezo ya WDC hupelekwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa
Mkurugenzi hupeleka Pendekezo kwny Kamati ya Fedha na UongoZi
Then Jina Pendekezwa hupelekwa kwny Baraza la Madiwani
Halafu huepelekwa DCC na RCC

Halafu Jina Pendekezwa hupelekwa Ofisi ya Rais ( Tamisemi)

Tamisemi hupeleka Jina kwa Mchapaji Mkuu wa Serikal
Mwishowe Jina hutangazwa kwny Tangazo rasmi la Serikli GN.

Jee Mayor wa Ubungo alifuata huu utaratibu?
 
MASWALI YA KIPUUZI YA VIJANA WA CCM NA MAJIBU MAKINI YA VIJANA WA UPINZANI.

SWALI: Kwanini Victor Wanyama amepewa mtaa na si Mbwana Samata?

JIBU: Kumpa Victor Wanyama jina la mtaa hakuzuii Mbwana Samata kupewa. Kuna mitaa mingi haina majina, Samata anaweza kupewa mmoja.

SWALI: Kwanini Mayor Bonny hakumpa kwanza Samata jina la mtaa kabla ya Wanyama?

JIBU: Si lazima Bonny afanye yote. Mameya wengine wanaweza kufanya pia. Zaidi ya 70% ya halmashauri zipo chini ya CCM. Mameya wa CCM wana nafasi kubwa zaidi ya kufanya kuliko mameya wa UKAWA ambao ni chini ya 30%.

SWALI: Samata ameanza kupeperusha bendera kimataifa tangu 2010 kwanini msingeanza naye?

JIBU: 2010 halmashauri zote za Dar Es Salaam zilikuwa chini ya CCM, walaumuni mameya waliokuwepo kwa kushindwa kuliona hilo.

SWALI: Wanyama ameifanyia nini Tanzania?

JIBU: Tanzania kuna mtaa wa Azikiwe,
Je, Hayati Nnandi Azikiwe aliifanyia nini Tanzania? Au Kwame Nkurumah? Au Sam Nujoma, wote hawa waliifanyia mini Tanzania?

Kenya kuna mtaa unaitwa Sokoine,
Je, Sokoine aliifanyia nini Kenya? Uingereza kuna mtaa wa Mwl.Nyerere,
Je, Nyerere aliifanyia nini Uingereza?

SWALI: Samata ni mtanzania wa kwanza kucheza Soka la Ulaya mbona hamjamuona?

JIBU: Tutengeneze mfumo wa kuwaenzi mashujaa wetu wote sio Samata tu. Filbert Bayi ni mtanzania wa kwanza kupata medali ya dhahabu katika riadha kwenye olympic, mbona hajawahi kuenziwa?
Mbona hakupewa mtaa na halmashauri zote zilikua chini ya CCM?

Saada Bint Said ni mtanzania wa kwanza kuimba nyimbo za ukombozi barani Afrika kupitia taarab na anafananishwa na Miriam Makeba wa Afrika Kusini, mbona hakumbukwi na hakupewa japo mtaa?
Tena wakati huo CCM ilikua inaongoza halmashauri zote, manispaa zote na majiji yote. Kwanini hamjawahi kuwaenzi mashujaa hawa?

Leo mnajifanya kuumizwa na Wanyama kupewa mtaa? Seriously?....
Kama uchungu huo ungekuwa wa kweli mngekuwa mshawapa mashujaa wetu kina Filbert Bayi, Marijani Rajabu etc majina ya mitaa ndani ya nchi hii mnayojiitia watawala.

Jiulize Meya wa Temeke (CCM) ameshindwa nini kuupa mtaa wowote kwenye manispaa yake jina la Samata au Bi.Kidude? Meya wa Mwanza (CCM) ameshindwa nini? Au mnataka vyote afanye Meya wa Ubungo?

SWALI: Wanyama kupewa mtaa ina maana yoyote kwetu kiuchumi na kidiplomasia?

JIBU: Hamjui hilo?...
Kiuchumi tutegemee ongezeko la watalii maana Tanzania imejitangaza.
Kumbuka wapo watu wengi mashuhuri wamekuja nchini kimyakimya.

Haikutusaidia sana kujitangaza. Lakini wanyama amekuja waziwazi na dunia inajua yupo kwetu. Ameshiriki social activities nyingi. So return yake si haba.

Pia Kidiplomasia tumeonesha kwa vitendo mtangamano wa jumuiya ya EAC. Kumbuka mwenyekiti wa EAC kwa sasa ni Rais JPM.

SWALI: Nini kifanyike??

JIBU: Kwanza, acheni uzwazwa!
Pili alichofanya Meya wa Ubungo kiwe chachu ya kuwaenzi mashujaa wetu wengine. Mameya wengine watoe mitaa yao waipe majina ya watanzania.

Kumlaumu mtu kufanya jambo ambalo hata wewe unaweza kufanya huo ni uzwazwa? Kama Bonny kampa mtaa Wanyama, mwambieni Meya wa Temeke (CCM) akamate fursa "chapchap" atangaze mtaa mmoja kuupa jina la Samata au Filbert Bayi au Bi.Kidude au "Bashite Zero Brain".
Acheni kulialia, chukueni hatua. Hata nyie mnaweza.

SWALI: Wanyama ni wingi wa mnyama?

JIBU: Hapana, Wanyama ni kifupi cha "TID Mnyamaaaa". Mazwazwa nyie.

Malisa GJ
Walioubadilisha mtaa huo akili zao finyu. Ndo maana namkubali Rais Trump kwamba Afrika itawaliwe tena.
 
Mbona mtaa wenu unaitwa nyati? Kuna wanaofanana na nyati hapa dar? Mbona hatulalamiki.....au wakati mnatunga haya majina mlikuwa mmemkunywa pombe. Nyie ccm sijui mna nini kwenye huo ubongo.
Kutawaliwa ni hasara sana maana unathamini cha mwengine na chako unakiponda. Laana kweli.
 
Ni Tanzania ambapo masuala ambayo hayana impact chanya katika maisha yao yanachukua nafasi kuu kwenye mijadala wakati masuala yenye kuwagusa kimaisha hayachukui nafasi.

Tanzania kuna vituko!
1. Bila shaka na watawala wanafurahia kuona hali kama hii! 2. Acha haya yachukue nafasi maana mengine ambayo pengine ndio yenye "impact chanya" hawana uhuru wa kuyadili!
 
Mimi ni CDM , Ila hilo la Wanyama napinga 100% . Hivi baada ya miaka 50 wajukuu wakikuuliza kwa nini mtaa unaitwa wanyama utawajibu nini cha kuwaridhisha? Leo mtoto wa uingereza akimuuliza babu yake kwa nini Mwl.Nyerere street anachakujibu. Kiongozi wa taifa, mpigania Uhuru nchi yake na nchi nyingine. Wanaopewa mitaa si lazima direct alifanya kitu kwenye nchi husika lakini anahistoria duniani ambayo kila MTU angelipenda kujua sasa na vizazi vijavyo. Kwa mfano ukiupa mtaa Pele , au Gaucho Dinho, kuna kitu unique ambacho MTU angelilenda kujua
 
Kama ilivyo kwa majina yote ya viongozi yanayotumika katika mitaa mbalimbali yasivyo na faida kwa wakazi wa mitaa husika,ndivyo ambavyo jina la Wanyama lisivyoweza kuwa na faida yoyote kwa huo mtaa.Tunaowatunza kwa kodi zetu huku majina yao tukiyatumia sehemu mbalimbali nchini,ndiyo walioingia mikataba inayozalisha takataka ziitwazo "makinikia" tunazozigombea leo,nini faida yao?
Utaratibu wa kuibadilisha mitaa majina kwa ajili ya watu utazamwe upya. Mitaa yote isiwe na majina ya watu hata kama ni kiongozi kisiasa.
 
Hakuna kitu wanachoniudhi Chadema pale unapowahoji wanajibu mbona na ccm wamefanya.......!
 
Ni Tanzania ambapo masuala ambayo hayana impact chanya katika maisha yao yanachukua nafasi kuu kwenye mijadala wakati masuala yenye kuwagusa kimaisha hayachukui nafasi.

Tanzania kuna vituko!

hah hah hah hah kuna mzee mmoja nusu nimzabe kibao leo...
eti anasema Tanzania ndio nchi pekee ambayo watakula Eid Jumatatu.

anasema eti Tanzania hata Mwezi ukionekana mkubwa kama Kalai, lakini wenyewe watasubiri eti mpaka Mufti awatangazie
 
Back
Top Bottom