Hofu ya Mwigulu Nchemba ni hofu ya CCM?

Hofu ya Mwigulu Nchemba ni hofu ya CCM?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,348
Reaction score
26,144
Katika mchango wake wa leo katika Bunge Maalum la Katiba,Mjumbe Mwigulu Nchemba ameonyesha hofu yake ya kuendelea na majadiliano kwa siku themanini na nne (84) na mwishowe kushindwa kupata theluthi mbili za Tanzania Bara na theluthi mbili za Tanzania Visiwani ili kupitisha Rasimu tayari kwa kupigiwa kura ya maoni na watanzania. Mwigulu Nchemba amemtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba afanye hesabu na kujiridhisha juu ya kupatikana kwa takwa hilo la Kikatiba.

Hii ni hofu kuu.Ni hofu isiyo na chembe ya shaka kuwa wapo Wajumbe wameshaona dalili za kulazimisha visivyolazimishwa. Hofu inayolenga kuponya fedha za walipakodi wa nchi hii ambazo zaweza kutafunwa kwa siku 84 bila ya kupelekewa Rasimu ya Katiba kuipigia kura. Ni hofu ya wengi. Wachambuzi wa kisiasa wanaiona kauli ya Mwigulu Nchemba kama kuanza kushtuka kwa CCM na kutaka kurejea 'kwenye njia sahihi' ya kupata Katiba mpya.

Kama Mwigulu Nchemba,kama Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara na Naibu Waziri wa Fedha ameshindwa hadi leo kujua kama wana theluthi mbili za pande mbili za Muungano,itoshe kuaminika kuwa CCM na wafuasi wao hawana uhakika wa kupitisha Rasimu iliyo Bunge Maalum la Katiba.Mwenyekiti Sitta anapaswa kuufanyia kazi ushauri wa Mwigulu Nchemba AS SOON AS POSSIBLE (ASAP). Binafsi naamini,takwa la theluthi mbili halitafikiwa kwa hali ilivyo sasa na hivyo Bunge Maalum la Katiba lapaswa kusitishwa hima.
 
Last edited by a moderator:
Mdogo wangu Petro,

Kuna maneno kwenye Biblia yanayosema "sema kweli daima na kwa kusema ukweli utakuwa huru". Naamini minyiroro iliyokuwa inamsumbua Mwigulu imemtesa sana,sasa anarudi kwenye mstari na kuanza kuiona kweli na kuisema kweli ili awe huru. Naaam,wito wake kwa wajumbe wa BMLK
utazamwe sasa na M/kiti wa Bunge Maalum,.M/kiti wa chama chake na pia chama chake na wanachama wenzake. Naamini maslahi ya taifa yakitangulizwa mbele basi wito wake utatamalaki

Wasalaam kutoka likizoni Bunda, Mara

Kilichonitia hofu zaidi ni kwamba wakati anaelezea hofu yake hiyo.wabunge wengine walikuwa kimya hawakumpigia makofi kama kawaida yao...kifupi aliongea kama mpinzani hivi..mwana UKAWA in disguise

Hakika Mkuu.Ukumbi ulikuwa kimya sana
 
Mdogo wangu Petro,

Kuna maneno kwenye Biblia yanayosema "sema kweli daima na kwa kusema ukweli utakuwa huru". Naamini minyiroro iliyokuwa inamsumbua Mwigulu imemtesa sana,sasa anarudi kwenye mstari na kuanza kuiona kweli na kuisema kweli ili awe huru. Naaam,wito wake kwa wajumbe wa BMLK
utazamwe sasa na M/kiti wa Bunge Maalum,.M/kiti wa chama chake na pia chama chake na wanachama wenzake. Naamini maslahi ya taifa yakitangulizwa mbele basi wito wake utatamalaki

Wasalaam kutoka likizoni Bunda, Mara

Kaka J.M.B.Mhozya,kweli itabaki kuwa kweli
 
Walaji hawajali.... Wanahonga meza kila sentensi inayotamkwa na kuishia na neno UKAWA!!!

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hakika Mkuu.Ukumbi ulikuwa kimya sana

Na hili linathobitisha zaidi na zaidi kwamba kilichowapeleka wengi pale ni hii fursa ya posho ya laki tatu kwa siku. Inahitaji mzalendo wa kweli kuikataaa hiii.....hapo kuna wanafunzi bodinya mikopo imeshindwa kuwalipia mafunzo wka vitendo hadi.muda huu....Mwigulu anatokea hazina anajua hali halisi ilivyo....
 
Ukweli ni kwamba CCM wanalazimisha mambo kwa kujidai kwamba hawawezi kujua kama theluthi itapatikana kwasababu kura ni ya wazi na siri. Lakini hii game UKAWA watashinda kwasababu kundi la 201 limeshapungua wajumbe 67 ambao wanatokea Zanzibar ambao wanawaunga mkono UKAWA, pia kuna jumla ya wabunge 72, idadi inayofanya jumla ya wajumbe 139 sasa hiyo theluthi inatokea wapi? pia ikumbukwe sheria ya mabadiriko ya katiba ibara ya 26 (2) inawataka wajumbe wa bunge maalum kupata theluthi mbiliya kura kutoka Zanzibar. Bara wataipata ingawa pia kuna wajumbe wa 201 wengine pia hawajatia mguu Dodoma mfano Maria Sarungi-Tshei ambaye alinitamkia pale Blue Pearl Hotel mara baada ya mdahalo kwamba hataenda bungeni. Labda wataalam watusaidie.
 
Kwa uhakika mimi ni mwana UKAWA lakini kwa uhakika napenda kumpongeza ndg Mwigulu Nchemba kwa msimamo na ushauri wake kwa Bunge maalum la Katiba.
Hajawa km kina Kigwangala wanaofwata Upepo.
Hongera sana Mwigulu.
 
Samwel Sitta ndiyo bure kabisa.
Bora mwigulu kwa siku mbili hzi ameonyesha kama amekomaa.
 
Viongozi wengi wa CCM wameshagundua kuwa hoja za chama chao hazikubaliki na wananchi zinazokubalika kwa wananchi na ambazo zinauzika kirahisi ni hoja za wapinzani.Kwa jinsi hiyo viongozi wengi wa CCM wamejigundulia kamtindo kakutoa hoja kama wapinzani ili waweze kukubalika kwa wananchi.
 
Kwa mara ya kwanza tangu nimjue Mwingulu Nchemba, nakubaliana naye kwa 100%. Mwingulu anaachana na siasa uchwara na kuwa realistic jinsi siku zinavyoenda !. Kwa week kama mbili hivi sasa amekuwa akiongea vitu ambavyo ni constructive kwenye suala la katiba...

Lakini ndugu yangu kwa CCM kwa ujumla wao hii ni too little too late.....Ki-ukweli CCM kwa ujumla wao ni wa-pu-mbavu kiasi kwamba hawawezi kuuona ukweli huu ulio dhahiri ! CCM kwa sasa hivi ni kama mtu asiyejua kuogelea halafu akaingia kwenye maji yenye kina kirefu !. Kule kutapatapa kwake ndio kunakomfanya azame....

Yaani CCM sasa hivi wanafanya decisions za kipuuzi na kila wanapojaribu kufanya decision ili kurekebisha upuuzi uliopita wanafanya decision ya kipuuzi zaidi na kutapatapa huku kutaendelea na ni kati ya vitu vitakavyowazamisha !

Its obvious hawana 2/3 ya wajumbe kutoka zanzibar lakini bado wanang'ang'ania kuendelea na mjadala !......hivi kuna ujuha kama huu !.

Lets say wamefanikiwa kuwanunua baadhi ya wajumbe wa CUF (very unlikely kwa sababu wanatikiwa 16) na kuipitisha rasimu hiyo kwenye bunge la katiba, hata hivyo mtu yeyote anayejua siasa za Zanzibar anajua for sure hakuna Chama kati ya CCM au CUF kinachoweza kupata 2/3 ya wananchi kwenye kura ya maoni bila kukubaliana na chama kingine !. Hivyo hata wakiipitisha hiyo rasimu kwa miujiza na kuipeleka kwa waTZ na ikifanikiwa kupitishwa na Watanganyika (ingawa nayo naona ni ngumu).....Haitaweza kabisa kupitishwa na wanzanzibari as long as CUF wanaipinga !

Sasa unawezaje kutumia mabilioni yote hayo wakati unajua kwa uhakika kabisa at the end of the day hiyo katiba mpya haitapatikana ?!

Ndio maana nasema CCM kwa ujumla wao ni wa-pu-mbavu.....Nasema hii kwa maana nzuri sio kuwakashifu bali ni ukweli kabisa. M-pumba-vu ni mtu asiyeelewa hata akielimishwa sana ! Sasa kama CCM wanashindwa kuelewa facts ambazo ziko wazi kiwango hiki kwa nini wasiitwe wa-pu-mba-vu ?

Katika mchango wake wa leo katika Bunge Maalum la Katiba,Mjumbe Mwigulu Nchemba ameonyesha hofu yake ya kuendelea na majadiliano kwa siku themanini na nne (84) na mwishowe kushindwa kupata theluthi mbili za Tanzania Bara na theluthi mbili za Tanzania Visiwani ili kupitisha Rasimu tayari kwa kupigiwa kura ya maoni na watanzania. Mwigulu Nchemba amemtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba afanye hesabu na kujiridhisha juu ya kupatikana kwa takwa hilo la Kikatiba.

Hii ni hofu kuu.Ni hofu isiyo na chembe ya shaka kuwa wapo Wajumbe wameshaona dalili za kulazimisha visivyolazimishwa. Hofu inayolenga kuponya fedha za walipakodi wa nchi hii ambazo zaweza kutafunwa kwa siku 84 bila ya kupelekewa Rasimu ya Katiba kuipigia kura. Ni hofu ya wengi. Wachambuzi wa kisiasa wanaiona kauli ya Mwigulu Nchemba kama kuanza kushtuka kwa CCM na kutaka kurejea 'kwenye njia sahihi' ya kupata Katiba mpya.

Kama Mwigulu Nchemba,kama Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara na Naibu Waziri wa Fedha ameshindwa hadi leo kujua kama wana theluthi mbili za pande mbili za Muungano,itoshe kuaminika kuwa CCM na wafuasi wao hawana uhakika wa kupitisha Rasimu iliyo Bunge Maalum la Katiba.Mwenyekiti Sitta anapaswa kuufanyia kazi ushauri wa Mwigulu Nchemba AS SOON AS POSSIBLE (ASAP). Binafsi naamini,takwa la theluthi mbili halitafikiwa kwa hali ilivyo sasa na hivyo Bunge Maalum la Katiba lapaswa kusitishwa hima.
 
Ili Mwigulu aweze kueleweka kwa wananchi ni vizuri angeenda mbali zaidi kwa kukataa kupokea lakitatutatu vinginevyo huruma zake kwa Taifa zitakuwa ni blabla tu.
 
Viongozi wengi wa CCM wameshagundua kuwa hoja za chama chao hazikubaliki na wananchi zinazokubalika kwa wananchi na ambazo zinauzika kirahisi ni hoja za wapinzani.Kwa jinsi hiyo viongozi wengi wa CCM wamejigundulia kamtindo kakutoa hoja kama wapinzani ili waweze kukubalika kwa wananchi.
si watachakachukua kwani kuna tume ya uchaguzi au
 
Hatuachi posho wengine itatusaidie kwenye uchaguzi next year

hilo ndio lengo kuu ukweli wa kukosa 2/3 wanaujua tangia UKAWA walipotoka bungeni ila Milioni 20 na ushee ni mtaji tosha wa kampeni mwakani kuchapishia t-shirt, kofia, kukodisha ma-fuso, muziki na kuandalia wali na nyama chezea mafisadi wewe
 
Hawa ni wabaka demokrasia. Watabadiridhha hata sheria kama wanavyobadirisha ksnuni ili kukidhi matakwa yao. Mwache Samwel atumike tu lakini atakuwa na makubwa ya kujibu mbele ya watanzania na Mungu wake. I support ukawa na wasithubutu kujitia unajisi huu...kiburi cha wa watawala.

Ujanja watakao ufanya nikubadirisha kanuni na wajadiri sura nyingine wakiacha hiyo sura 1 na 6 ambazo kimsingi ndo zimewapotezea muda bila hitimisho. Watarudia sura hizo mwishoni baada ya kura posho zote na kila mjumbe ' asepe' zake. Huu utakuwa ni utapeli wa kitaifa na wa kwanza kutokea ktk historia ya dunia.
 
katika mchango wake wa leo katika bunge maalum la katiba,mjumbe mwigulu nchemba ameonyesha hofu yake ya kuendelea na majadiliano kwa siku themanini na nne (84) na mwishowe kushindwa kupata theluthi mbili za tanzania bara na theluthi mbili za tanzania visiwani ili kupitisha rasimu tayari kwa kupigiwa kura ya maoni na watanzania. mwigulu nchemba amemtaka mwenyekiti wa bunge maalum la katiba afanye hesabu na kujiridhisha juu ya kupatikana kwa takwa hilo la kikatiba.

Hii ni hofu kuu.ni hofu isiyo na chembe ya shaka kuwa wapo wajumbe wameshaona dalili za kulazimisha visivyolazimishwa. Hofu inayolenga kuponya fedha za walipakodi wa nchi hii ambazo zaweza kutafunwa kwa siku 84 bila ya kupelekewa rasimu ya katiba kuipigia kura. Ni hofu ya wengi. Wachambuzi wa kisiasa wanaiona kauli ya mwigulu nchemba kama kuanza kushtuka kwa ccm na kutaka kurejea 'kwenye njia sahihi' ya kupata katiba mpya.

Kama mwigulu nchemba,kama naibu katibu mkuu wa ccm bara na naibu waziri wa fedha ameshindwa hadi leo kujua kama wana theluthi mbili za pande mbili za muungano,itoshe kuaminika kuwa ccm na wafuasi wao hawana uhakika wa kupitisha rasimu iliyo bunge maalum la katiba.mwenyekiti sitta anapaswa kuufanyia kazi ushauri wa mwigulu nchemba as soon as possible (asap). Binafsi naamini,takwa la theluthi mbili halitafikiwa kwa hali ilivyo sasa na hivyo bunge maalum la katiba lapaswa kusitishwa hima.

hizo bilioni 20 tukubali kupoteza. Ila faida tutakayopata ni anguko la ccm!.. Wakikosa theluthi mbili tu.... Mtaani hakuna atakayewapokea!
 
Back
Top Bottom