Hofu ya Mwigulu Nchemba ni hofu ya CCM?

Hofu ya Mwigulu Nchemba ni hofu ya CCM?

kwa mara ya kwanza namuona mwigulu akivaa koti la uzalendo hongera sana brother,sio siri siku zote nilikuwa na muona mwigulu wa chama cha mapinduzi kama kada halisi wa chama ambae kila wakati ni kutetea misimamo ya chama lkn kwa hili ni dalili njema kwa wanasiasa wetu kuweka maslahi ya nchi mbele kwani kujadili katiba ktk mazingira ya UKAWA kuwa nje ni hatari ya kupoteza kodi za watanzania bila sababu za msingi.hongera sana!
 
UKAWA ni tumaini la watanzania. Lkn alichokifanya Leticia kinapaswa kulaaniwa vikali kwa kumvua uanachama mara moja. Bado masaa 15 niandae maandamano kuja Kinondoni endapo sitasikia tamko la kumfukuza bibi huyu toka uongozi wa juu wa chadema.
 
Jamani mtanzania aliye na access za 'daftari la mahudhurio' ya hili BMLT atujuze idadi ya wanaohudhuria kwa kila siku.
Natumai si jinai kudondosha hizo takwimu humu jukaani.
Nawakilisha
 
kwa mara ya kwanza namuona mwigulu akivaa koti la uzalendo hongera sana brother,sio siri siku zote nilikuwa na muona mwigulu wa chama cha mapinduzi kama kada halisi wa chama ambae kila wakati ni kutetea misimamo ya chama lkn kwa hili ni dalili njema kwa wanasiasa wetu kuweka maslahi ya nchi mbele kwani kujadili katiba ktk mazingira ya UKAWA kuwa nje ni hatari ya kupoteza kodi za watanzania bila sababu za msingi.hongera sana!

Unafahamu Mwigulu nafasi aliyo nayo kwenye chama chake haitofautiani na nafqsi ya propaganda au mpiga debe. Lazima atetee hoja za chama chake hata kama hoja hizo hazina manufaa mapana kwa wananchi.Hizo ndio siasa zetu Afrika kote kuurembesha uongo ufanane na ukweli tofauti na wenzetu walioendelea ambako ukigundulika umewapotosha wanachama wa chama chako au hata wasio wanachama unaweza kupoteza nafasi uliyo nayo.Kwa nafasi aliyopewa ya unaibu waziri wa fedha ambayo naamini hadi sasa anaimudu vizuri lazima aongee ukweli mtupu bila propaganda kwani nafasi yake ni ya taifa zima tofauti na ya kisiasa. Lazima kama naibu waziri na kwa kutumia elimu yake nzuri na uzoefu kwenye masuala ya fedha awe na maono.Nami niungane nae kuwa na hofu aliyo nayo. Mawazo kuwa tuanze kwa kujua idadi ya wabunge waliobakia bunge la katiba haina mashiko zaidi kwa kuwa sio wote wataunga mkono mapendekezo mliokubaliana na kuyapisha haswa litakapofikia kupiga kura. Uelewe bara mnaweza pata hiyo theluthi mbili inayotakiwa kisheria ila mkaikosa visiwani.Hivyo hivyo ikakosekana visiwani kupitishwa na wananchi.Uelewe suala lolote linalohusu maslahi ya wazanzibari wote huungana pamoja bila kujali itikadi zao kisiasa.Hivyo wasiwasi wa Mwigulu una mashiko na kama nilivyoeleza kwenye michango yangu ya awali ni kuwa nategea raisi akirudi toka safari alisimamishe hili bunge hadi muafaka upatikane kwa wale waliosusia mchakato.
 
Umegusia jambo la msingi sana kwasababu wanataka kujadili mambo ambayo kwa kina yatashughulikiwa na Nchi Washirika siyo SMT. Wameambiwa mambo yote ambayo si ya Muungano yatajadiliwa wakati wa Mchakato wa Katiba ya Tanganyika lakini kwa tabia yao ya Kushupaa wanaona eti Tume imesahau na mengine haikuandika kwa kina!!! Aibu aibu aibu!
Sijui itakuwaje watakapojadili masuala yanayohusu Tanganyika tu na Yale yanayohusu Zanzibar. Je wajumbe wa Zanzibar na wa bara watapigia kura mambo hayo ya nchi washirika (Zanzibar kwa Yale ya Tanganyika na Tanganyika kwa Yale ya Zanzibar) yasiyowahusu?
 
Naukumbuka mwongozo wa Mwigulu Nchemba alioutoa bungeni alipokwenda kinyume na msimamo wa chama chake kwa kusema kuwa mchakato wa katiba usiendelee kwa sababu ni dhahiri kuwa hatutopata akidi ya theluthi mbili kutoka Zanzibar kwa hiyo the whole exercise will be null and void na ni kupoteza muda na fedha za umma. Namkumbuka sana hii leo. Nashangaa hawa wengine wanajisikiaje sasa wanapoona utabiri wa Mwigulu, kada maarufu wa CCM, alipoweza kuuona huu mwelekeo na akausema ukweli wa imani yake pasi kumumunya maneno na bila unafik, lakini wengine wakaendekeza unafik na njaa zao.
Tujitathmni kama Watanzania
 
Asituletee mambo yake katiba imekamilika halafu mnaleta mambo yenu.
 
Back
Top Bottom