Hofu ya Kenya katika akili za Tanzania

Leo nimekuta umeniquote mara nyingi umeamka kwa mzuka, are you using words simply because you came across them or you're just trying to remain relevant. How am I on denial, corona is a scientific problem and every nation is dealing with it scientifically, you're the only country in the world that has chosen the path of apathy, completely doing nothing and expending too much energy crying wolf when anyone calls you out.
Wewe tu endelea kujiongelesha ongelesha. Leo Laizer kaongeza bilion 4.8 kwenye akaunti
 
Wewe tu endelea kujiongelesha ongelesha. Leo Laizer kaongeza bilion 4.8 kwenye akaunti
Kumbe tulikuwa tunapigwa aise, seems madini yaliyokuwa yanaibiwa ni mengi sana, ndio maana hawa 🐒 wanamchukia Magu.
 
Mk254, wewe ni mmoja wa wakenya wachache wanaojitahidi kujenga hoja angalau zenye mashiko,humu JF,kwa hili,umeandika upuuzi kabisa,mtoa post,amejikita kwenye hoja ya power struggle btn these two powers,TZ n Kenya,ningetegemea na wewe ujikite kutoa challenge zako Kama alivyofanya.umejikita kwenye stupid propaganda za Corona na kupost ramani kulingana na UAE tu na kusema ni dunia nzima.Corona haipo Tz hata nyinyi mnajua hilo.ni hivi,kila nchi Ina njia zake kupambana na tatizo kulingana na mazingira,hata Sweden,hakuenda curfew,Wala lockdown,walitumia njia Kama ya Tz,Ila huwezi kusikia majirani zake wakipiga kelele Kama mnavofanya.najua hii article imemaliza battle iliyomo humu muda mrefu,ndio maana hamna Cha kuipinga!
Nadhani wengi wamemshangaa hakuna aliyetegemea hicho alichoandika.
 
Hizi nguvu mnatumia kuficha udhaifu wenu kwenye suala la corona na kulilia Wakenya, mngezitumia kwa kuhakikisha mnapima na na kutolea taarifa za hali yenu hamngejikuta kwenye hali hii ya kukataliwa na dunia, mtaandika hizi insha mpaka mjaze vitabu vya dunia ila hali ni ile ile, corona ni tatizo la kisayansi na linapaswa kushughulkiwa kisayansi sio kwa matamko ya wanasiasa.

Leo hii Mtanzania ukionyesha paspoti ya Tanzania kwenye uwanja wowote wa ndege jamaa wote ghafla wanavaa barakoa na kujilinda na kukupitishia kwenye ukaguzi wa hali ya juu, hii ramani inaonyesha mlivyotiwa alama nyekundu na kanuni za kuwakagua mara mbili mbili.

Yaani mtelekeze jitihada dhidi ya corona kwa jinsi mlivyojichokea kisha muanze kulazimisha na kung'ang'ania kuingia ndani ya mataifa ya watu.

Kwetu huku njooni tumewaruhusu mje maana mumelia sana ila lazima kila anayefika na paspoti ya Tanzania apanue mdomo hadi jino la mwisho lionekane kisha kifaa cha kupima corona kitumbukizwe humo, ukipita huo mtihani wa kupimwa walau mara mbili kisha utfuatiliwa siku 14, utolee taarifa wapi unakwenda na utaishi kivipi, zikiisha hizo 14 basi hapo unaruhusiwa kujiachia huru na kufurahia maziwa na asali ya Kenya.

Health Alert: U.S. Embassy Dar es Salaam | U.S. Embassy in Tanzania

2473175_20200801_164531.jpg
WHO ilitangaza march toka kwamba afrika tutaanza kuokota miili ya wapendwa wetu mitaani na majumbani, mpaka sasa ni zaidi ya miezi mitano hapa Tanzania kwa macho yangu sijaona wala kufiwa na ndugu, jirani ama rafiki kwa corona, hata kumwona mpita njia kafa bado sijaona. Na hapa nyumbani Tanzania kwa sasa sioni watu wakinawa mikono wala kuvaa barakoa.

Pia hata baadhi ya Watanzania wenzangu watadhirisha hali ya hapa nyumbani ni salama na shwari kabisa.

Huu ugonjwa ni vita dhidi ya uchumi, iko wakati ukifika muda utathibitisha hilo.
 
Wapumbavu hawa mpaka leo corona bado inawapakata vyuo mnafufungua mwakani wakati wenzetu Tanzania wanakula tu mapindi.
 
Wapumbavu hawa mpaka leo corona bado inawapakata vyuo mnafufungua mwakani wakati wenzetu tz wanakula tu mapindi
Hapa Tanzania kila kitu kinaendelea kama kawaida,shule zote zimefunguliwa,unajua siku hizi ni ulimwengu wa digital kama kungekuwa na lolote habari zingeshafika mitandaoni,najua wakenya wanabisha ubishi tu ila hali halisi wanaijua kwamba mengi ni maigizo ya serikali yao.
 
Hizi nguvu mnatumia kuficha udhaifu wenu kwenye suala la corona na kulilia Wakenya, mngezitumia kwa kuhakikisha mnapima na na kutolea taarifa za hali yenu hamngejikuta kwenye hali hii ya kukataliwa na dunia, mtaandika hizi insha mpaka mjaze vitabu vya dunia ila hali ni ile ile, corona ni tatizo la kisayansi na linapaswa kushughulkiwa kisayansi sio kwa matamko ya wanasiasa.

Leo hii Mtanzania ukionyesha paspoti ya Tanzania kwenye uwanja wowote wa ndege jamaa wote ghafla wanavaa barakoa na kujilinda na kukupitishia kwenye ukaguzi wa hali ya juu, hii ramani inaonyesha mlivyotiwa alama nyekundu na kanuni za kuwakagua mara mbili mbili.
Yaani mtelekeze jitihada dhidi ya corona kwa jinsi mlivyojichokea kisha muanze kulazimisha na kung'ang'ania kuingia ndani ya mataifa ya watu.

Kwetu huku njooni tumewaruhusu mje maana mumelia sana ila lazima kila anayefika na paspoti ya Tanzania apanue mdomo hadi jino la mwisho lionekane kisha kifaa cha kupima corona kitumbukizwe humo, ukipita huo mtihani wa kupimwa walau mara mbili kisha utfuatiliwa siku 14, utolee taarifa wapi unakwenda na utaishi kivipi, zikiisha hizo 14 basi hapo unaruhusiwa kujiachia huru na kufurahia maziwa na asali ya Kenya.

Health Alert: U.S. Embassy Dar es Salaam | U.S. Embassy in Tanzania

2473175_20200801_164531.jpg
Mgonjwa akiugua ataenda hospitali na nzuri zaidi hospitali hakuna wagonjwa wa corona. Takwimu zipi zinafichwa. Acha kuwa mtumwa wa Mabeberu wewe
 
Mpaka Sasa kupima na kutoa taarifa imewasaidiaje kuamaliza Corona?alafu wewe una ubongo mdogo Sana,nimekwmbia hivi,kila nchi Ina njia zake za kupambana na tatizo, nyinyi mme opt kupima na kutangaza bila kuchukua hatua ya kupunguza maambukizi,usilazimishe tufuate huo utaratibu wenu,Sisi sio kila Jambo lazima sayansi itumike bali akili,hiyo kupima na kutangaza ndio sayansi ya kumaliza maambukizi,au?alafu mtoa post,amejikita kwenye uchumi na kuliko Corona wewe una divert mada.hakuna mtz anayetaka kuingia kwenye mataifa mengine,kwa nguvu,Kama unaweza yataje hapa, Sisi tumepiga marafuku hivyo vindege vyenu,mna'nga'ngania kuja TZ eti mnataka mazungumzo,sisi,hatutaki mtuletee Corona huku.

Wacha kuwa mjinga tumia ubongo kufikiria, hakuna mtu anayeweza kupona corona kwa kupima tu, fahamu corona kama ilivyo UKIMWI, watu hupima ili kujua hali yao na kuchukua hatua za kujilinda na kulinda wanaowapenda, imebainika corona inaua sana au kuwatesa sana watu wenye magonjwa mengine kama kisukari, hivyo ukijua hali yako mapema unamlinda mwenzako mwenye hali nyinginezo.

Dunia yote kila nchi inapima na kutoa taarifa, labda mataifa machache tu kama yenu hiyo iliyojichokea mapema na kutelekeza wanaanchi kila mmoja ahangaike kivyake, hata mataifa sugu wa kuficha data kama Korea Kaskazini kwa hili la corona wamekubali kufuata mbinu za kisayansi, hawajajiingiza kama nyie kwenye kuamini pumba za wanasiasa badala ya kutumia ubongo.
 
WHO ilitangaza march toka kwamba afrika tutaanza kuokota miili ya wapendwa wetu mitaani na majumbani,mpaka sasa ni zaidi ya miezi mitano hapa Tanzania kwa macho yangu sijaona wala kufiwa na ndugu,jirani ama rafiki kwa corona,hata kumwona mpita njia kafa bado sijaona.Na hapa nyumbani Tanzania kwa sasa sioni watu wakinawa mikono wala kuvaa barakoa.

Pia hata baadhi ya watanzania wenzangu watadhirisha hali ya hapa nyumbani ni salama na shwari kabisa.
Huu ugonjwa ni vita dhidi ya uchumi,iko wakati ukifika muda utathibitisha hilo.

WHO walitangaza kwa kuzingatia vigezo vya kisayansi na walikua sahihi, ni ile tu corona haijawa balaa kwa Waafrika maana hata sisi ambao hatujajichokea kama nyie, ambapo tunapima na kusoma takwimu hatujafa sana kihivyo, na sio kwamba kuna lolote la maana tumelifanya Afrika, ni ile tu kimiujiza fulani hivi tumeponea kufa.

Japo pia inasemekana mataifa ambayo watu wake huchanjwa sana dhidi ya maradhi kama homa ya njano wanaonekana kuwa na kinga dhidi ya corona.

Ukweli ni kwamba tuna bahati sana Afrika, na hamna lolote kubwa ambalo yeyote anaweza akajisifia kwamba kafanya dhidi ya corona, ingekua ya kutuua aisei nyie hapo na Burundi mngepukutika hadi balaa maana mlitangulia kujichokea mapema kisa umaskini.
 
WHO walitangaza kwa kuzingatia vigezo vya kisayansi na walikua sahihi, ni ile tu corona haijawa balaa kwa Waafrika maana hata sisi ambao hatujajichokea kama nyie, ambapo tunapima na kusoma takwimu hatujafa sana kihivyo, na sio kwamba kuna lolote la maana tumelifanya Afrika, ni ile tu kimiujiza fulani hivi tumeponea kufa.

Japo pia inasemekana mataifa ambayo watu wake huchanjwa sana dhidi ya maradhi kama homa ya njano wanaonekana kuwa na kinga dhidi ya corona.

Ukweli ni kwamba tuna bahati sana Afrika, na hamna lolote kubwa ambalo yeyote anaweza akajisifia kwamba kafanya dhidi ya corona, ingekua ya kutuua aisei nyie hapo na Burundi mngepukutika hadi balaa maana mlitangulia kujichokea mapema kisa umaskini.
Mkuu kwa nini mnatunyooshea vidole, kama sisi tungetangulia ni nini ambacho kingewaacha nyie salama? Hio curfew yenu?

Mkuu tambua ili uweze pambana na maradhi lazima upate mlo bora,kama jibu ni "ndio" umesahau kama kenya mna janga la njaa, nimeona mpaka wanajeshi wenu walikamatwa na camera wanaiba mikate, mligawa chakula cha bure mkaumizana mpaka mkataka na kuuana, je umesahau sisi ndio tunawalisha?kama corona ingeanza na sisi nyinyi ingewachapa mara mbili. So endelea kutuombea mabaya.
 
Just a quick reminder, $100b > $63b
Halafu ajabu kuu huyo mwenye $ 100b watu wake wana njaa kwa kukosa mlo wa siku na ili washibe wanawategemea hao wenye $ 63b watu wake wanashiba.

Kumbuka kuwa mwenye chakula ndiye anayemtawala mwenye njaa. Inakuwaje una $100b huwezi kujilisha na mwenye $ 63b anajilisha na anakulisha hata wewe?

Vv
 
Mkuu kwa nini mnatunyooshea vidole, kama sisi tungetangulia ni nini ambacho kingewaacha nyie salama?hio curfew yenu? Mkuu tambua ili uweze pambana na maradhi lazima upate mlo bora, kama jibu ni "ndio" umesahau kama kenya mna janga la njaa, nimeona mpaka wanajeshi wenu walikamatwa na camera wanaiba mikate, mligawa chakula cha bure mkaumizana mpaka mkataka na kuuana, je umesahau sisi ndio tunawalisha?kama corona ingeanza na sisi nyinyi ingewachapa mara mbili. So endelea kutuombea mabaya.

Nilitegemea utakua na uwezo wa kujadili hoja kwa kutumia ubongo, hivi ina maana Tanzania yote hakuna mwenye akili ya kuweza kujadili hili janga la corona, nyote mko hovyoo kiasi hiki.

Kila anayeniquote nafungua nikitazamia nitakuta nondo tujadili nakuta ni mipasho utadhani yuko kwenye vigodoro Tandale. Mpaka sasa hata nimejikuta napuuza sifungui comments ambazo niko quoted maana nyote mumekua level moja.
 
Chakula kwa wenye akili.

Credit: Na Abbas Mwalimu

Jumapili, 2 Agosti, 2020.

Alhamisi tarehe 30 Julai, 2020 Serikari ya Kenya kupitia Wizara ya Uchukuzi ilitangaza kanuni mpya kwa wasafiri kutoka mataifa ya kigeni.

Katika hatua hiyo, mataifa 11 yalitangazwa kuruhusiwa kuingia nchini humo kuanzia Agosti Mosi, 2020 baada mlipuko wa Covid-19 uliosababisha safari nyingi za ndege duniani kusitishwa.

Waziri wa Uchukuzi wa Kenya, James Machira alizitaja nchi hizo kuwa ni Uganda, Rwanda, China, Korea Kusini, Japan, Canada, Ethiopia, Uswisi, Namibia, Morocco na Zimbabwe.

Idadi hiyo ilitangazwa kuongezwa mnamo tarehe 31 Julai, 2020 na kufikia mataifa 19 baada ya kuongezeka nchi za Marekani (Isipokuwa kwa majimbo ya California, Florida na Texas), Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Qatar, Umoja wa Falme za Kiarabu na Italia.

Kufuatia kanuni hizo zilizotolewa na Wizara ya Uchukuzi ya Kenya, kwa upande wake Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imefuta kibali kilichokuwa kikiruhusu Shirika la Ndege la Kenya (KQ) kutua nchini.

Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania bwana Hamza Johari Jumamosi tarehe 31 Julai, 2020 kwenda kwa Meneja wa Operesheni za Uhandisi Ukuraji wa Shirika la Ndege la Kenya imeeleza kuwa Tanzania imeiarifu Kenya Airways juu ya hatua hiyo ya kufuta safari zote za KQ kwenda Dar es Salaam, Kilimanjaro na Zanzibar kuanzia tarehe Mosi Agosti, 2020 mpaka pale watakapojulishwa tena kama sehemu ya utaratibu wa kurejesha lililofanywa na mwingine (on a reciprocal basis).

Huu ni muendelezo wa vitendo vya nchi ya Kenya dhidi ya Tanzania mara kwa mara hali inayoonesha kuna jambo huenda limejificha nyuma ya tabia hizi za Kenya.

Hatua ya uamuzi huu wa sasa wa kuifutia KQ kibali ni wazi kuwa utaliyumbisha shirika hilo. Kwa nini?

Kwa sababu mwezi Machi, 2015 Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ilipunguza safari za shirika hilo Tanzania kutoka 42 kwa wiki hadi 14 na kumlazimu Rais Uhuru Kenyatta kuomba mzungumzo na Rais wa wakati huo Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ili kulinusuru shirika hilo.

Ikumbukwe kuwa mwezi Mei, 2020 Rais Uhuru Kenyatta alitangaza kufunga mipaka ya nchi hiyo dhidi ya nchi za Tanzania na Somalia kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kujikinga dhidi ya kusambaa kwa virusi vya Corona.

Hatua hiyo ilipelekea wakuu wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga kuzuia malori yanayoingia kutoka nchini Kenya na hatimaye Kenya kupitia Balozi wake nchini, Mheshimiwa Dan Kazungu kuomba muafaka.

Baadae Rais Uhuru Kenyatta alimpigia simu Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na kumuomba pande hizo mbili zikae katika meza ya majadiliano baada ya kuona raia wake wanaathirika kwa kukosa huduma za msingi hasa vyakula na mbogamboga kutoka Tanzania.

Historia ya vitendo vya Kenya dhidi ya Tanzania ilianza miaka mingi sana, tukumbuke hata mwaka 2010 Kenya iliwahi kuikatalia Tanzania kuuza pembe za ndovu zenye thamani ya dola za Marekani milioni 20 katika mkutano wa Nchi wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Hifadhi ya Mimea na Wanyama walio katika hatari ya kutoweka duniani uliofanyika Doha, Qatar licha ya Afrika Kusini na Zambia kuiunga mkono Tanzania.

Katika miaka ya hivi karibuni pia mwezi Aprili mwaka 2017 Kenya ilipiga marufuku uingizwaji wa ngano na gesi ya kupikia kutoka Tanzania na hivyo Tanzania nayo kuchukua hatua ya kuzuia maziwa ya ng'ombe na sigara kuingia nchini kutoka Kenya.

Baada ya kuona hali inaenda vibaya Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta alifanya mazungumzo na Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na hatimaye makubaliano kufikiwa tarehe 24 Julai, 2017.

JE, NI NINI KINAPELEKEA KENYA KUWA NA TABIA HIZI DHIDI YA TANZANIA?
Kabla sijaeleza sababu za Kenya kufanya kile inachofanya mara kwa mara na namna Tanzania inavyojibu mapigo, kuna haja ya kufahamu kanuni zinazongoza Uhusiano wa Kimataifa.

Kwa mujibu wa Goldstein (2008) Uhusiano wa Kimataifa unaongozwa kwa kanuni kubwa tatu ambazo ni:
(i) Dominance
(ii) Reciprocity
(iii) Identity

Hapa nitazungumzia kanuni mbili za kwanza. Kenya inaamini kuwa yenyewe ina nguvu katika Afrika Mashariki hivyo inajaribu kuonesha namna inavyoweza kutawala (Dominance) nchi nyingine za Afrika Mashariki. Nitaeleza baadae namna Kenya inavyojiona.

Tanzania kwa upande wake inatumia zaidi kanuni ya pili pale inapofanyiwa vitendo visivyo stahiki na nchi ya Kenya yaani kurejesha kile ilichofanyiwa (reciprocity). Hii kwa namna fulani inalenga kuionesha Kenya kuwa si dola lenye nguvu kama wanavyojiita kwani kila mara Tanzania inapochukua hatua hii Kenya huomba kukaa kwenye meza ya makubaliano kuondoa tofauti. Lipi ni dola lenye nguvu?

Kanuni hizi mbili zinauelezea uhusiano wa kimataifa kama mfumo wa makabiliano au ushindani (Confrontational or Competitive) zaidi.

Rochester (2010: 2018) katika kitabu chake "Fundamental Principles of International Relations" alijaribu kuondoa dhana hii ya makabiliano au ushindani kwa kujenga uwiano baina ya maslahi kinzani na yale ya pamoja kwa kutazama hali ya kutegemeana kwa nchi (Interdependence).

Baada ya kufahamu hayo sasa ni vema tukajifunza sababu za Kenya kufanya vitendo hivi mara kwa mara.

Kuna mambo matatu ambayo yanasababisha Kenya kufanya hivi, mambo haya ni:

(i) Survival of the State (Kuishi kwa Dola)
(ii)I ncrease in interdependency (Kuongezeka kwa kutegemeana)
(iii) Hegemony (Ukuu wa Dola).

SURVIVAL OF THE STATE (Kuishi kwa Dola)
Mambo haya yote matatu yanatazamwa katika maslahi ya taifa likiwemo hili la survival. Je maslahi ya taifa ni nini?

Hans Morgenthau (1948; 1950; 1952) alitafsiri maslahi ya taifa kwa kusema:

"The meaning of national interest is survival power."

Brookings Institution wao walitafsiri maslahi ya taifa kwa kueleza ifuatavyo:

"What a nation feels to be necessary to its security and well being…National interest reflects the general and continuing ends for which a nation acts."

Kwa tafsiri yangu, "Kile ambacho taifa inahisi kuwa ni muhimu kwa usalama na kuwa njema kwake...maslahi ya taifa yanaakisi malengo ya jumla na endelevu yanayoendewa na taifa."

Malengo haya huwa ya kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa. Hivyo hili la vitendo vya Kenya moja kwa moja linajikita katika malengo ya kiuchumi.

Ni wazi kuwa Kenya ina hofu kubwa ya kumalizika kwa nafasi yao ya kiuchumi dhidi ya Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki hasa baada ya kuona uwekezaji mkubwa unaofanywa katika nchi ya Tanzania.

Tufahamu kinachofanyika nchini Tanzania kinaenda kuipa Tanzania nafasi kubwa ya kuvutia wawekezaji, hii ndiyo sababu Tanzania imezipiku nchi nyingi za EAC na SADC katika uuzaji wa bidhaa nje.

Ukitazama changamoto zote ambazo zimeainishwa na Benki ya Dunia katika "Urahisi wa Kufanya Biashara" yaani 'Easy of Doing Business' kwa kiasi kikubwa vinafanyiwa kazi, kwa mfano ujenzi wa miundombinu wezeshi ya kiuchumi na kibiashara kama vile ujenzi wa barabara, madaraja, ununuzi wa ndege, ununuzi na ujenzi wa meli, upanuzi wa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, Kigoma na Katavi na kuanzishwa kwa Blue Print ambayo inalenga kuondo changamoto zote za uwekezaji na biashara kunaipa nafasi kubwa Tanzania dhidi ya Kenya.

Ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere katika mto Rufiji lenye kuzalisha megawatts 2115 pindi likikamilika kunatoa tafsiri ya moja kwa moja ya kushuka kwa bei ya umeme viwandani hali itakayochochea wawekezaji wengi kutokana na viwanda kupunguza gharama ya uzalishaji hivyo kuwa na uwezo wa kushindana katika soko la jumuiya za kikanda na duniani kwa ujumla.

Tunadhani Kenya watafurahia haya?

Tukumbuke Kenya wamejenga reli ya kisasa (SGR) lakini treni zake zinatumia dizeli wakati Tanzania kwa upande wake treni yake inatumia umeme na ina kasi zaidi ya ile ya Kenya, hili tunadhani haliwaumi? Tukumbuke treni hii inatarajiwa kwenda hadi Rwanda hapo baadae. Tunadhani Kenya watafurahia?

Ni lazima waumie kwa sababu Kenya inategemea umeme kutoka Uganda kwa ajili ya uchumi wake wakati Tanzania ina uwezo wa kuuza umeme wake nchi jirani. Hili ni dogo?

Sote tunakumbuka namna Kenya ilivyopigwa mweleka katika mchakato wa bomba la mafuta ambalo Tanzania ilifanikiwa kuingia mkataba na Uganda kusafirisha mafuta kutoka Hoima mpaka Chongoleani, Tanga. Hili linawauma Kenya mpaka kesho.

Mbali na hayo Tanzania inaendelea na mchakato wa kulifungua eneo la Magharibi hasa bandari ya Kigoma katika Ziwa Tanganyika na Katavi ambazo moja kwa moja zitapanua wigo wa biashara baina ya Tanzania Burundi na DRC. Bado Kenya watakuwa na amani juu ya survival yao?

Kwa ujumla ujenzi huu wa miundombinu ya kiuchumi unatishia survival ya uchumi wa Kenya ndiyo maana Kenya wanajaribu kutumia kila hila kuivuruga Tanzania ama kwa haya inayofanya au kupitia washirika wake, kwa mfano, tumekuwa tukiona mara kwa mara ubalozi wa Marekani nchini Tanzania ukiingia matatani kwa kutoa taarifa ambazo haina uthibitisho wake kama vile ulivyowahi kutoa taarifa ya kile walichoeleza kuwa ni tishio la ugaidi Masaki na pia kuitaka Tanzania itoe taarifa za Covid-19 mpaka kupeleka aliyekuwa Kaimu Balozi Imni Patterson kuitwa mara kwa mara Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kujieleza. Hivi Tanzania ina tishio la kushambuliwa na magaidi kukiko Kenya?

Tunajua kwa nini wanafanya hivi? Lengo la propaganda hii ni kuonesha kuwa Tanzania si mahala salama kwa uwekezaji hasa tukizingatia nchi ambayo Marekani imejielekeza kuwekeza yaani Kenya inapata hofu kubwa kutokana na uwekezaji unaofanyika Tanzania. Hii ndiyo sababu hasa ya Kenya kuingia mkataba wa kibiashara na Marekani ambao utaipa nafasi Marekani kuuza bidhaa zake katika soko la EAC, lengo hapa ni kuidhoofisha Tanzania kwa Marekani kuifanya Afrika Mashariki eneo la kuuza bidhaa kwa bei ya chee (Dumping). Hatujilizi kwa nini Kenya iliamua kuwalipa fidia raia wake ili Marekani ijenge base ya kijeshi pamoja na kuwapa eneo la bahari kwa ajili hiyo? Hatujiulizi?

Hatushangai Kenya ilifanya lockdown ikiwa na wagonjwa 7 lakini inakuja kuondoa lockdown ikiwa na wagonjwa elfu 7 na hapo hapo Balozi wa Marekani nchini Kenya anajigeuza bosi wa bodi ya utalii ya Kenya na kusema kuwa Kenya ni mahala salama kutalii na kusisitiza "...There is no better place to travel other than Kenya..." Kweli hatushangai?

Kama Mkataba wa Vienna wa mwaka 1961 unaohusu Mahusiano ya Kidiplomasia unaeleza kuwa Mabalozi huwawakilisha wale waliowateua ndani ya nchi zilizowapokea (soma ibara ya 3) je Balozi Kyle McCarter aliteuliwa na Rais wa Kenya?

KUONGEZEKA KWA KUTEGEMEANA (INCREASE IN INTERDEPENDENCE)
Tanzania kutangazwa kuwa nchi ya uchumi wa kipato cha kati na Benki ya Dunia Julai Mosi, 2020 kunaongeza kiwango cha kutegemeana (interdependency) kati yake na Kenya na hali inayozidisha changamoto kubwa kwa Kenya.

Haya yalibainishwa na Hanggi na wenzake (2006:27) walipoeleza:

"Confrontation or cooperation in interregional relations depends on the degree of economic interdependence and the degree of institutionalization of interregional cooperation."

Kwa bahati nzuri kwa Tanzania, ni kwamba Kenya inaitegemea Tanzania katika vitu ambavyo kama Kenya wasipovipata uchumi wao na maisha ya kawaida ya Wakenya yanaathirika kwa kiasi kikubwa.

Tanzania ni soko kubwa la bidhaa za Kenya na Tanzania ni msambaji mkubwa wa mahitaji muhimu kama chakula kwa Kenya. Haya yalibainishwa na Dkt. Duncan Onjwang alipofanya mahojiano na kituo cha luninga cha KTN katika mada iliyopewa jina, "Genesis of the tiff between Kenya and Tanzania." Wakenya wengi walichukia alichosema Dkt. Onjwang kwamba katika msuguano baina ya nchi hizi mbili, "...Kenya will suffer more..."

Ndiyo maana Hanggi na wenzake (2006:27) walisisitiza:

"The degree of interdependence can have some impact on the way in which trade disputes are resolved..." Sijui kama Kenya wanaliona hili, hasa pale wanapoanza na Tanzania kumalizia na hatimaye kujikuta wanaomba meza ya majadiliano na Tanzania.

HEGEMONY (UKIRANJA DHIDI YA MATAIFA MENGINE)
Kuna dhana ambayo imeenea vichwani mwa Wakenya wengi na hasa wasomi, wao wanaamini kuwa Kenya ni Dola Kiranja au Nchi Kiongozi (Hegemonic State) katika Afrika Mashariki.

Ukimsikiliza Dkt. Duncan Onjwang katika mahojiano na KTN katika "The Genesis of tiff betwen Kenya and Tanzania" utagundua hili la kujiona ni dola kiranja kama nilivyogusia awali, Dkt. Onjwang anasema, "We are the leaders in this region..." Kwamba Kenya ndiyo dola kiranja katika ukanda huu. Si ajabu kumuona Mkenya akiandika mitandaoni, "We are the super power of East Africa." Huu ndiyo mtazamo na mawazo yao.

Kuthibitisha hili, Mkenya Lee Mwiti Mugambi mwaka 2015 alifanya utafiti wake uliojikita katika kuitazama Kenya kama Dola Kiranja (Hegemony) ndani ya Afrika Mashariki. Utafiti wake ulikwenda kwa jina la "Hegemony and Regional Stability in Africa: A critical analysis of Kenya, Nigeria and South Africa as Regional Hegemons."

Katika utafiti huo Mugambi anasema na hapa ninamnukuu:

"In regard to Eastern Africa, it's sufficient to recognize the role of Kenya as another major power. It's an economic powerhouses in the region and over the years, Nairobi has become the multinational capital of the region." Mwisho wa kunukuu.

Kwa tafsiri yangu Mugambi anamaanisha kwamba "Kenya ndiyo nchi kubwa Afrika Mashariki,kwamba ina uchumi mkubwa katika eneo la ukanda huu na Nairobi ndiyo kitovu cha mitaji mikubwa ya kikanda."

Mugambi anawakilisha mtazamo wa wakenya wengi namna wanavyoitazama nchi yao dhidi ya Tanzania.

Lakini ukweli wa hili upoje?

Tuitazame nadharia ya hegemony ili kuona kama hiki wanachojiona nacho wakenya ni kweli au lah!?

Nadharia hii inayotokana na mwananadharia wa kiitaliano Antonio Gramsci na kuja kutoholewa baadae inaeleza kama ifuatavyo:

Hegemonic Stability Theory: "International system is likely to be stable if a single nation-state is dominant or outright hegemon. Conversely, the absence of such a state would be associated with disorders."

Kwamba: "Mfumo wa Kimataifa unaweza kuwa imara ikiwa nchi moja itatawala nyingine au kuwa kiranja kwa wengine. Kinyume chake, kutowepo kwake kutasababisha kutokuwepo kwa utulivu."

Brown nae aliongezea, "Hegemon is a state that has the capacity to set rules of action and by extension enforce them, the state also needs to have the alacrity to act on this ability."

Hivyo basi, wakenya wanaamini kuwa mustakabali wa uchumi wa Afrika Mashariki unaitegemea Kenya kinyume chake hakuwezi kuwa na utulivu. Kwamba Kenya inaweza kuweka kanuni na kulazimisha wengine wafuate hizo kanuni kama vile walivyofanya lockdown n.k na wanajaribu kuonesha utayari wao katika hili.

Mugambi ametazama uchumi wa Kenya na pia kulinganisha jeshi la nchi hiyo na nchi kama Ethiopia na kutoa majibu ya jumla kama walivyo wakenya wengi pasina kujua kuwa takwimu za majeshi nyingi haziwezi kuwekea wazi kwa sababu za kiusalama.

Wanachoshindwa kutambua wasomi wengi wa kikenya ni kuwa nchi kuwa hegemon kuna vigezo vingi sana ambavyo tukitazama vyote havithibiti kwa Kenya.

Aneek (2010:59-63) na Schenoni (2017) wameainisha sababu nane za nguvu ya taifa aliposema: The national power of a State is the product of a number of elements. These are; (i) Geography (ii) Population (iii) Natural Resources (iv) Popular Support (v) National Character (vi) Technology and military strength (vii) Ideology (viii) Leadership

Hivi kweli kabisa Kenya inaweza ikasema ipo eneo zuri la kimkakati kijiografia kuizidi Tanzania ambayo imezungukwa na nchi 8 zinazoitegemea moja kwa moja ikiwemo Kenya yenyewe? Kweli Kenya inaweza kusema ipo eneo zuri kwa kuwa kwake karibu na Somalia?

Tanzania ni ncho ya tatu kwa idadi ya watu katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi Kusini mwa Afrika (SADC) nyuma ya DRC na Afrika ya Kusini na kwa hivi sasa Afrika Kusini inaweza kuwa imeachwa. Katika EAC ni ya kwanza, hili nalo Kenya hawalipimi?

Kenya ina rasilimali gani nyingine ukiacha mbuga ya Masai Mara ambayo nayo kwa kiasi kikubwa nyumbu wanaofuatwa kutazamwa na watalii hukaa Tanzania miezi 9 na kumalizia miezi mitatu Kenya? Kipi kingine wanacho?

Walitumia propaganda nyingi kuutambulisha Mlima Kilimanjaro kuwa upo Kenya mpaka kuandika "Visit Kenya and see mount Kilimanjaro" yote ikiwa katika kuwavutia wataliii ambao walikuwa wakitua JKIA na kisha kuwavusha kuja Tanzania wakiwa tayari wameshalala kwenye hoteli za Kenya. Baada ya Tanzania kununua ndege pumzi zimewaishia. Superpower gani hawa?

Inawezekana vipi nchi ambayo mpaka sasa Rais wake na Makamu wa Rais hawaelewani inaweza kuwa na popular support dhidi ya Tanzania?

Kwa kule kutazamana kwa misingi ya kikabila na kukosa umoja wa kitaifa Kenya inaweza kuwa na national character kubwa kuliko Tanzania?

Ukiitazama Kenya imegawanyija katika itikadi (ideology) kuna maeneo wanaamini katia ujamaa na kuna maeneo wanaamini katika ubepari hasa kundi la watawala hivyo kukosa muunganiko tofauti na Tanzanian ambayo itikadi yake imeelezwa wazi katika Katiba na inajidhirisha hata katika maisha ya kawaida ya watu. Kwa Tanzania mtu kushiriki msiba wa jirani si jambo geni huu ndiyo ujamaa lakini Kenya uone kama hali ipo hivi.

Hili la leadership (uongozi) lipo wazi kwamba wakenya wenyewe wanatamani wangekuwa na Rais wa nch yetu.

Kwa bahati mbaya sana katika Uhusiano wa Kimataifa tunapozungumzia Dola Kiranja (Hegemon) barani Afrika watu wengi hutazama sifa hizo kama zilivyoainishwa hapo juu na kuacha ile nguvu isiyoonekana (Soft power), hasa ushawishi wa nchi dhidi ya nchi nyingine na namna maamuzi ya nchi moja yanavyoweza kuwa na athari kwa nyingine.

Flemes (2007 na 2009) na Ogunnubi (2014) walibainisha hili waliposema:

"Regional power studies on Africa have often excluded soft power to understand the foreign policy behaviour of contenders for regional powerhood. It is also clear domestic challenges have been an important factor in disqualifying some state contenders as regional powers despite their potential or real influence."

Tumejiuliza kwa nini viongozi wengi wa nchi za Kusini mwa Afrika hutembela Tanzania hasa nchi zao zinapokuwa na changamoto? Kwa nini wasiende Kenya? Tanzania ina hii soft power yaani ushawishi mkubwa katika nchi hizo. Hiki ndicho walichomaanisha Flemes (2007 & 2009) na Ogunnubi (2014).

Lakini pia tujiulize, kwa zile changamoto za ndani ambazo Kenya inazo hasa za kikabila na kiutawala kwamba kabila gani liongoze Kenya, wanaweza kuwa dola kiranja?

Mbali na hayo ukuu wa nchi dhidi ya nyingine hupimwa kwa namna maamuzi yake yanavyoweza kuathiri wengine ndiyo maana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema wazi wakati ule ncho nyingi zinafanya lockdown kuwa yeye hatofunga mipaka kwa sababu Tanzanian inategemewa na nchi 8 kufunga mipaka ni kuumiza uchumi wa nchi hizo.

Walizuia malori kule Sirali mwaka 2015, Tanzania ikapunguza safari za ndege kutoka 42 hadi 14 wakaomba kukaa mezani. Walizuia unga wa ngano na gesi ya kupikia toka Tanzania mwaka 2017, Tanzania ikazuia maziwa na sigara wakaomba kukaa mezani. Walifunga mipaka Mei, 2020 Tanzania ikazuia malori wakaomba kukaa mezani.

Tatizo linalonishangaza hadi leo ni kweli hawajui reaction ya Tanzania katika maamuzi wanayofanya? Kama wanajua reaction ya Tanzania na mimi ninaamini wanafahamu hilo, inakuaje wanafanya maamuzi ambayo mwisho wa siku yanawafanya kuwa wadogo kama sisimizi.

Hofu ya Kenya ipo kwenye kuzidiwa kiuchumi jambo ambalo hawawezi kuliepuka wakati Tanzania inatumia akili kubwa kudeal nao.

Wenu:

Abbas Mwalimu (Facebook|Instagram|Twitter).

+255 719 258 484

Uwanja wa Diplomasia (Facebook|WhatsApp)
Nahisi kwamba kwa sababu ya nia ya kupata pesa, most of corona. cases are fix in order get more from WHO. Pili, nahisi pia kwamba maadui waTanzania wanatumia Kenya ili kuifikia Tanzania.

Stori za Tanzania kuwa na wagonjwa wa covid-19 ni za kitambo sana. Hata Zambia waliwahi kutangaza kwamba WaTz wanaanguka barabarani na kufa kwa covid-19 na gali ni mbaya sana, wakati hakuna kitu. Shule na Vyuo vimefunguliwa: hakuna mwalimu wala mwanafunzi aliyepoteza maisha kwa covid-19.

TUACHE MATANI KABISA. TANZANIA NI MFANO WA KUIGWA DUNIANI. Wakenya mjifunze kwa Balozi mpya wa Marekani aliyevua barakoa mbele ya Dr. JPM.
 
Nilitegemea utakua na uwezo wa kujadili hoja kwa kutumia ubongo, hivi ina maana Tanzania yote hakuna mwenye akili ya kuweza kujadili hili janga la corona, nyote mko hovyoo kiasi hiki.

Kila anayeniquote nafungua nikitazamia nitakuta nondo tujadili nakuta ni mipasho utadhani yuko kwenye vigodoro Tandale. Mpaka sasa hata nimejikuta napuuza sifungui comments ambazo niko quoted maana nyote mumekua level moja.
Sasa unataka nondo wakati umeleta vijiti!!!!wewe bata kweli.

Corona haina point za kuijadili tokea ijulikane haina tiba rasmi ila kinga tu,embu tuelezee ni kwa jinsi gani mkipima mnakinga wengine?
 
Ni uchambuzi mzuri ambao haujaingiza ushabiki wa vyama vya siasa ndani na hivyo kuufanya kuwa ni moja ya uchambuzi mzuri na makini kati ya chambuzi nzuri zilizowai kutokea hapa JF.

Hongera sana mdogo wangu. Kenya wanashikiwa akili na nchi za magharibi, hawana akili ya kujitegemea na watashuhudia kwa macho yao Tanzania ikiovertake kwa kasi na kuwa dola kuu lenye nguvu Afrika ya mashariki.
 
Hizi nguvu mnatumia kuficha udhaifu wenu kwenye suala la corona na kulilia Wakenya, mngezitumia kwa kuhakikisha mnapima na na kutolea taarifa za hali yenu hamngejikuta kwenye hali hii ya kukataliwa na dunia, mtaandika hizi insha mpaka mjaze vitabu vya dunia ila hali ni ile ile, corona ni tatizo la kisayansi na linapaswa kushughulkiwa kisayansi sio kwa matamko ya wanasiasa.

Leo hii Mtanzania ukionyesha paspoti ya Tanzania kwenye uwanja wowote wa ndege jamaa wote ghafla wanavaa barakoa na kujilinda na kukupitishia kwenye ukaguzi wa hali ya juu, hii ramani inaonyesha mlivyotiwa alama nyekundu na kanuni za kuwakagua mara mbili mbili.

Yaani mtelekeze jitihada dhidi ya corona kwa jinsi mlivyojichokea kisha muanze kulazimisha na kung'ang'ania kuingia ndani ya mataifa ya watu.

Kwetu huku njooni tumewaruhusu mje maana mumelia sana ila lazima kila anayefika na paspoti ya Tanzania apanue mdomo hadi jino la mwisho lionekane kisha kifaa cha kupima corona kitumbukizwe humo, ukipita huo mtihani wa kupimwa walau mara mbili kisha utfuatiliwa siku 14, utolee taarifa wapi unakwenda na utaishi kivipi, zikiisha hizo 14 basi hapo unaruhusiwa kujiachia huru na kufurahia maziwa na asali ya Kenya.

Health Alert: U.S. Embassy Dar es Salaam | U.S. Embassy in Tanzania

2473175_20200801_164531.jpg
MK 254 UMEANDIKA UONGO MTUPU.
Ulichoandika hapo ni uongo mtupu bro.

Mimi ni shahidi kuhusu hili na nadhani wapo wengine wanakushangaa kwa kutunga uongo kisha unauandika kwa wino mzito.
Nimesafiri kama wiki tatu zilizopita kuja nchi za magharibi. Nimeshuka kiwanja kimoja kwaajili ya connection. Walikuwepo na watanzania kadhaa ambao pia walikuwa wanaconnect kwenda nchi zingine.

Hakuna mtanzania yeyote anayeogopwa wala kutengwa kwaajili ya uchunguzi wa ziada. Tena habari za Tanzania kuwa haina corona zimesikika sehem nyingi duniani.

Watu wana hamu ya kufika Tanzania kujionea hali ilivyo, watu wanatamani kuwaona watanzania ambao wanatoka nchi isiyo na corona.
Duniani huku Tanzania ni washindi. Tunapata heshima kwa kuwa na uwezo wa kujitegeme kusolve matatizo yetu.

Nyie Wakenya bado mnastruggle kupata uhuru kutoka kwa wazungu ndio maana hamuwezi kuwa na njia zenu isipokuwa kuabudu wasemayo watu wa Magharibi.

ACHA KUTUNGA UONGO.
 
Baki kwenye hoja, tunaijadili corona na mbinu zenu za kutokufanya chochote huku mkilazimisha muingie kwenye mataifa ya watu bila kupimwa.

Mimi nimesema mara nyingi humu kwamba nimewahi kuishi Tanzania, nilikatiza mikoa mingi sana hata kuwaliko wengi wenu ambao huwa mumeganda Dar tangu kuzaliwa, hivyo hamna haja ya kunijadili, pambana na mimi kwenye hoja, la sivyo nitakupuuza kama ninavyowapuuza baadhi ya ndugu zako.

Binafsi huwa sina chochote dhidi ya Tanzania nje ya ligi za kawaida baina ya ndugu na watani, ila humu huwa tunaumbuana ikitokea mmoja kaleta taarifa za kuisifia nchi yake ilhali zina kasoro.

Corona ni tatizo la kisayansi, na haiwezekani mkapona kwa kutumia matamko au mikwara ya wanasiasa.
Mimi Niko kwenye hoja...tunajadili hapa issue mbalimbali na hoja mojawapo ni kuhusu nyie wakenya ambao the majority are arogant, jealous, bullish and to a great extent stupid and idiots at the same time...watz hawajataka kwenda nchi nyingine bila sijui kupimwa Corona...the issue ni nyie mnaowawekea ban Watz na ndege zao lakini kwa upumbavu na ujinga wenu mnataka ndege zenu zije TZ ' kwenye corona'...very stupid indeed..TZ tumetumia sayansi kupambana na Corona..we 'activated' our immunity by deciding kuishi na corona kama WHO walivyothibitisha na kuzitaka nchi zote zikubali kwamba ni lazima ziishi na corona..

Tulichukua hatua mapema za kuwaweka watu karantini wanaotoka nje tukasisitiza watu wavae barakoa na kunawa mikono na pia kuji-sanitize...kubwa zaidi tukaongeza na traditional medicine kujifukiza kunywa juice ya limao na tangawizi..sisi hatukufanya ujinga was lockdown Wala mjomba wake na shangazi take lockdown..tukawaondoa hofu wananchi kuhusu corona na wakaendelea kufanya kazi...tunaendelea kumchukua hatua kadhaa..Sasa nyie mnaona wivu kwani maambukizi kwetu yamepungua mno.

Kutangaza takwimu za corona ni ujinga kwani corona haiwezi kwisha kwa kutangaza takwimu...Kama ni kutangaza tangazeni na takwimu za yellow fever, ukimwi, malaria na kadhalika..Wakenya wengi siyo wapumbavu tu Bali wengi wao no wahuni...wakati wa JK Wakenya mulizuia magari yetu yasije Kenya kuchukua abiria na sisi tukazuia ya kwenu mkaanza kulia..Kama ukinipuuza na Mimi nitakupuuza pia...tit for tat...hamwezi kuendelea kuichezea TZ...hakuna Tena...Kila mtu abaki kwake...we don't need arrogant and jealous Kenyans...we don't need you.
 
Back
Top Bottom