Nina hofu ya Hepatitis B naomba ushauri

Hofumoyoni,
Ninachokiona hapa watoa huduma uliokuwa unakutana nao walikuwa wanashindwa kutoa tafsiri sahihi ya nini kinachokusumbua,hivyo kukuacha kwenye msongo mkubwa wa mawazo.

Kwa upande wangu sijaona kitu cha kutisha sana kulingana na vipimo ulivyokiwisha fanya. Nashauri malizia kufanya "CT scan ya ini" ili kjilizisha tu. Kumbuka sensitivity ya CT scan ipo juu kulinganisha na ultrasound.Siyo kwamba naipondea utrasound, tatizo la utrasound majibu yake yanategemea na operator hivyo kuwa na bias.

Narudia tena kulingana na maelezo yako sijaona hatari kubwa yoyote inayokukabili zaidi ya wasiwasi uliokwishajijenga kwenye ubongo wako.
 
moesy, Asante sana mkuu.
Nitazingatia japo wakati mwingine watoa huduma huwa hawapendelei sana kuelekezwa.

Lakini pia nafurahi kwa sababu unaongea lugha ya kitabibu, hii ni faraja kwangu.

Kuna wakati inafikia operators wanaitana kuja kusaidiana ama kushuhudia kilichopo mbele yao, kwa hali ya kawaida ni lazima ikutishe.
 
Usiwe kama yule jamaa aliye jitaa folk bado tunakuhitaji .Hata king hezekia aliambiwa kua hatopona atakufa.....

Bro Mungu akutangulie ktk mapito haha
 
Pole sana bro. Ila haina haja ya kupanic sana haswa ukizingatia kwa sasa unajihisi upo normal ingawa madaktari wanasema unaumwa,Kila siku moja unayoamka ukiwa salama ni muhimu sana kwako na kwa jamii yako Jaribu kuishi maisha uliyonayo sasa,USIKUBALI KESHO YAKO IKUHARIBIE LEO YAKO!
 
Hofumoyoni,

Pole sana ndugu hakika nimeumia sana baada ya kusoma Artical yako. Katika harakati za maisha niliwahi kutembelea nchi za wenzetu "Scandinavia Countries" utaratibu wa kule ni kwamba ukishuka tuu Airport unapimwa HPV then ukikutwa hauna wanatoa chanjo na endapo unamaambukizi wanakupa Kijarida cha kusoma ili ujifunze jinsi ya kuishi na tatizo hilo.

Kimsingi "Human Papilona Virus" ndio wanaosababisha "liver Cirrhosis" na hivyo kupelekea mtu kufariki. Ugonjwa huu umegawanyika katika makundi yafuatayo. Hepatitis A, Hepatitis B na Hepatitis C.

Watu wengi wanapata huu ugonjwa katika mazingira rafiki ambayo ni vigumu wewe kugundua. Mfano. Jasho, Mate, Ngono (Maji maji ya uke). Kimsingi huwa nawaonea huruma sana ninapoona wadogo/kaka zangu wanaocheza mpira halafu Sub mtu anatoka nje anampa mwenzie Tshirt ya sare yenye jasho lake Avae kisha aingie uwanjani kucheza mpira. Utaratibu huu huleta maambukizi fasta mno.

Kuna kipindi nikiwa Bongo nilienda Hospital fulan hivii ya Rufaa ili kupata Vaccine yake lakini nilifeli nikaenda mkoa mwingine kwenye hospital ya Rufaa bado nilifeli. Nilifanya uchunguzi nikagundua kuwa wale "Laboratory Technician" huwa wanapewa chanjo yake kwasababu wapo katika risk kubwa ya kupata maambukizi kutokana na kudeal na Sample mbali mbali za wagonjwa.

My take:

1) Naimani One day Kupitia Rais wetu Mhe. John Magufuli anaweza akafanya utaratibu mzuri wa kutoa chanjo hiyo free kwa wananchi wote ili kunusuru Watoto/ labour force/Wazee waweze kuwa salama na vile vile hao watoto wadogo wapewe chanjo hizo mapema wakiwa wangali wadogo. Akifanya hivyo Mhe atakuwa ameongeza credit sana kwa sisi wanyonge tusiokuwa na fedha za kupata chanjo hiyo.

2) Serikali itoe matangazo yakutoa elimu kuhusu ugonjwa huo maana ni janga kwa Taifa. Jirani yangu hapa ameupata mwezi uliopita, alikuwa ni mcheza mpira sana na amejingundua ana maambukizi ya Virus hao pale mke wake alipokuwa mjamzito na alipopelekwa hospital akaambiwa anatakiwa kuongezewa damu ndipo jamaa akajitolea damu ila majibu ya vipimo yakaonyesha damu yake ina virus hivyo.

Najisikia furaha nilifanikiwa kupata chanjo hiyo lakini bado sijamaliza tiba kamili.
 
KINGSLEE,
Fanya masahisho kwenye bold, unasema human papiloma ndiye anasabisha liver cirrhosis? Alafu amegawanyika kwenye hepatitis A, B na C? Ebu kasome tena alafu ufanye marekebisho.
 
One of my family members was diagnosed with hepatitis B three decades ago, akaambiwa hakuna tiba. Baadae akapata complication ya ini. Alifuata masharti ya dr ya don’ts. My late mother alihangaika na dawa za kienyeji mbalimbali. Ajabu mgonjwa alipona na anadunda vizuri, lakini hajui specifically ni dawa ipi ilimponya kwa sababu alitumia concoction ya kutosha
 
Back
Top Bottom