Black Walker
Senior Member
- Oct 8, 2018
- 107
- 238
Wakuu! Habari za muda huu?
Mimi ni mwanaume mwenye mke na watoto kadhaa, shida yangu ni kwamba nimekuwa nikijihisi kuwa huenda nimeathirika lakini kila nikienda kufanya vipimo majibu yanasomeka negative.
Nilianza kujihisi kuwa hivi kama miaka 11 iliyopita nikaanza kuwa ni mtu wa hofu na mawazo mengi sana yasiyokoma hali hii ilipelekea niwe nahudhuria hospitalini na vituo vya afya mara kwa mara kwa ajili ya kujiridhisha lakini majibu yakitoka yako negative.
Nikaona labda nadanganywa nikawa naenda hadi baadhi ya vituo nalipia lakini majibu yakitoka ni vile vile.
Mwaka jana nilisafiri kwenda mkoani Shinyanga kule nako nikaenda kupima lakini majibu yalivyotoka niko sawa.
Hata navyoandika hapa nina miezi mitatu nimetoka kupima hospitali ya private tena kwa kulipia lakini majibu ni the same.
Ni mtu ambae nina mwili wa kawaida lakini nikijitathmini naona kabisa kwamba kuna shida mahali sio kama nilivyokuwa hapo kabla.
Kiukweli kuna muda nachoka lakini najikaza nikiwaangalia watoto wangu moyo unaniuma sana.
Kama kuna mtu anaweza kunisaidia nipo tayari kufanya vipimo tena na tena na nikigundulika ni mgonjwa pia ninao utayari wa kuanza tiba.
Napatikana Morogoro mjini. Ahsanteni.