Nina hofu ya Hepatitis B naomba ushauri

Nina hofu ya Hepatitis B naomba ushauri

One of my family members was diagnosed with hepatitis B three decades ago, akaambiwa hakuna tiba. Baadae akapata complication ya ini. Alifuata masharti ya dr ya don’ts. My late mother alihangaika na dawa za kienyeji mbalimbali. Ajabu mgonjwa alipona na anadunda vizuri, lakini hajui specifically ni dawa ipi ilimponya kwa sababu alitumia concoction ya kutosha
Can you connect me with that family member of yours?
 
Ndugu, habarini za maisha.

Nachukua fursa hii kuwashirikisha hofu kubwa na kujikatia tamaa kunakoniandama kutokana na kugunduliwa kuwa na HBV.

Mwaka 2000 nilianza kuhisi kwamba size ya spleen imeongezeka. Lakini nilikuwa sijisikii kuumwa na chochote. Nilienda kituo cha afya Dr. akasema ni kweli ni kubwa lakini akasema ni jambo la kawaida, kuna utofauti wa size za spleen kati ya mtu na mtu lakini pia akasema jamii zingine kama Wamasai wanakuwa na spleen kubwa. Hilo lilinipa amani japo mimi sio Mmasai.

Mwaka 2006 nikiwa masomoni, niliamua kwenda kwenye zahanati ya chuo ili nisikie nitaambiwaje pia. Yule Dr. alinipa maelezo yanayo shabihiana na yale ya mwanzo lakini akanituma kwenye kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi. Daktari wa chuo alinitaka niende Muhimbili kufanya vipimo zaidi, ambavyo ni Ultra Sound na Full Blood Picture.

Matokeo ya Ultra Sound ni kwamba nilikuwa na Portal Hypertension ambapo flow ya damu kwenda kwenye ini haikuwa normal na kwamba damu inayokwama inalazimika kwenda kwenye spleen na ndiyo chanzo cha spleen kuenlarge.

Kwenye upande wa damu ndipo ikathibitika kuwa nina Hepatitis B. Kabla ya hapo nilikuwa sijawahi kuusikia ugonjwa huu. Hivyo nilianza kusoma ili niufahamu na ndipo nilipogundua kuwa hauna tiba. Kwa kweli niliishiwa nguvu na mwili kufa ganzi.

Kwa miezi kadhaa nilikuwa sijui natakiwa nifanye nini. Kuna wakati nilijiuliza, kuna haja gani ya kuendelea kusoma? Ila nilipokumbuka mpendwa mmoja ambaye tulikuwa wote chuo ambaye kwa wakati huo yupo chuo alikuwa na saratani, nami nilijipa moyo kwamba bado tumaini lipo.

Dr. wa chuo aliniandikia kufanya kipimo kingine cha mfumo wa chakula Endoscopic pale Regency ambapo ilionyesha kuna mishipa inaanza kutanuka kutokana na kupokea damu nyingi lakini inayotoka ni kidogo. Hivyo nilishauriwa kutofanya mazoezi mazito sana kwani yanaweza kupelekea kupasuka kwa mishipa hiyo.

Taarifa hii ilinikumbusha kipindi nipo darasa la sita, kuna mwalimu mmoja alikuwa analazimisha wanafunzi wote kukimbia kuzunguka uwanja hadi round 20 na kuendelea, na ukishindwa unapata viboko visivyo na idadi. Ni kipindi hicho tunakimbia nilijihisi kifua kubana, ila kwa hofu ya viboko niliendelea.

Baada ya kutulia nilianza kukohoa mate au makohozi yaliyochanganyika na damu. Hali hii iliendelea kwa miaka kila nilipokimbia, kufanya zoezi la viungo linalohusisha kunyonga mikono au kifua, au kuogelea kwa muda mrefu baadaye nilitoa makohozi yenye damu. Na nilipoenda kwenye kituo cha afya nilipimwa makohozi nikaambiwa niko salama sina TB.

Baada ya taarifa mpya juu ya afya yangu, niliendelea kuhudhuria Clinic Muhimbili, na Dr. aliyekuwa ananiona kwa wakati huo alisema sina sababu ya kutumia dawa yoyote. Mwaka 2016 nilifanyiwa US ambapo baada ya kupimwa walionyesha mshituko wa wazi, nilipomdadisi yule mmoja alisema kwa hiki kinachoonekana Mwenyezi Mungu akuonekanie.

Ni maneno ambayo yaliibua hofu yangu ya siku nyingi. Ikumbukwe kwamba, pale nilipo huwa ninajihusisha na mambo ya ushauri kwa vijana, kwa hiyo hata ninapowauliza madaktari ninaona kama wanajaribu kunituliza tu kwa kutumia mbinu ambazo hata mimi huzitumia.

Kitu cha ajabu zaidi ni kwamba, sijisikii kuumwa lakini ninapokuwa na watoa huduma wananiangalia kwa mshangao wa dhahiri. Kuna wakati ninaulizwa, mgonjwa yuko wapi? Kwa sasa ninaendelea na tiba Muhimbili, lakini inavyoonesha nimeshapata Liver Cirrhosis. Kuna wakati nilisikia kwamba MNH wana mpango wa kuanza huduma ya kupandikiza ini, lakini kwa sasa inaonekana kama zoezi limesimama na kwa sisi Watanzania masikini hatuna hata ndoto ya kupata huduma nje.

Kwa muonekano wangu mimi ni mzima sana, na sina historia ya kupata hata malaria au mafua. Ajabu ya kuumwa kwangu ni kwamba kunaonekana kwenye vipimo tu wakati mimi ninendelea na majukumu yangu kama kawaida.

Ninajua sote tu mavumbi na mavumbini tutarudi, lakini kuna wakati nafsi yangu inakuwa na maumivu makali ambayo siwezi kuyaelezea. Sijui mpaka lini, ila ninamuomba Mungu awasimamie wale wanoendelea na tafiti za tiba halisi ya maradhi haya.

Nina hofu na maumivu ya nafsi. Mungu awabariki nyote na kuwaepusha na madhila ya namna hii.

Asanteni.
pole sana mkuu,mimi nimepitia magumu mengi hasa kwenye afya,lakini still napambana ,japo yangu na yako ni tofauti...
 
pole sana mkuu,mimi nimepitia magumu mengi hasa kwenye afya,lakini still napambana ,japo yangu na yako ni tofauti...
Pole mkuu.
Maisha ni mitihani, tuendelee kuyakabili kwa namna yanavyotujia. Tuamini Mungu ana makusudi na maisha yetu.
 
Asante mkuu.
Ukiniona huwezi fikria kama nina tatizo la kiafya.
Niko stable na sijisikii kuumwa na chochote, ila vipimo vinaonesha hali yangu si shwari.
Pole Mkuu dawa umeshaanza kutumia?
 
kama hadi sasaivi hujisikii kuumwa naimani kubwa..kuna siku utaenda hospital hawatoona ugonjwa...Mungu hutukumbuka ni swala la Muda tu
 
Hauna haja yakuwa na hofu, maana wote tutakufa. Nivile hatujui siku wal saa, ishi kamilisha ndoto zako, gusa maisha ya wengine. Ikiwezekana andika kitabu chenye lengo laku wapa moyo wengine wenye maradhi, fikra zako zitaishi milele. Dr ni binadamu, wako walio ambiwa hawatamaliza mwaka ila miaka 30 imepita wako hai. Mimi siamini kwenye impossible as long God is alive. Nakuja PM tushare kitu kidogo.
 
Pole na changamoto ya afya unayoipitia nimewahi kusikia majani ya ukwaju ni dawa unaweza Kujaribu kama ukipata amani ya kuyatumia
 
Hauna haja yakuwa na hofu, maana wote tutakufa. Nivile hatujui siku wal saa, ishi kamilisha ndoto zako, gusa maisha ya wengine. Ikiwezekana andika kitabu chenye lengo laku wapa moyo wengine wenye maradhi, fikra zako zitaishi milele. Dr ni binadamu, wako walio ambiwa hawatamaliza mwaka ila miaka 30 imepita wako hai. Mimi siamini kwenye impossible as long God is alive. Nakuja PM tushare kitu kidogo.
Nakushukru
 
Back
Top Bottom