Hofu ya CCM dhidi ya Zitto kufukuzwa CHADEMA

Hofu ya CCM dhidi ya Zitto kufukuzwa CHADEMA

Status
Not open for further replies.

why

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
203
Reaction score
82
HOFU YA CCM DHIDI YA KUFUKUZWA KWA ZITTO CHADEMA.
Kumekuwepo na hofu kubwa kwa watawala na wanachama wa CCM juu ya kufukuzwa kwa naibu katibu mkuu wa CHADEMA Mh Zitto Zuberi Kabwe kitu ambacho bado wengi wamekuwa na maswali baina yao kwa nini msiba huo ambao ulitarajiwa kubebwa na wana CHADEMA cha kushangaza unabebwa na CCM.
Taarifa za kushitusha zilitokea tuu baada ya kikao cha kwanza kilichomsimamisha Zitto Kabwe uongozi na kikao kikafanyika kati ya January Makamba, Deo Filikunjombe, Mwigulu Nchemba, Mohamed Dewji, Nape Nnauye pamoja na Zitto kabwe kilichafanyika Level 8 katika hotel ya Hyat Regency Kilimanjaro, Pamoja na majadilino juu ya kuvuliwa nyadfa zake aliulizwa kuwa ni kwa nini mkakati huo ulivuja ndani ya chama chake naye alidai ni kwa sababu Mwigamba wamekua katika migogoro na Godbless Leman a ndio chanzo cha kuvuja kwa mkakati huo, lakini aliwatoa hofu washirika wake alipowaambia kuwa anao uwezo wa kumaliza hali hiyo ya sintofahamu ndani ya chama chake kwani anao ushawishi na anaweza kushawishi wajumbe na kuweza kumpinga mwenyekiti wake wa chama.
Lakini walionesha hofu kubwa sana kama Zitto atashindwa kurudisha nyadhfa zake ndani ya chama kwa kuwa uwekezaji uliofanywa umetumia nguvu kubwa ili kuweza kupita salama katika kipindi hiki cha uchaguzi wa seriakli za mitaa, lakini kikubwa ni kura ya maoni na uchaguzi mkuu ujao, lakini hofu ilitanda zaidi baada ya kamati kuu kuwafukuza rasmi Kitila Mkumbo na Mwigamba ndipo walipoamka na kuitaka mahakama isubiri kwanza na kutoa maamuzi siku ya pili ambapo kikao kilifanyika Ikulu kikiongzozwa na Vigogo wa serikali kwa maagizo ya Rais kuitaka mahakama ibadili maamuzi ambayo yalitarajiwa kufanywa na kutaka mahakama itoe amri kwa CHADEMA na Zitto abaki na ubunge wake huku wakijiandaa kuja na mbinu mbadala ya kuiadhibu chadema.
Mkakati unaoandaliwa sasa ni kutengeneza mienendo yenye kuonesha CHADEMA inakiuka misingi ya kidemokrasia na kuonesha kukiuka sheria ya uanzishaji wa vyama vya siasa kwa lengo la kuipoteza CHADEMA kabla ya kuifikia uchaguzi mkuu ujao, bado naamini viongozi wa CHADEMA mnayo fursa ya kuendelea kusimama imara na kuonesha uongozi katika kuheshimu katiba ya chama chenu.
CHADEMA kumbukeni Zitto alianza kukisakama chama aliposema Ruzuku haitumiki sawa hii haikuwa agenda yake niliwahi kusema mapema juu ya hili,kuwa iweje agenda ya Zitto ibebwe na Nape na mwigulu hamkuona kama nina maanisha nini kwa wakati ule lakini sasa mnaweza kuona nini kilikuwa chini ya agenda hiyo, lakini niliwahi sema juu ya mabilioni ya uswis ka nini sio agenda ya chama na kwa nini yupo nayo peke yake kitu ambacho si cha kawaida kwa hoja zinazotoka CHADEMA? Lakini pia hatima yake ikawa ni baada ya kuitwa na wamiliki wa mabilioni baadhi ambao walilengwa na hoja hiyo isipo kuwa Mh Mbowe ambae amekuwa akijiamini na umililki wa fedha zake mali nje ya nchi kuwa ni halali ndio mana hakuwa nahaja ya kuzungumza na mtu wala kumhonga mtu, moja ya vigogo waliomwita Zitto na kufanya nae mazungumzo ya kuwataja wamiliki wa mabilioni ya uswis alinukuliwa akisema katika vyombo vya habari kuwa ni vema sasa Zitto akawataja hao wamiliki ili ijulikane nani ni mwizi, huku akijua kuwa tayari alishafanya mazungumzo nae na walishakubaliana kutowataja, lakini pili alipohojiwa kwa kiapo chini ya mwanasheria mkuu wa serikali alikana kuwa na majina hayo ya wamiliki wa fedha nje ya nchi na kutaka serikali ishughulikie mfumo mzima wa utoroshaji fedha.
Hofu dhidi ya CHADEMA imeendelea kutanda kwa kuwa chama hiki kimeendelea kutoa msimamo wake juu ya kuanika ufisadi nchini na kushughulikia swala la mabilioni ya uswis ambapo bado wana CCM wanashaka nani sasa ndio msemaji wa hoja hiyo mana wanajua siri itakuwa wazi kwani waliamini msemaji ni Zitto ambae walifanikiwa kuzungumza nae na akakubali kuwa kimya, je sasa nani wa kumfata? Lakini CCM wamekuja na mkakati mpya wa kuhakiki wanamkosesha mamlaka Mwenyekiti wa chama kwa kuzungumzia masuala yake binsfsi na familia yake, lakini cha msingi ambacho naona mwanga ndani ya CHADEMA ni pale wanapoweza kubeza hoja ya maisha binafsi ya kiongozi wao ambapo hawahitaji kujua zaidi ya kuimarisha chama chake ambacho amekifikisha kilipo sasa huku wanachama wakihoji tuhuma hizo zilizotolewa na Zitto kuwa je anayo nia ya dhati ya kukisaidia chama kwani kama yeye angekuwa mwenyekiti angeacha ufuska alionao sasa, na kwa hili nikamshangaa mwanajamii mmooja ambae alithubutu kuwataja Wanawake alioweza kuwa nao kimapenzi Ndugu Zitto Kabwe kama Mtoto wa Kikwete, Waandishi wa habari 6, Wabunge wa CCM 3, Mbunge wa CUF 1, Mbunge wa CHADEMA 1 na viongozi wa Chama mikoani je huyu anaweza kujifananisha na Mbowe kwa yale anayoyasema?
Hofu hii ya CCM haiwezi kukiacha CHADEMA kikiwa salama ni dhahiri itakwenda kuwa na madhara makubwa kwa CHADEMA pale CHADEMA ispochukua tahadhari ya kuonesha uongozi ulio stahimilika mbele ya wanachama na wapenzi wake wa chama, lakini pia CCM ni vema ikajielekeza katika kuwasaidia wananchi katika kutatua kero zao kubwa na sio kuishi kwa kutengeneza watu wasio waaminifu ndani ya chama na kuvujisha taarifa za vyama ili kupunguza nguvu ya wapinzani wanaohoji juu ya uwajibikaji wa dola kwa wananchi.
Kwa kuwa sio mshabiki wa chama chochote lakini napenda sana harakati za CHADEMA na kujikuta nahitaji sana CHADEMA iliyo imara kwa kuwa imetutoa katika vimbunga na kutuweka katika unafuu ambao bila CHADEMA huenda sasa tungeweza hata kununua umeme kwa sh 2000 kwa uniti moja ingawa bado tunahitaji nguvu kubwa ili tutoke hata hapo tulipo na kupunguza gharama za umeme ambazo ni kero kwa wananchi tulio wengi.
Hofu hii ya CCM kutoka madarakani na kuacha CHADEMA itawale isijikite kukimaliza CHADEMA kisiasa ijikite kutekeleza ahadi zilizo ndani ya ilani za CCM tangu 2005 na 2010 huenda ukawa ndio muarobaini wa CHADEMA kutoingiza ikulu ila kwa kupiga kelele juu ya maamuzi ya CHADEMA kwa wanachama wake haiwezi kuwatoa katika hoja yao ya kuwasaidia watu kwa kulinda makubaliano yao na wananchi yaliyomo katika katiba ambao hutafsiriwa kuwa ndio mkataba wao na wananchama na nwanachi.
 
CCM watakuja kushtuka baadaye watakuta mtoto kumbe siyo wao, Nchi itakuwa mikononi mwa chadema
 
ukiweka paragraph nitarudi, vinginevyo inachosha
 
CCM watakuja kushtuka baadaye watakuta mtoto kumbe siyo wao, Nchi itakuwa mikononi mwa chadema
amka wewe kushakucha!!!!!!!!acha ndoto.....au ndio unafukuzia nafasi ya ndoto za clouds media?sio kwa mtindo huo sasa
 
Msiba wa jirani wewe mpita njia unalia kuliko aliyefiwa
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom