Hofu Siyo Heshima ya Kweli

Hofu Siyo Heshima ya Kweli

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,061
Reaction score
850
Ukishakuwa na watoto wanaofikiri kukuheshimu ni kukuogopa, watoto wasioweza kuonesha hofu zao mbele yako, wasioweza kukasirika mbele yako, wasioweza kukueleza hisia zao, wasioweza kusema mawazo yao mbele yako, ni suala la muda tu utashangazwa wakishaanza kuamini huna unachoweza kuwafanya.

Usidanganyike na utulivu usioambatana na uhuru. Usidanganyike na nidhamu inayotegemea woga. Usidanganyike na adabu inayoegeshwa kwenye unafiki. Binadamu ukimlazimisha kukuogopa atakushangaza. Familia inaweza kuwa na utulivu wa hatari unaochochea mifarakano mikubwa mbeleni.
 
Back
Top Bottom