Hofu kubwa

Fyong'oxi

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
266
72
Ninae mpenzi wangu ambaye tumekuwa kwenye uhusiano katika kipindi cha miaka miwili sasa naTunapendana mno.

Nimefanikiwa kupata nafasi ya kwenda kusoma Degree ya pili nje ya nchini Canada. Ninatarajia kutumikia masomo yangu katika kipindi cha miaka miwili mfululizo bila kurejea nyumbani TZ kwakuwa kipindi cha likizo ninatarajia kufanya shughuli fulani ya kuniingizia pesa nikiwa hukohuko.Tunaahadi ya kuoana baada ya mimi kumaliza masomo nirejeapo nyumbani TZ.Yeye amemaliza masomo yake ya degree ya kwanza ndio kwanza anatafuta kazi sasa.

Hofu yangu ni kuwa
-Je ni kweli atakuwa na moyo wa kusubiri nimalize masomo tutimize ndoto zetu?
- Je nikweli atakuwa na uwezo wa kuvumilia bila kuwa na mwanaume/au kufanya mapenzi kwa kipindi chote cha miaka miwili?
 
hofu na mashaka kwako wewe uliembali na macho yangu.............. umenukumbusha mbalisana...... UNAMAANISHA HUTAKI KIMPOTEZA????? na je yeye ame respond vip kulingana na situation iliyopo
 
wewe unaweza kutenda hayo unayomuuliza?? if yes ongea nae na umwamini kama yeye anavyokuamini, otherwise ____
 
Those same questions can be asked to u pia.
Usiencourage negative thoughts, kuwa na imani kuwa atakusubiri na mtakuwa pamoja; if she can't it is her loss, the same way ukishindwa wewe meaning u are not worth her love!
 
Sasa unataka Jf wakujibie swali au? Wewe nenda shule, ikirudi ukimkuta na bado mnapendana, oa.
 
Trust me, ukienda huko UTAFUNGUKA UPEO!!!! Hata ukirudi mapenzi yatakuwa magumu. APANA CHEZEA LONG DISTANCE RELATIONS!!!!!!! Kwanza hata perception yako ya vitu vingi ukirudi itakuwa imebadilika!!!! Binafsi alieniacha akaenda huko 1st world IMEBAKI STORY TU. 
 
Binafsi nakushauri usichukulie mzaha mambo ya distance relationship..yana consequences nyingi aisee!!
Achana na habari kwamba 'utamkuta tu'...kuna jitihada zinahitajika kuhakikisha kwamba kwa miaka hiyo miwili mambo hayawi mabaya. Binafsi ningeshauri ujitahidi uwe unarudi japo mara moja au mara mbili kwa mwaka. Vinginevyo lolote linaweza tokea..nikisema hivi ninao ushahidi wa kutosha!..Kikubwa communication iwe kama sala ya baba yetu!
 
Hofu yote yanini?
Kama ana kupenda kweli bila shaka atakuvumilia na kukusubili.

Naamini unamjua vizuri zaidi yetu!
Hebu twambie kwanini una wasiwasi?
 
Hapo mkuu lolote laweza tokea..
Uwezekano wa yeye kukusubiria na akiwa mwaminifu upo na kuchoka kusubiri pia inawezekana, yote hayo ni kutokana na msimamo wako na utaratibu utakaojiwekea kulinda hiyo distance relation.
Ila inaonekana we mwenyewe hujiamini, Chagua 1.
 
Jiulize vp na wewe utaweza yote hayo?

Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums
 
hofu na mashaka kwako wewe uliembali na macho yangu.............. umenukumbusha mbalisana...... UNAMAANISHA HUTAKI KIMPOTEZA????? na je yeye ame respond vip kulingana na situation iliyopo

Yeye amesikitika mimi kwenda mbali, ingawa alikuwa akinipa moyo wa umuhimu wa kusoma zaidi
 
Those same questions can be asked to u pia.
Usiencourage negative thoughts, kuwa na imani kuwa atakusubiri na mtakuwa pamoja; if she can't it is her loss, the same way ukishindwa wewe meaning u are not worth her love!

Kwangu mimi ninamoyo naye sana katika future yetu. wasiwasi ndio umenifanya niombe ushauri
 
Trust me, ukienda huko UTAFUNGUKA UPEO!!!! Hata ukirudi mapenzi yatakuwa magumu. APANA CHEZEA LONG DISTANCE RELATIONS!!!!!!! Kwanza hata perception yako ya vitu vingi ukirudi itakuwa imebadilika!!!! Binafsi alieniacha akaenda huko 1st world IMEBAKI STORY TU. 

Kw hiyo nianze tuu kujikatia tamaa au?
 
Kwanini msifunge ndoa mkaenda naye.

Ndoa ya harakaharaka ilikuwa ni ngumu kutokana na mda, na hii nafasi ya masomo iliyojitokeza ni ya kwenda mbali.nilikuwa na wazo la kumvisha pete ya uchumba ila bado likawa na mijadala mingi ya ndugu zake na ndugu zangu!
 
Kuna msemo usema "aliwazalo mjinga ndilo litakalo mtokea" look hard the way u think about her
 
Hofu yote yanini?
Kama ana kupenda kweli bila shaka atakuvumilia na kukusubili.

Naamini unamjua vizuri zaidi yetu!
Hebu twambie kwanini una wasiwasi?

Namwamini sana, ile sometimes nashindwa kutabiri chochote kutoka nafsi yake, na woga wangu wa kugeukwa!
 
Back
Top Bottom