Hofu husababishwa na nini?

Binafsi natambua hivi;
Hofu ni hali impatayo mtu pale anapokosa ujasiri/ni matokeo ya kukosekana kwa ujasiri...kwa tukio hatarishi ambalo bado halijatokea, linalotokea au linatarajiwa kutokea.

Hivyo mtu anapokosa ujasiri iwe ni 'inner power' au 'physical ability' huingiwa na hofu na kuona kuwa atamezwa na hatari iliyopo mbele yake...

Unaweza kuikimbia hofu kwa kufanya au kufuata yafuatayo;
1. Kujiamini (kuwa na mtazamo chanya)...

2. Kujiandaa kimwili na kiroho...(kuwa na ujuzi wa mambo yanayokukabili na yatayokukabili)

3. Kuomba msaada toka katika NGUVU zilizokuzidi nguvu...

 

Anawezaje kushinda jambo hilo na kua hulu kifikla kisha kutatua tatizo?
 

inasababishwa na life experience, kwako au kwa kuona kwa watu wengine.
 
Atiii???

Mbona umeni-quote tena miye miye Watu8?

Nimezinguka... Hahaaa
Kujibu swali lako kwanza yapasa kujua Binadamu ni kiumbe kilichoumbwa na kupewa uwezo mkubwa mno ambao ni free will. Yaani binadamu ana uwezo hata wa kumkana aliyemuumba na akatumia will yake kujidai anavyotaka humu Duniani.
Lakini mimi binafsi naamini katika Higher power na naona ukiamua ku align your will with the higher power unakuwa even more powerful.
Kwahiyo nikiangalia jibu lako la post #21 naona umeiweka vyema all the same.....lol
 
Hahah...pole sana kwa kuzinguka lol

Kwa kujibu hivi sasa nadhani nimekuelewa...

 
Fear is not real. It is a product of thoughts you create by forecasting what will happen. Do not
misunderstand me. Danger is very
real. But fear is a choice.
 
Ni mawimbi ya fikra tu yanapojihami... Wakati mwingine ni defence mechanism ya ubongo.
^^
 

nimecheka sana!well said ndugu
 

Mkuu mbona mstari uliou-quote hauzungumzii Hofu bali hasira..., au nimeshindwa kuelewa!
 


Sawa kabisa mpwa Watu8. . . . Kuchagiza kidogo tu ni kuwa namba moja msingi wake uko kwenye namba mbili "Kujiandaa" hapa ndipo haswa kwenye ushindi dhidi ya hofu. . .Kujiandaa kifikra, kiuchumi, kisaikolojia, na yote yahusianayo na jambo ambalo unaenda kulikabili na ili kuishinda hofu na kuishi kwa kujiamini ni bora kila mtu ajiweke katika hali ya tahadhari kwa mambo kama ugonjwa, vifo, hali ngumu za kimaisha kama uchumi, ujuzi wa kazi unayoifanya na mambo kama hayo ujitengenezee "comfort zone" ambayo lolote likitokea basi una operate humo kwenye zone yako.. . . . . . .Jiandae kana kwamba uko peke yako ili ikitokea hali itayosababisha ukose msaada basi ndani ya zone yako uweze kukabili changamoto hata pasipo msaada!!! Ingawa pia unatakiwa uwe na social capital sambamba na comfort zone yako binafsi. . .. .

Mwisho ni kumuomba sana Mungu akuepushe na yale yasiyo na heri kwako, akutie nguvu juu ya changamoto za kilimwengu na kiimani. . . .
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…