vukani
JF-Expert Member
- Dec 30, 2009
- 244
- 166
Wana JF,
Jana nilikuwa na Dine na rafiki yangu mmoja, binti wa Kijerumani katika mghahawa mmoja marufu ulioko maeneo ya Masaki..
Yeye, yuko hapa nchini kama Expert akiwa anafanya kazi katika sekta ya Utalii.
Wakati tukiendelea kula huku tukipiga soga, mara wakaingia Wachina kama kumi hivi wakataka waandaliwe meza ya pamoja, lakini baada ya kuingia hao Wachina, atmosphere ya pale ndani yote ilibadilika kwani karibu wateja wote waliokuwepo pale ndani ambao mostly walikuwa ni wazungu waligeuka kuwatazama.
Wachina wale walikuwa wakiongea kwa kikwao tena kwa sauti kiasi kwamba utulivu uliokuwepo pale mghahawani ulitoweka ghafla.
Yule rafiki yangu ambaye muda wote alikuwa amewatumbulia macho, alinigeukia na kuniuliza, "Ninashangazwa sana na serikali yenu kuwakumbatia Wachina kiasi hiki, mnadhani watasaidia kuinua uchumi wenu"
Kwa kifupi nilimjibu kuwa huu ni utandawazi na serikali yetu haina mkataba na taifa Fulani kuwa ndilo lenye mamlaka ya kuingia na kuishi au kufanya kazi hapa nchini, kwa hiyo yeyote yule mwenye kutaka kuja kuwekeza hapa nchini anaruhusiwa ili mradi asivunje sheria a afuate taratibu za kuingia hapa nchini basi.
"Nadhani huko sahihi", alisema binti wa Kijerumani, "Unajua sisi inapotokea tunataka ku renew working permit zetu, kunakuwa na usumbufu mkubwa sana, ukilinganisha na hawa Wachina, wao wapo kila mahali na wanafanya biashara ambazo zilipaswa kufanya na nyie lakini hawabughuziwi kama tunavyobughuziwa sisi wazungu, imefikia mahali sasa tunahisi kubaguliwa waziwazi tofauti na hawa Wachina"
"Wewe unadhani tatizo ni nini?" Nilimuuliza.
"Sikiliza, hawa wachina ni wajanja sana wameleta miradi ya ujenzi wa barabara kama danganya toto, na katika miradi hiyo wamejipenyeza kwa kisisngizio cha expert na baada ya mradi kuisha wanendelea kuishi hapa nchini kwa kisingizio kingine cha wawekezaji ambapo hufanya shughuli ambazo zilipaswa kufanywa na nyie wazawa, na wamejipenyeza katika maeneo ya uswahilini na kuishi na wenyeji kwa ushirikiano na wamejifunza Kiswahili kiasi kwamba wamegeuka sehemu ya jamii ya chini kabisa, lakini baadae hawa watu wata take over kila kitu na kuwaacha mkishangaa, sio watu hawa jiangalieni"
"Ok, kwa nini na nyie msifanye hivyo" nilimshauri,
Haiwezekani, unajua sisi tuna utamaduni tofauti na nyie, lakini Wachina huenda utamaduni wao hauna tofauti kubwa na wa kwenu na ndio maana wameweza ku corp na society yenu bila shaka" alinijibu……….
Nilishusha pumzi...........
Kwa kifupi mjadala ulikuwa ni mzito na mrefu kiasi kwamba ulichukua sehemu kubwa ya mazungumzo yetu…….any way labda nilichotaka kuwauliza wana JF,ni Je kuna haja ya watanzania kuhofia ujio wa hawa wachina, au wamekuja kusukuma mbele gurudumu la maendeleo?…………………