'Hodhi' ya majimbo... Inakuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Hodhi' ya majimbo... Inakuwaje?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by WomanOfSubstance, Jun 24, 2010.

 1. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Inakuwaje mbunge ulalamike ati kuna watu wananyemelea jimbo lako! Kwani hilo jimbo umeliwekea "hatimiliki"? Nijuavyo mimi mtu anapopata ubunge, anadumu miaka mitano kisha uchaguzi unapowadia wananchi watapima na kuamua wamrudishe au wamuondoshe ili waweke mtu mwingine atakayewahudumia vema.Sasa wananchi watachagua vipi kama incumbent anang'ang'ania na kukataa ushindani? Nimeshaona hadi sasa wabunge kadhaa "wakilia" wanaingiliwa majimbo yao - mfano ni mama Anne Kilango Same Mashariki na Dr Zainab Gama - mbunge wa Kibaha.Badala ya kulialia kwanini msiache wananchi ( mabosi wenu) waamue wanamtaka nani?
  Ndugu yangu kama mpiga kura je hii imekaaaje?..kwangu mimi imekaa vibaya sana!
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Jun 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  nadhani wanacholilia (kama tunaweza kuita hivyo) ni mbinu chafu za kuwanyima wananchi nafasi ya kuwachagua tena. Mbinu ambazo wakati mwingine kwa maoni yao zinapakana na vitendo vya uhalifu na ndio maana wanataka vyombo vya sheria vifuatilie. Sidhani kama kuna mtu ambaye atalalamika kama watu wanajitokeza kugombea katika mazingira mazuri.
   
 3. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2010
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,219
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280

  Mwanakijiji,
  Mbinu walizoingilia madarakani akina Kilango na wenzake ndo hizo hizo ambazo zinatumiwa na wale wanaotangaza 'NIA' za kugombea majimbo hayo. Sijajua kwa nini hawa wabunge walio madarakani wanalia lia ovyo utadhani majimbo ni 'YAO'. Tatizo wanataka kuziba njia ambazo wao walipitia, ili wanaokuja wasipite hizo, wakati njia hizo ndio short cut za kuelekea kwenye unono.
   
 4. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  What goes round comes round.. sidhani kuna mbunge hata mmoja anaweza kujigamba kuwa ati hakutumia mbinu "tainted" kama siyo "chafu" kuwalainisha wapiga kura haswa wale walio kwenye "vulnerability". Kila mbunge ama katoa chakula, au katoa chochote japo hata " kitochi" ili akumbukwe kwenye kura....Bila shaka wanaowania nao wanatumia mbinu ili waonekane kwa mpiga kura. Takrima ilishapigwa marufu kisheria lakini bado kuna vijitakrima vinaendelea pamoja na TAKUKURU kutoa onyo.

  Labda ndugu zanguni MKJJ na wengineo tujadili ni vipi mbunge utaenda jimboni na maneno matupu uwavute wananchi waache mashamba yao na shughuli zao waje wakusikilize wewe na ahadi zako.

  Ninatumia uzoefu wangu kwenye shughuli za kijamii huko vijijini.Ukienda hata kwenye utafiti angalau lazima u oganazi wananchi wapate japo ubwabwa na chai ya rangi ndipo wakusikilize na wakupe ushirikiano na hapo ni kwa manufaa yao- huendi kuwaomba kura wala kula!
   
 5. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Bado tuna mengi ya kusikia
  Watuachie wananchi tuamue na wasitupangie
  Siku zote wanatumia mbinu chafu mno!!!!!!!!!!!!!
  Tuwe macho na uppuzi uliojaa ndani ya ahadi zao
   
Loading...