Habari wana jf, kutoka bungeni jioni hii.
Mh. Mkosamali amehoji juu ya kazi gani maalumu aliyonayo "waziri wa nchi,ofisi ya raisi kazi maalumu" profesa mark mwandosya.
Profesa alipopata nafasi ya kuchangia hoja alianza kwa kujibu hoja ya mkosamali kwa kusema "kazi niliyonayo ni maalumu".
Mkosamali alihoji suala hilo kwa kua haoni ulazima wa kua na wizara hiyo kwa kua pesa inayotumika kuendesha wizara ni nyingi na akashauri ifike wakati serikali ibane matumizi yasiyo ya lazima.
Mwana jf, wewe unadhani hiyo kazi maalum ya mh.mwandosya ni ipi ambayo haiwezi kutekelezwa na wizara nyingine ama taasisi nyingine za serikali?
Usiyejua utokako, hata unakoelekea hujui!Kwani Nyerere ni nani ? Mungu ? Mtakatifu ?
Una mawazo ya chekechea.Anaweza ku exercuse hizo ministerial power zake akiwa nje ya Baraza la mawaziri au angempeleka wizara soft kama Habari, Kazi na ajira au wanawake na watoto kuliko kumrundika kwenye kabinet kuongeza gharama unnecessarily
No wonder wanaCCM wanataka tutunge Katiba nyingine mpya MBOVU ili waendelee kufanya u.puuzi walouzoea!!!!Madhara ya Katiba mbovu inayompatia fursa rais kuteua mtu yeyote na idadi yoyote ya mawaziri wakati mwingine kadri anavyoshauriwa au kadri ya maslahi na matakwa ya mke wake au hata watoto wake.
Profesa na taaluma yake anakubari kudharirishwa kwa kupewa kazi maalum!!?
Nna haraka kidogo bosi wangu ntakujuza nikirejea sorry for inconvinience caused.mkuu huko downstairs ndo wapi tena?
Huyu mh ametangaza nia ya kugombea Urais! Muda mwingi yuko ofisi ya Rais,waziri asiyekua na wizara maalum mwenye kazi maalum.
Kwanini tusiamini kwamba huyu mh tayari alikua anaandaliwa kurithi ofisi hiyo? Tunafaham mpaka sasa anaifahamu vizuri ofisi hiyo!Huyu mzee anakubalika sana katika jamii kwa kutoa ushauri, Ni mtu wa watu, hana hata chembe ya kashfa ya aina yeyote ndani ya utumishi wake wote japo naye sio Malaika.
Naikumbuka sana ile siku mheshimiwa huyu alipoingia bungeni baada ya kutoka kwenye matibabu India jinsi ambavyo Ukumbi wa bunge ulirindima!
Nakumbuka jinsi alivyoguswa na lile sakata la ESCROW na kusimama kutoa msimamo wake jinsi alivyochukizwa na suala hilo.
Ila wasi wasi wangu ni kufanya maamuzi magumu kwa masuala mbali mbali na makubwa yahusuyo taifa! Ni mpole sana.
Mwenye koneksheni tafadhali...Cha muhimu kwa sasa ni afya yake itengemae. Sijui kazi maalumu ndio nini ila Ikulu kuna kazi nyingi hata kusoma makaratasi yanayoletwa kutoka kila kona inaweza ikawa kazi maalumu pia.