Hizi Traffic signs mpya zinatuchanganya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi Traffic signs mpya zinatuchanganya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MdogoWenu, Dec 2, 2011.

 1. M

  MdogoWenu Senior Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 174
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Jamani,

  Leo hapa D'Salaam nimepita Bridge street. Wasiofahamu majina ya mitaa hii ni kwamba ni ule mtaa ambao ukiwa unaelekea baharini unapita katikati ya iliyokuwa Forodhani Secondary ikiwa kushoto na Kanisa Katoliki la Saint Joseph linakuwa upande wako wa kulia.

  TUmezoea kwamba ukifika hapo unakutana na Sokoine Drive ambayo kwa miaka mingi ni One Way Street na hivyo kuna alama inayokukataza kupiga kona kuingia upande wa kushoto na hivyo unalazimika kupiga kona kungia kulia.

  Leo nilipofika hapo nikaona imeongezeka alama inayofanana na ile lakini inaonekana kama nakataza kupga kona kuingia kila!
  Hivyo, kuna alama mbili sasa, moja inakataza kuingia kushoto na nyingine inakataza kuingia kulia. Nimeuliza traffic police aliyekuwepo kwa kweli haikunisaidia nikakumbuka kwamba JF kumejaa kila aina ya wataalamu hata kama mimi kuna baadhi ya mambo nimesahamu wakati ninajifunza udereva miaka 20 iliyopita.

  Nilipokumbuka JF nikaona maneno hayatoshi na nikaamua kupiga picha yenye alama zote mbli kama inavyoonekana hapa.

  Traffic.jpg

  Je, wandugu,

  Mnaweza kunisaidia kwamba alama zote hizi mbili ni za nini, maana leo nimetumia dakika kadhaa ku-park gari na kutafuta ni ipi niifuate?

  Saidia, tafadhali. Kuuliza si ujinga kama kusahau kusivyokuwa ujinga iwapo nimesahau.

  MdogoWenu
   
 2. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona zinaeleweka
   
 3. M

  MdogoWenu Senior Member

  #3
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 174
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Ni vizuri umejiunga na mimi pamoja na kundi zima linalosubiri kwa wale zinazoeleweka watueleweshe zina maana gani.
   
 4. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #4
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hurusiwi kwenda kulia,kisha hurusiwi kwenda kushoto.
  Labda wengine mtakosoa na kuelekeza vinginevyo
   
 5. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #5
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  tafsili nyingune ni one way
   
 6. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #6
  Dec 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hata mimi nimepita hapo na kuona utata huo, nafikiri walioweka walitakuwa wamechanganya au wamechanganyikiwa
   
 7. M

  Mutambukamalogo JF-Expert Member

  #7
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mpaka sasa hai ruhusiwi kwenda kushoto. Kwenda kulia inaruhusiwa. Alama mpya zilizowekwa hivi karibuni city center,zote hazija anza kutumika mpaka mtakapotangaziwa.
   
 8. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #8
  Dec 2, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,920
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kwa sasa fuata alama za zamani...mpaka pale watakaposema tuanze kutumia hizo mpya (in which case wataondoa alama za zamani). Alama mpya zilitakiwa kufunikwa mapaka pale zitakapoanza kutumika...tatizo wahusika inaelekea wanazifunika kwa magazeti!.....yanatoka kirahisi kwa mvua/umande/upepo na hivyo kulera tabu kwa watumiaji. Kuna siku nilizunguka sana mjini maana kiala njia niliyoizoea nilikuwa naona imewekwa one-way na kunifanya nigeuze geuze mara kadhaa kabla ya kuuliza na kupewa ufafanuzi huo.
   
 9. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #9
  Dec 2, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  No way neither left nor right!
  Sasa mbona iyo V8 ni kama imetoka left inaenda right?
  Au ndo ya wakubwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Dec 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Usiende kulia wala kushoto, nenda moja kwa moja kuelekea njia inayoingia bandari ndogo, maarufu kwa boti za kwenda Unguja.
   
 11. Ze burner

  Ze burner JF-Expert Member

  #11
  Dec 2, 2011
  Joined: Jan 5, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  alama ya mwanzo inayokuface ni kwamba kwa anayetokea kanjia haka hatakiwi kupiga L turn kuelekea kulia, alama ya pili ni kwamba hakuna njia kuelekea kushoto. hivyo basi nyooka moja kwa moja ingia bandarini na utokee kwa baharesa kule juu. zinatofautishwa na mchoro uliyokatiza katikati. wa kwanza umekatiza katika V center na wa pili umekatiza ncha na ncha.
   
 12. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #12
  Dec 2, 2011
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  tazama kama ifuatavyo

  kutakuwa na njia inakwenda kushoto na nyingine inakwenda kulia, imeanza ya kwenda kulia , halafu inafuata inayokwenda kushoto, hizo zote zipo karibu sana, lakini hazipo pahala pamoja.
  sasa:
  amri inasema usipinde kulia, na mara baadaye usipinde kushoto. hizo amri zipo sawa. nasema hivi kwasababu wengine wanaweza fikiri kungekuwa na ile ya nenda moja kwa moja. lakini kumbuka hizo njia za kushoto na kulia hazipo kwenye makutano sawa, hivi kusema moja kwa moja kungechanganya watu , kwani baada ya kuvuka ya kwanza mtu angehisi mwisho wa nenda moja kwa moja. ndiyo maana umewekewa zote, kwanza usiende kulia, na baadaye unaambiwa usiende kushoto
   
 13. Wisdom

  Wisdom JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 473
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi vibao ni vingi sana na viko karibu katika kila barabara ya katikati ya jiji, mamlaka husika zituambie basi badala ya kuviweka na kukaa kimya!
   
 14. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  ukiangalia kwa makini utaona kuwa kibao cha kwanza kinachokataza usiende kulia ni kama vile kilikuwa kimezibwa na karatasi halafu likachanika labda kutokana na mvua,upepo n.k, ila kibao kinachofuata, cha pili(usiende kushoto) hakidhihirishi kama kilizibwa, kwa mantiki hiyo kibao cha kwanza hakitumiki bali cha pili yaani utaratibu ni kama awali, USIKATE KONA KWENDA KUSHOTO!
   
 15. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #15
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu ni uhuni, wanafikiri kuwa barabara zetu zinatumiwa na watanzania pekee? jamani tutaacha lini ubabaishaji kila sehemu! kama hazitakiwa kutumika sasa iweje zimewekwa sasa si wangeweka muda huohuo zinzpotakiwa kutumika?
   
 16. L

  Leliro Member

  #16
  Dec 3, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kinachotuumiza hapa ni tenda za kutengeneza hivyo vibao. Inasikitika sana toka miaka hiyo toka hii barabara imekuwa one way bila uchafu huu na sasa mahitaji ndo yamepatikana. Ikumbukwe kuwa kuna watu wa mikoani nao wanakuja jijini na wanachojua kuwa alama za barabarani kadri walivyojifunza zinaonya, zinakataza na zinaruhusu - basi! sasa unapoweka madowido haya utawachanganya sana wageni toka miji mingine na matokeo yake ni ajali au msongamano wa magari. Huyu alieleta manunuzi ya tender ndo alietuua. Isitoshe hata afisa aliedesign vibao hivi wakati vinawekwa hajawahi kufika hapo. Mtu wa tender pamoja na kuwa na cheti cha ujuzi anaetengeneza na kusimika ni kjana kama amemaliza drs VII basi ni bahati. Kijana anaetaka amalize kazi yake aondoke. Hii ni hatari sana
   
Loading...