Jamani,
Leo hapa D'Salaam nimepita Bridge street. Wasiofahamu majina ya mitaa hii ni kwamba ni ule mtaa ambao ukiwa unaelekea baharini unapita katikati ya iliyokuwa Forodhani Secondary ikiwa kushoto na Kanisa Katoliki la Saint Joseph linakuwa upande wako wa kulia.
TUmezoea kwamba ukifika hapo unakutana na Sokoine Drive ambayo kwa miaka mingi ni One Way Street na hivyo kuna alama inayokukataza kupiga kona kuingia upande wa kushoto na hivyo unalazimika kupiga kona kungia kulia.
Leo nilipofika hapo nikaona imeongezeka alama inayofanana na ile lakini inaonekana kama nakataza kupga kona kuingia kila!
Hivyo, kuna alama mbili sasa, moja inakataza kuingia kushoto na nyingine inakataza kuingia kulia. Nimeuliza traffic police aliyekuwepo kwa kweli haikunisaidia nikakumbuka kwamba JF kumejaa kila aina ya wataalamu hata kama mimi kuna baadhi ya mambo nimesahamu wakati ninajifunza udereva miaka 20 iliyopita.
Nilipokumbuka JF nikaona maneno hayatoshi na nikaamua kupiga picha yenye alama zote mbli kama inavyoonekana hapa.
Je, wandugu,
Mnaweza kunisaidia kwamba alama zote hizi mbili ni za nini, maana leo nimetumia dakika kadhaa ku-park gari na kutafuta ni ipi niifuate?
Saidia, tafadhali. Kuuliza si ujinga kama kusahau kusivyokuwa ujinga iwapo nimesahau.
MdogoWenu