MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,966
Nalisema hili kwa yakini ya moyo wangu kabisa tena bila kumung'unya maneno, hii ni hatari!hatari!ambayo itatutafuna baadaye na madhara yake hayawezi kuonekana hivi sasa.CCM walilianzisha hili wakati wa chama kimoja,tuko kwenye mfumo wa vyama vingi lakini bado wanaliendeleza hadi sasa.Nalisema hili humu lakini iko siku maneno yangu yatakumbukwa.
Sikatai na naelewa sana kufanya kazi na mtu unayefahamiana naye ni bora na ni rahisi zaidi kwa maana ya mawasiliano kuliko usiyemjua, lakini kuna nafasi ambazo hazihitaji ukada wala wanasiasa lakini sisi tunaangalia kua "flani ni mwenzetu lazima nisimwangushe", Kuna wasiokua wanachama wa chama chochote cha siasa wala sio wanasiasa lakini ni watendaji waadilifu na wazoefu katika idara flani, hawa ndio watendaji wazuri tena wasiokua na utashi wowote wa kisiasa! Ikumbukwe kua imani ya kisiasa haina tofauti na dini ya mtu.
Najua kukua CCM walilianzisha na hili na bado wanaliendeleza, iko siku chama kiingine kikiingia madarakani nacho kitafanya hivyo hivyo! Unajua tatizo litanzia wapi? Endapo CCM ambao walizoea kutawala muda mrefu wakawekwa pembeni halafu wapinzani wao wakagawiana vyeo kiitikadi, hapa ndipo CCM watakapoona kua wanaonewa kwa sababu hawakuzea kukaa bench huku wakisahau kua wao walikua waasisi wa utaratibu huo. Kunaweza kutokea mgawanyiko Mkubwa sana katika taifa na chuki kujengeka miongoni mwa jamii zetu.
Nimemaliza lakini hiki kitu nimekua nikikiwaza muda mrefu sana hasa KWA madhara yake tu, muda hua umazungumza na utasema.