Hizi teuzi kwa kuangalia itikadi za kichama ipo siku zitaleta matatizo makubwa

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Nalisema hili kwa yakini ya moyo wangu kabisa tena bila kumung'unya maneno, hii ni hatari!hatari!ambayo itatutafuna baadaye na madhara yake hayawezi kuonekana hivi sasa.CCM walilianzisha hili wakati wa chama kimoja,tuko kwenye mfumo wa vyama vingi lakini bado wanaliendeleza hadi sasa.Nalisema hili humu lakini iko siku maneno yangu yatakumbukwa.

Sikatai na naelewa sana kufanya kazi na mtu unayefahamiana naye ni bora na ni rahisi zaidi kwa maana ya mawasiliano kuliko usiyemjua, lakini kuna nafasi ambazo hazihitaji ukada wala wanasiasa lakini sisi tunaangalia kua "flani ni mwenzetu lazima nisimwangushe", Kuna wasiokua wanachama wa chama chochote cha siasa wala sio wanasiasa lakini ni watendaji waadilifu na wazoefu katika idara flani, hawa ndio watendaji wazuri tena wasiokua na utashi wowote wa kisiasa! Ikumbukwe kua imani ya kisiasa haina tofauti na dini ya mtu.

Najua kukua CCM walilianzisha na hili na bado wanaliendeleza, iko siku chama kiingine kikiingia madarakani nacho kitafanya hivyo hivyo! Unajua tatizo litanzia wapi? Endapo CCM ambao walizoea kutawala muda mrefu wakawekwa pembeni halafu wapinzani wao wakagawiana vyeo kiitikadi, hapa ndipo CCM watakapoona kua wanaonewa kwa sababu hawakuzea kukaa bench huku wakisahau kua wao walikua waasisi wa utaratibu huo. Kunaweza kutokea mgawanyiko Mkubwa sana katika taifa na chuki kujengeka miongoni mwa jamii zetu.

Nimemaliza lakini hiki kitu nimekua nikikiwaza muda mrefu sana hasa KWA madhara yake tu, muda hua umazungumza na utasema.
 
Najaribu kufikiria tu brains zilizobaki Chadema eti mtu kama Mmawia au Yericko Nyerere au Ben Saanane apewe ubalozi ili tu rais aonekane yuko fair japo hao jamaa wameonyesha dalili zote za gross incompetence
 
Ni madhara ya watanzania kuingia VYAMA VINGI kwa chama tawala kulazimishwa kukubali bila ridhaa yake.

Mwaka 1992 kuna vitu vingi sana walivichukulia poa madhara yake nchi inadumaa kila kitu kinategemea makada ambao wako limited kwa uwezo na idadi.
Ndio maana hata Vitu kama Economic Diplomacy Havijaleta tija maana ubalozini ni sehemu ya mapumzika kwa makada na wapambe wao.

Mfumo huo ni kivutio na kichocheo cha umasikini tanzania.
 
Naona somo halijakuingia kabisa
 
Na haya yote ndiyo yanayozaa ufisadi
 
ulitaka tumteuwe SUGU, LEMA, PROF JAY, MDEE??

MNACHEKESHA
 
Mbona wengine kutoka upinzani wakiteuliwa huitwa wanafiki aganga njaa....mfano enzi za JK Mbatia alivyoteuliwa aliitwa majina mengi.

Hapa vp mkuu?
 
Mbona wengine kutoka upinzani wakiteuliwa huitwa wanafiki aganga njaa....mfano enzi za JK Mbatia alivyoteuliwa aliitwa majina mengi.

Hapa vp mkuu?
Aliyekuambia wateuliwe makada wa vyama vingine ni nani? Kwani tuna mseto sisi? Hakuna watumishi wazuri wasiokua na vyama?
 
Najaribu kufikiria tu brains zilizobaki Chadema eti mtu kama Mmawia au Yericko Nyerere au Ben Saanane apewe ubalozi ili tu rais aonekane yuko fair japo hao jamaa wameonyesha dalili zote za gross incompetence
Mmawia awe balozi??? Labda nyumba 10.
 
ulitaka tumteuwe SUGU, LEMA, PROF JAY, MDEE??

MNACHEKESHA
Mbona hamjamteua kibajaji na profesa maji marefu kama unadhani wabunge wanateuliwa kuwa mabalozi pindi wakiwa bado Wakilisha wa majimbo,jaribu kuijongeza
 
Mbona wengine kutoka upinzani wakiteuliwa huitwa wanafiki aganga njaa....mfano enzi za JK Mbatia alivyoteuliwa aliitwa majina mengi.

Hapa vp mkuu?
Wateue na sasa mbona sasa hajateua wa ukawa? Hata JK kwenye Ubalozi alikuwa akifanya upendeleo wa ajabu.
 
Aliyekuambia wateuliwe makada wa vyama vingine ni nani? Kwani tuna mseto sisi? Hakuna watumishi wazuri wasiokua na vyama?
Mkuu nimekusoma, mm naunga mkono uteuzi wa nyadhisha zinazohitaji utaalam fulan kupewa watumishi waadilifu na wachapakazi hususan wasio na vitazamo ya kivyama ili wasaidie nchi kusonga mbele; ninakerwa na baadhi ya wenye nyadhifa na hata wasio na nyadhifa kuingiza siasa hata kwenye mambo yasiyohitaji siasa matokeo yake migogoro na kuchelewesha maendeleo
 
Tatizo pia hao ambao sio wanasiasa unawapataje kama sio kwa kuwaambukiza siasa hizohizo, pia kibongobongo ukimchukua mtu wa chama kingine ukampa madaraka inaonekana kama umekwama au unajipendekeza au unatoa rushwa au unamfanya kuwa kama msaliti wa chama chake. Tatizo la siasa za Tanzania zimejaa usisi au umimi zaidi kuliko kujali maslai ya wengi.
 
Back
Top Bottom