Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 464
- 687
Katika maisha yangu yote ya kusoma sayansi ya biologia, hakuna topic ambayao mpaka sasa nimeshindwa kuielewa kama EVOLUTION. Hii ndio topic inayojaribu kuaminisha watu kuwa ulimwengu na viumbe vyote vilitokea tu spontaneously na vimekuwa vikibadilikabadilika kuwa vilivyosasa. Huu upuuzi unapofundishwa, hata ukimtazama usoni mwalimu anayekufundisha, unaona kabisa naye hakiamini anachokufundisha.
Tutafakari; kama vitu kama magari, nyumba, simu na hata viti tunavyokalia, havitokei tu hivi hivi, lazima visanifiwe kwa ubunifu mkubwa na kuundwa kwa ustadi wa hali ya juu, iweje mtu, kiumbe mwenye akili, maarifa na ubunifu wa ajabu namna hii tuamini alitokea tu sijui kutoka kwenye mamyani?
Natumia mfano huu wa EVOLUTION kutathmini yanayoendelea CHADEMA. April 9, mwenyekiti wake alikamatwa akafunguliwa kesi ya UHAINI, May 13 msajili katengua uteuzi wa Sekretariat ya CHADEMA, Mei 27 Msajili kasitisha ruzuku, June 10 mahakuma kuu imetoa amri ya kusitisha shughuli zote za CHADEMA.
Kila nikijaribu kudhani ni mazingira gani yanayoweza kupelekea kadhia zote hizi kuikumba CHADEMA kwa wakati mmoja in such a coordinated manner? Moyo wangu unaniambia EVOLUTION is a LIE. Unahitaji imani ya kuhamisha milima kuamini kuwa matukia makubwa manne kukishambulia chama kimoja yanaweza kutokea spontaneously bila kuratibiwa. Kwa vyovyote vile, kuna mtu au watu nyuma ya hizi kadhia za CHADEMA.
Swali linabaki ninani anayeratibu mpango wa kuhujumu CHADEMA, na ananufaikaje? Je, ni Lembruce Mchome aliyeishtaki CHADEMA kwa msajili? Au ni Saidi Issah Mohammed, Ahmed Rashid na Maulidah Anna Komu walioishtaki CHADEMA mahakamani? Ni Mbowe, maana wote wanaotajwa ni waliomuunga mkono? Ni dola na vyombo vyake au ni wote hawa niliowataja?
Bila kujali nani anahusika na madhila haya ya CHADEMA na ana nia gani, nadhani sote tunakubaliana kuwa hujuma dhidi ya vyama vya siasa zinaua Demokrasi. Siasa zetu zinakuwa na radha pale CCM tunaposhindana na upinzani wenye nguvu, sio huu wa CHAUMA!