Hizi shangilia shangilia za watu kwa Rais nimezishtukia!

Kuna vitu vinashangaza ni lazima ufanye uchunguzi binafsi.

Mfano si ajabu kwenye kampeni hizi za udiwani ccm kumleta Dr Luis wa Lugumi ili ipate watu wa kuwasikiliza porojo zao kwenye mikutano.

Kama 2015 walileta fisi kwenye kampeni itakuwaje issue kumleta le Dr Kamata? Sema umefanya kosa moja kubwa hapa kuwasanua so hawatamleta tena huyo mzee na kwa hilo umempotezea ulaji mkuu next time think twice.
 
Ch

Chadema na Lowassa wakishangiliwa ni sahihi. Mheshimiwa Rais Magufuli akishangiliwa kuna kitu, Mkuu huyu Mheshimiwa Rais Magufuli amejikitaa sana kwa watu wa chini kwahiyo usitegemee kama mipango inapangwa ashangiliwe.
Hujajibu hoja ya msingi, kubomolewa kwa jingo la umma ni swala la kushangiliwa? na kwa nini washangiliaji wako katika kundi moja lililojitenga eneo? tuache usanii kwenye mambo ya msingi. Mbembe hizo zinafanyika wakati wa uchaguzi sio katika kutimiza majukumu ya taifa
 
Kijijini kwetu kulikuwaga na taahira moja linaitwa Gwanchele,, sasa watoto (wakati huo) tukawa tumelijulia kwa vile lilikuwa bingwa la kuruka "samasoti" (Somersault), tukiliona tu tunaanza kulishangilia kwa nderemo na vifijo. Siku moja bwana likawa limesimama kwenye kifusi cha mawe ya kujengea daraja, vijana wakaanza tena kulishagilia kama kawaida, bwana eeeeh, Gwanchele akapiga "samasoti" hapo hapo kwenye mawe kilichomkuta sitaki kusimulia (maana hapa nilipo machozi yananitoka). Sasa hii inanikumbusha kwamba wananchi tuangalie na maneno ya kupigia nderemo na vifijo, miongoni mwetu kuna mataahira ingawa yanavaa suti, sasa kuna siku yatakuja kuamua kitu ambacho hatutakaa tusahau kwa vile tu yamepandisha mzuka kama jamaa yangu "Gwanchele"

Gwanchele! ha ha ha hah ah
 
Siasa ni kama mieleka! Adui anapoangushwa, usually watu wa upande mmoja watashangilia kwa sababu sitting arrangement huwa zinataka mashabiki wa timu hii wakae upande mmoja na mashabiki wa timu pinzani wakae upande mwingine.
Kwa hiyo ile ilikuwa kama mieleka. JPM kamdondosha hasimu wake (jengo la TANESCO) So mafans wake lazima washangilie shujaa wao katwanga ngumi mpinzani!
Au we huangaliagi michezo?

Professional-Wrestling-1.jpg

Pichani! JPM akilitwanga jengo la TANESCO kwa pigo moja takatifu! Mashabiki washangiliaji (wanaonekana kwa mbali) wakimwangalia kwa umakini JPM akifanya vitu vyake!
kuna kitu jana nimeicheki inaitwa BOYKA Undisputed ni nomaaaaa
 
Niekumbuka wimbo mmjoa wa zamaniuliimba hivi:

Bomoa eh! Bomoa maama tutajenga kesho!
Bomoa eh! Bomoa maama tutajenga kesho!
Ima ima
Bomoa eh! Bomoa maama tutajenga kesho!
 
Nilikuwa naangalia clip ya mheshimiwa kwa sana.
Kwenye clip hiyo zilisikika sauti zikishangilia kila alichoongea mheshimiwa, nikawa najiuliza wanashangilia nini? Au sisikii vizuri anachoongea mheshimiwa? Nika-replay ile clip, kwa kweli maneno yaliyozungumzwa na mheshimiwa na kupelekea wale watu washangilie ni ya kawaida sana!! Na mengine kwa akili tu ya kawaida, si ya kushangilia. Mfano, naagiza jengo hili na hili liangushwe....eti watu wanashangilia!! Sasa jengo kuangushwa ni jambo la kushangilia kweli? Wanashangilia ili iwe nini?

KOSA LA KIUFUNDI:
Ukiangalia kwa umakini ile clip, utagundua watu wanaopiga kelele kwa maana ya kushangilia wanapatikana sehemu moja au ni kusanyiko la watu wanaopatikana sehemu fulani aidha kusini, mashariki, magharibi au kaskazini. Yaani ni kusanyiko la watu limemzunguka mheshimiwa, lakini wanaoshangilia wanakuwa sehemu moja tu.

Yaani hawa jamaa kila kitu wao ni kuchemsha tu, sijui huwa hawapati muda wa kufanya mpango wa muda mrefu.
cc ile clip ya arusha ambayo alishhangaa aliowalipa wamshangilie wametimka akaishia kuwatukana kuwa ni wapumbavu kabisa :D:D:D:D:D
 
sasa mtu anaenda kusimama katikati ya barabara na kuwaambia watu eti weka X hapa kwenye hili jengo full foleni tu anasababisha huyu mzee au ndo kusema wenzie nao hua wanafanya haya?mtu anashindwa kujali muda wa wenzie wanatoka na kwenda makazini yeye anakalia kujitengenezea vivituo na kusema kasimamishwa duuuh washangiliaji hongereni next time waambieni wawaletee na msosi kabisa hapohapo kazini kwenu
 
Back
Top Bottom