Hizi noti ni mbovu!

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Watanzania tufikeni mahali tuwe wa kweli na tumuogope Mungu kudanganya peupe. Binafsi yangu nimeona noti nyingi niliona noti ya brown ya shilingi 5, nimeona 100 ya Mmasai mpaka noti za sasa. Sijawahi kuona noti mbovu kama hizi. Ukisikiliza kila mmoja analalamikia ubora wa noti hizi. Hii si mbaya sana, mbaya zaidi ni majibu ya Benki Kuu. Wanasema tatizo ni jinsi tunavyozitunza kama vile hizi noti za kwanza kuwa nazo, haya ni maneno ya kihuni. Wanakuwa wakali kutetea uozo uliofanyika ambao huhitaji kuwa mtaalam kujua zimechakachuliwa. Sijawahi kuona noti inafumuka naiona sasa. Wakati zinatoka walituambia hizi zimetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa zaidi na hazitaweza kugushiwa. Mara tukaanza kusikia watu wanalia kwani ghafla feki zilizagaa kila mahali. Wanageuka wanatuasa kusema ili usibambikiwe feki chunguza special features moja iangalie noti kwenye jua utaziona, au hata unuse. Hapa unachukia na kutaka kupasuka kwani unaambia ufanye kisichowezekana- yaani umelipwa millioni yako pale kariakoo utoke dukani ukae pale nchi uanzee kuangalia juani noti mojamoja ndiyo ukimaliza umpe bidhaa mteja huyu. Jamani hivi viongozi wetu hamlioni hili? Mmeshindwa kabisa kuona kuwa tumeibiwa katika tenda hii na hivyo tuachane nazo, tuzibadili noti hizi na safari tuwe makini? ningeongeza kusema tuwawajibishe waliohusika lakini wewe na mimi tunajua hiyo ni ndoto ya mchana. All in all these are the worst notes we have ever had in Tanzania.
 
Tanzania bila ufisadi inawezekana. Ukishangaa mambo ya TANESCO unageuka na kukumbana na ufisadi wa BOT.
 
Tanzania bila ufisadi
inawezekana. Ukishangaa mambo ya TANESCO unageuka na kukumbana na
ufisadi wa BOT.

mramba na ballali pamoja na tuhuma zao za ufisadi walitoa noti zenye viwango kuliko hizi za mkulo na ndulu.
 
nyie mnaweka hela kwa chu+@ halafu unategemea itakuwa vilevile?itunze noti ikutunze....
 
nyie mnaweka hela kwa chu+@ halafu unategemea itakuwa vilevile?itunze noti ikutunze....
Joy ingekuwa shida ni hiyo ingeonekana na noti ya sh 5 nafikiri wakati huo hata bank zilikuwa chache acha muamko wa kuweka pesa bank - tuwe wakweli tumeingizwa mkenge wamepiga cha juu.
 
Waambie Padri Slaa Mchungaji Natse na Mchungaji Msigwa watengeneze noti zao tuzione kama zitakuwa bora
 
Hasa noti ya shilingi 500 ndio balaa zaidi, hizo zingine wawezaziombea 'foo' kwanza!
 
Kinachoshangaza hawataki kuondoa noti za zamani. Bado wanatoa noti za zamani mpya, kwa nini?
 
Member Array


Join Date : 31st July 2012
Posts : 39
Rep Power : 308
Likes Received5
Likes Given1


[h=2]
icon1.png
Re: Hizi noti ni mbovu![/h] Waambie Padri Slaa Mchungaji Natse na Mchungaji Msigwa watengeneze noti zao tuzione kama zitakuwa bora
 
halafu noti zenyewe zilichapishwa kipindi cha uchaguzi..na kipindi hichohicho tulishuhudia jk akitumia helicopter 3,mabango expensive hadi vyooni,ridhiwan na mama yake wa kambo wakimwaga mahela kila mkoa waliopita...TIT=this is tanzania
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom