Hizi ni Sababu kwanini Scotland Yard na FBI hawana uwezo wa kuchunguza Kushambuliwa Tundu Lissu

Habarini wanajamvi. Kufuatia Tundu Lissu kumiminiwa risasi na Watu wasiojulikana, kumekuwa na madai kadhaa kuwa pengine nchi (TZ) iitishe uchunguzi huru wa kuwabaini wahusika wa tukio hilo kutoka kwa vyombo vingine vya kiuchunguzi kutoka nchi za kigeni hasa Scotland Yard ya Uingereza au FBI ya Marekani.

Kwa mtazamo wangu Scotland Yard ya Uingereza na FBI ya Marekani hawana uwezo wa kuchunguza kubaini wahusika wa mashambulizi dhidi ya Tundu Lissu. Sababu ni hizi zifuatazo:

1. FBI hadi leo wameshindwa kubaini Urusi iliwezaje kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani hadi kudictate matokeo ya uchaguzi huo, bila wao kubaini jambo hilo na kulizuia mapema.

2. FBI hadi leo hawajatuambia ni nani alimuua Rais John F Kennedy.

3. Hadi leo Scotland Yard hawajatuambia ni nani alimuua Princess Diana.

4. Scotland Yard, hadi leo hawajatuambia kwanini hawakuzibaini mapema athari za Uingereza kujiunga na Umoja wa Ulaya hadi miaka kadhaa imepita ndipo Uingereza inahaha kujitoa EU.

Tukielezwa na kupatiwa majibu ya mikanganyiko hiyo, nitakuwa wa kwanza kuunga mkono ujio wa hao Watu, vinginevyo ni mjambo tu kama ilivyo mijambo mingine ya wanasiasa uchwara.

Uchunguzi huru, una mawili.Moja kuyasema ambayo siyo, na la pili, kuyasema ambayo ndiyo.Kwa nini, wapo wa upande ule wa kulalamika, watapenya kwa namna moja ama nyingine kwa uchunguzi huo wa huru waonekane nao ni wahusika waweze kulazimishia report iwe YES, Hususani na wale wa kulalamikiwa, watapenya pia, na kulazimisha report iwe NO, kosa ukishasema, upelelezi HURU, alafu mbaya kabisa ni kutoka nje, ni hivi lazima information zianzie kwa makundi mawili, walalamikaji,ama mtuhumiwa, sasa hapo ndiyo kuna kupenya kwa watu ili kulazimisha taarifa.Mimi ni mtazamo wangu. Ushauri , tuiache serikali ifanye kazi
Mkuu waliomo humu hawatajibu hoja zako zaidi watakutukana wewe na wote unaomini ni watendaji bora kwa Taifa hili...
wao wamekalilishwa kuwa kila akisemacho malaika wao Mh Mbowe ni sahihi kwa asilimia 200 kuondoa huo uozo wa mawazo yao wataikuita Bwege, taahira, hujitambui, lumumba, na mengineyo mengi...
swali ni je hao wachunguzi wa Nje ambao mwenyekiti wao amewasiliana nao, FBI, CIA,Scotlanda Yard, na wengineo amewasiliana nao kama nani? Je Taasisi hizo hazifanyi kazi kwa kushirikiana na Utawala wa Nchi zao?
 
Sawa, lakini kumbukeni Wasijulikana ni watu, msilazimishe Upande ule utengeneze wasiojulikana wao, hapo ndipo mtajua matukio mnayoyafanya sio mazuri,

Nyinyi ni Binadamu mna akili, na wale ni Binadamu wana akili

Kuweni Makini na majubu yenu

Wasiojulikana, ndo hao wanaweza kujiingiza sehemu zote, hata kwenye uchunguzi huru, sisi tunaweza kusema uchunguzi unafanywa huru kumbe kuna Kuna watu wamejiingiza kwa msaada fulani, matokeo yake hayatakua na mazingira mazuri sana.
 
Mwambie huyo boya mwenzio hapo juu hao FBI walishindwa kumpata muuaji wa J.F. Kennedy kwa kuwa alikuwa amekufa, lakini Lissu yupo hai wataweza.
Farasi huyo hasomi historia kuwa muuwaji wa JFK alikamatwa? Lakini bahati mbaya alikufa kabla hajatoa maelezo ya kutosha? Waache ujinga vyombo vyetu vimefanikiwa lipi katika haya
= viloba vya maiti
= Mawazo
= Roma
= Saanane
= Ulimboka
Na mambo mengi yenye utata hayana majibu halafu tuwaamini kwa lipi?
 
Si ushabiki tuu wa BAVICHA kama CIA, NSA,FBI, SWATS walindwa kubaini aliyemuua JFK wataweza hili?
Sio kweli. Jambo lolote matokeo yake hutegemea na mlaji wa mwisho. Namaanisha dondoo za uchunguzi wowote mara nyingi hutegemea mwisho wake nani akabidhiwe? Wanaangalia wakipublish je kwenye ustawi as jamii litakaaje? Hasa kiusalama. Try to think tank Mr/Miss.
 
binafs nnashangaaa sana japo sitokei uko lumumba kuwa; TL n mbunge tu inausianaje na nchi jiran ktk uchunguz coz hata wakija kina nan pasipo msaad wa wazawa n kaz bure mana mzung mpak apajue tandale c kaz ndog isitoshe sio tukio la kitaifa hilo
 
Namshangaa mleta Uzi, sijui in huyu Majid mjengwa au ni mjengwa yupi? Majid huwa anafanya uchambuzi mzuri sana.
Kinachokataliwa ni vyombo vya serikali kufanya uchunguzi kwa sababu serikali iliyowaajiri inatuhumiwa. Hawapo huru kuchunguza mwajiri wao. Tunataka wachunguzi huru. Kama siyo FBI au Scotland basi pendekeza wachunguzi wasiofungamana na serikali.
 
binafs nnashangaaa sana japo sitokei uko lumumba kuwa; TL n mbunge tu inausianaje na nchi jiran ktk uchunguz coz hata wakija kina nan pasipo msaad wa wazawa n kaz bure mana mzung mpak apajue tandale c kaz ndog isitoshe sio tukio la kitaifa hilo
Kwn umeambiwa wakija hao wageni watakosa ushirikiano na wazawa? au wetu wamekosa ushirikiano na wazawa?tatizo lililopo ni kua hao waharifu wapo kwa IGP wanakunywa nae chai na kupiga nae story so hata iwe vipi hawawezi kukamatwa na wafanya kazi wenzao
 
Habarini wanajamvi. Kufuatia Tundu Lissu kumiminiwa risasi na Watu wasiojulikana, kumekuwa na madai kadhaa kuwa pengine nchi (TZ) iitishe uchunguzi huru wa kuwabaini wahusika wa tukio hilo kutoka kwa vyombo vingine vya kiuchunguzi kutoka nchi za kigeni hasa Scotland Yard ya Uingereza au FBI ya Marekani.

Kwa mtazamo wangu Scotland Yard ya Uingereza na FBI ya Marekani hawana uwezo wa kuchunguza kubaini wahusika wa mashambulizi dhidi ya Tundu Lissu. Sababu ni hizi zifuatazo:

1. FBI hadi leo wameshindwa kubaini Urusi iliwezaje kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani hadi kudictate matokeo ya uchaguzi huo, bila wao kubaini jambo hilo na kulizuia mapema.

2. FBI hadi leo hawajatuambia ni nani alimuua Rais John F Kennedy.

3. Hadi leo Scotland Yard hawajatuambia ni nani alimuua Princess Diana.

4. Scotland Yard, hadi leo hawajatuambia kwanini hawakuzibaini mapema athari za Uingereza kujiunga na Umoja wa Ulaya hadi miaka kadhaa imepita ndipo Uingereza inahaha kujitoa EU.

Tukielezwa na kupatiwa majibu ya mikanganyiko hiyo, nitakuwa wa kwanza kuunga mkono ujio wa hao Watu, vinginevyo ni mjambo tu kama ilivyo mijambo mingine ya wanasiasa uchwara.
Hayo yote walioshindwa waliyafanya wao, wale yasiyowahusu uone kazi yao?!
 
Huwezi kulinganisha mataifa yenye watu timamu na taifa lenye matahira hapa hata Mimi nikifanya uchunguzi nitajua
 
Back
Top Bottom