MJENGA
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 884
- 848
Habarini wanajamvi. Kufuatia Tundu Lissu kumiminiwa risasi na Watu wasiojulikana, kumekuwa na madai kadhaa kuwa pengine nchi (TZ) iitishe uchunguzi huru wa kuwabaini wahusika wa tukio hilo kutoka kwa vyombo vingine vya kiuchunguzi kutoka nchi za kigeni hasa Scotland Yard ya Uingereza au FBI ya Marekani.
Kwa mtazamo wangu Scotland Yard ya Uingereza na FBI ya Marekani hawana uwezo wa kuchunguza kubaini wahusika wa mashambulizi dhidi ya Tundu Lissu. Sababu ni hizi zifuatazo:
1. FBI hadi leo wameshindwa kubaini Urusi iliwezaje kuingilia uchaguzi mkuu wa Marekani hadi kudictate matokeo ya uchaguzi huo, bila wao kubaini jambo hilo na kulizuia mapema.
2. FBI hadi leo hawajatuambia ni nani alimuua Rais John F Kennedy.
3. Hadi leo Scotland Yard hawajatuambia ni nani alimuua Princess Diana.
4. Scotland Yard, hadi leo hawajatuambia kwanini hawakuzibaini mapema athari za Uingereza kujiunga na Umoja wa Ulaya hadi miaka kadhaa imepita ndipo Uingereza inahaha kujitoa EU.
Tukielezwa na kupatiwa majibu ya mikanganyiko hiyo, nitakuwa wa kwanza kuunga mkono ujio wa hao Watu, vinginevyo ni mjambo tu kama ilivyo mijambo mingine ya wanasiasa uchwara.