Hizi ndoto zinanitesa sana jamani

Hizi ndoto zinanitesa sana jamani

Pole sana.

Ndoto mara nyingi hutumia ishara badala ya picha halisia ya mambo. Hivyo usichukulie unayoyaona ndotoni kama uhalisia bali ishara.

Ndoto za kurudi shule/mitihani zina maana moja kuu na zingine ndogo ndogo kulingana na "details" zilizopo kwenye ndoto yenyewe; wahusika pia mpangilio wa matukio.

HOFU
Shule na mitihani imechukua sehemu kubwa ya maisha ya wasomi. Wazee wa zamani walikua wakiota kuhusu kilimo na mifugo haswa haswa; mimea kuharibiwa au mavuno kiduchu pia waliota mifugo kufa ama kushambuliwa na wanyama wakali.

Ndoto za kurudi shule hususani kuingia katika chumba cha mitihani bila ukiwa umechelewa pia hujasoma hushabibia "self confidence" kushuka.

Akili huamua kutumia taswira ya shule na mitihani kwasababu ndio wakati pekee katika maisha yako ulipokuwa na hofu ya kushindwa na ndio sehemu pekee ya maisha unapokua "under pressure". Ukiwatafuta vipanga wa darasani walikua wanaongoza mitihani yote, hutokuta wanaota ndoto kama zako.

Sikudharau lakini kulingana na ndoto zako inaonyesha elimu yako ulipitia misukosuko mingi na ufaulu wako ulikua wa kati au chini ukilinganisha na matarajio yako pia "jinsi ujianavyo na kujitambua"

Hivyo ndoto zinaonyesha unapitia wakati mgumu unaokupa wasiwasi wa maisha na hofu kutokana na "mental pressures" za maisha. Na jinsi ya kuzishinda/kubadilisha ndoto hizo ni mtizamo wako wa maisha. Ongeza kujiamini, jichanganye na watu pia punguza mitazamo hasi ya maisha (kuwa optimistic) maana hizo ndoto zinasema wewe ni pessimist.

Labda kama unajiuliza nikupe jibu, waliokua wakiongoza darasani hususani kwenye mitihani huwa na ndoto tofauti zinazowasumbua ukilinganisha na walio chini. Kwasasa "your concern should be that of yourself not others" maana nikikwambia wanachoota utashaanga zaidi na kuuliza kwanini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naweza kusema that's the truth ! Nilivomaliza chuo 2017 nilivoingia tu mtaani hzi ndoto ziliniandama Sana na nilihangaika kupata utatuzi! Ila katika kutafuta utatuzi unaweza ukajiingiza kwenye Mambo ya ushitikina pia! Namshukuru mungu hzo ndoto ziliisha ila kwa maaelezo ya huyu mkuu ndo nimejua kwann Kila cku zilikuwa ndio ndoto zangu!
 
Naweza kusema that's the truth ! Nilivomaliza chuo 2017 nilivoingia tu mtaani hzi ndoto ziliniandama Sana na nilihangaika kupata utatuzi! Ila katika kutafuta utatuzi unaweza ukajiingiza kwenye Mambo ya ushitikina pia! Namshukuru mungu hzo ndoto ziliisha ila kwa maaelezo ya huyu mkuu ndo nimejua kwann Kila cku zilikuwa ndio ndoto zangu!
Mkuu toa maelezo kidogo ilikuwaje kipindi unaota ukirelate na hapa.
Mambo yako yalikuwa hayaendi au nin? Na ulitumia njia gani kutatua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom