Hizi ndizo tabia za Kenge na Mamba

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,701
71,034
1. Kenge
Kenge na mamba wanafanana sana kwa mambo mbalimbali, Kenge hupendelea kula wanyama wadogo wadogo, mayai ya ndege na mamba, na wadudu wa aina mbalimbali. Kwa umbile Kenge ni mdogo ukimlinganisha na mamba, Kenge hawezi kupigana na mamba na mara zote wakikutana Kenge hukimbia, lakini jambo la kushangaza ni kwamba Kenge ni mmoja wa wanyama wanaoongoza kwa kula watoto na mayai ya mamba na kuleta uharibifu mkubwa sana kwenye viota vya mamba, kenge pia hula nyoka mbalimbali akiwemo koboko, huyo ndiye Kenge

2. Mamba
Mamba kwa umbile ni mkubwa kuliko kenge, kwa kawaida mamba hula samaki na wanyama wa aina mbalimbali, mamba ni mkatili sana na hata ukimuangalia anapokamata au kumla mnyama utagundua ni mkatili sana, lakini pamoja na ukatili wake wote huo ni mara chache sana mamba kuweza kumkamata Kenge.

Mtazamo wangu ni kwamba Kenge ni Kenge tu hata akinenepa vipi, na mamba ni mamba tu hata akiwa amekonda sana, usije ukajaribu kumgroom Kenge awe kama mamba ni kazi bure
 
Umetumia fasihi kali sana mkuu, sijakupata!
 
Hahahahhaaaa Kenge ni kenge tu, kenge anaujua mchezo vizuri ana akili na anatumia mbinu stahiki, mamba anaringia mwili na nguvu. hahahaha Asante Mpwa you made my day
 
Back
Top Bottom