Hizi ndizo kazi za vyama vya siasa

Nzelu za bwino

JF-Expert Member
Jan 12, 2020
376
450
Salaam wanajamvi,

Tukiwa tunaendelea kupambana vita dhidi ya kirusi Covid 19 au Corona, nimeona tukumbushane kidogo baadhi ya kazi za vyama vya siasa pamoja na asasi zisizo za kiserikali.

Pamoja na mambo mengine kazi za vyama vya siasa ni pamoja na kuelimisha wananchi juu ya haki za binadamu, kutetea uhuru wa wananchi, kuhamsisha wananchi kuhusu suala lolote lenye maslahi kwa wananchi, kulinda na kutetea afya za wananchi. Nk.

Katika hii vita ya kupambana na Covid 19 isiyozalisha wakimbizi ni muhimu sana kwa kila chama cha siasa, asasi zisizo za kiserikali kutumia nguvu na ushawishi uleule wa kila siku kuhamasisha na kuelimisha wananchi juu ya madhara ya Covid 19. Najua kwa pamoja tunaweza.

Nawaomba viongozi wote wa vyama vya siasa ikiwezekana wakutane ili kuweka mkakati wa pamoja namna ya kupambana na hili gonjwa.

Asasi zisizo za kiserikali nazo kwa nafasi yake zijitahidi kuwafikia wananchi kwa njia zilezile wanazotumia kuwafikia wakati wa kutetea haki zao zinazo husu masuala mbalimbali.

Lengo letu kama taifa liwe moja tu, kutokomeza Covid 19.

Nawasilisha.
 
Umoja katika suala hili ni muhimu lakini kwa bahati mbaya tuna kiongozi ambaye amepandikiza chuki miongoni mwetu kwa hiyo mapigano yanaweza kuwa magumu.
 
Back
Top Bottom